Mleta mada hueleweki na wala huelewi mantiki nzima ya utumishi kufanya usaili kabla ya kuajiri. Sikulaumu sana kwa sababu hujazoea kusailiwa kwenye kuomba ajira.
Wewe jua tu, waombaji wa ajira wenye sifa ni wengi na nafasi ni chache, hivyo namna ya kuchuja ni kuandaa usaili ili wale bora zaidi tu wachukuliwe.
Sasa usilazimishe waombaji wote nchi nzima wapimwe sawa sawa kwa aina moja tu ya mtihani iwe wa kuandikwa au kujieleza.
Wewe omba ajira, nenda kwenye usaili, mwisho wa siku walio bora zaidi kwenye kundi lenu mlioasahiliwa ndio watakuwa wamepata ajira.
Maisha hayajawahi kuwa fair popote pale, japokuwa sekretari ya ajira wanajitahidi kuwa fair.