Mch. Msigwa: Jeshi ni la Wananchi, mmeumbuka kama wachawi. Yule kiongozi wa CCM amesema maaskari wote waliosimama hapa, eti ni mali ya CCM

Mch. Msigwa: Jeshi ni la Wananchi, mmeumbuka kama wachawi. Yule kiongozi wa CCM amesema maaskari wote waliosimama hapa, eti ni mali ya CCM

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mchungaji Peter Msigwa amesema mfumo wa vyama vingi unahitaji kuwepo kwa uhuru wa mawazo na nafasi ya wananchi kuikosoa serikali bila kuhusishwa na usaliti au mapinduzi. Akizungumza katika Mkutano, Msigwa amedai kuwa kuna viongozi wanaona kuikosoa CCM ni sawa na kukosa uzalendo, huku akisema hali hiyo inasababisha kulindwa kwa watawala badala ya nchi.

Amesisitiza kuwa CHADEMA imekuwa ikitumia hoja na mawasiliano ya kisiasa badala ya kuitisha kumwagika kwa damu, akilalamikia matumizi ya nguvu dhidi ya wanaotoa hoja na kuandamana. “Jibuni kwa hoja,” amesema, huku akitaka vyombo vya ulinzi vitimize wajibu wa kuwalinda wananchi badala ya kuwajibika kisiasa kwa viongozi.

 
Back
Top Bottom