Mchakato wa ajira za ualimu mwaka 2025 si wa haki, umekaa upendeleo

Database inayotumika ni ya Nani?

Usahili upi unatumika kuona kama walifaulu sawa?

Kwanini hawakupangiwa vitu kuona nafasi zilizo bado wazi?
Ndugu yangu naona suala la uelewa ni gumu sana kwako.
Kama ww n mwalimu bc sitoshangaa ukiwa unawapiga mawe utumishi.
 
Basi ungekosa swali moja tuu bwashee πŸ˜€πŸ˜€, kwanini kuna "0" inamaana hata swali moja limeshindikana kweli
 
FACT , hata mm bila PSRS nisingepata kazi goverment.
PSRS wapo fair 100%.

Na interview ziendelee kuwepo maana ndio njia pekee ya kupata watumishi wenye uwezo.
 
Mleta mada hueleweki na wala huelewi mantiki nzima ya utumishi kufanya usaili kabla ya kuajiri. Sikulaumu sana kwa sababu hujazoea kusailiwa kwenye kuomba ajira.

Wewe jua tu, waombaji wa ajira wenye sifa ni wengi na nafasi ni chache, hivyo namna ya kuchuja ni kuandaa usaili ili wale bora zaidi tu wachukuliwe.
Sasa usilazimishe waombaji wote nchi nzima wapimwe sawa sawa kwa aina moja tu ya mtihani iwe wa kuandikwa au kujieleza.

Wewe omba ajira, nenda kwenye usaili, mwisho wa siku walio bora zaidi kwenye kundi lenu mlioasahiliwa ndio watakuwa wamepata ajira.

Maisha hayajawahi kuwa fair popote pale, japokuwa sekretari ya ajira wanajitahidi kuwa fair.
 
Sasa waliomaliza muda mrefu nyuma walikuwa wamekaa nyumbani wanasubiri kuajiriwa serikalin, ww c unaona wanalalamika ety wamepoteza muda kwenda kwenye usaili πŸ˜‚ utadhani walivyokuwa nyumbani miaka yote hy sio kupoteza muda
 
Mitihani ya utumishi mifumo wao hawajiandai watapass vipi, sawa magumashi yapo lakini linakushindaje Swali la kitenzi kivumishi, ukiulizwa masaki ya Linux utatoboa ? Bado sijaelewa kwanini mtu anapata zero kabisa
Ungekuwa umefanya mtihani hata usingesema hivyo.
 
Kama haujaelewa Kaa kimya. Hakuna anaekataa usaili Wala anaekataa wingi wa wahitimu. Tunachotaka ni usawa na haki itendeke. Eg waliomaliza let say 2015,2016,2017 wanaweza sailiwa Kwa pamoja na siyo mtu hata kitaa hajakaa afu aje afanyiwe usaili sawa na aliyemaliza 2015 hiyo ndiyo hatutaki. Tanzania ni yetu sote
 
Ungekuwa umefanya mtihani hata usingesema hivyo.
Mkuu nishawah kufanya mtihani sawa ? Yule Elias kayombo alikuwaga T.O alikuwepo hakuna aliefikisha 50, ilikuwa ya moto sana, waulize wanaofanya mitihani ya programing mkuu ni moto wa kuotea mbali, ufaulu written ufaulu practical ndio uende oral we mitihani mikiki inakutoaje jasho mkuu ? Pambana
 
Wewe ndiyo ulifail na mpenda sifa mwenzako(marehemu kayombo maana hamkufikisha hata 50%. Je, aliyepata 90% afu hajawa selected unamchukuliaje?
 
Mm najiuliza mbona watu wa afya hawakulalamika kama hawa waalimu wakati hata wao hawakuwa na usaili kama waalimu πŸ˜‚
Watu wa Afya ni wachache compared na walimu wa physics, huwezi kumskia mwl. wa physics analalamika, subiri malalamiko tena kwa wengi watakao fika oral pdf iwapite kushoto.
 
Kwann umalize chuo 2015 afu ukae kusubiri ajira serikalini, huo n upumbavu bora mkose kazi wote tuu
 
Kwa hiyo point yako ni kuwa, kigezo cha aliyemaliza chuo zamani zaidi ndio kiwe kipaumbele cha kupata ajira badala ya kutumia ufaulu wa juu katika usaili?
Wewe unadhani hiyo ndio itakuwa fair?

Waza haya maswali.
1. Utaratibu huo unaopendekeza (old graduated applicant to be first priority), kwanini utumike kwa waalimu tu na sio kwa ajira zingine za serikali kwa miaka yote iliyopita?
2. Unawezaji kutambua kuwa mhitimu wa zamani zaidi alikuwa hana ajira kabisa tangu ahitimu au kwa kipindi chote hicho cha nyuma huenda alikuwa hana interest ya ajira ya serikali?
3. Kwanini usiwaze kuwa mhitimu wa zamani ni mtu mwenye uzoefu zaidi hivyo atakuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kufaulu usahili kuliko mhitimu mpya?
4. Ukimaliza kuwaza hilo la uzamani kuwa sifa, vipi utaepuka suala la uwiano wa Kijinsia, kiumri, kanda, mikoa na makabila?
 
Hicho unachokitaka (wahitimu wa zamani wapendelewe) huo ndio upendeleo, haufai.
Mchakato wa sasa haubagui mhitimu yoyote, vigezo vya msingi vyote ni sawa, yule atakayeonyesha uwezo wa juu zaidi katika usahili ndiye atakaye ajiriwa kwanza.
 
Waalimu wanaomba maji baada ya kupelekewa moto na utumishi ila hawapewi πŸ”₯
 
Mtihani wa geogaraphy haukuwa na title ya geography hii imekaaje kwa upande wako
Uzuri n kwamba ushajua n geography.
Kwahy ukiulizwa swali la geography hutoweza kujibu kwa sababu somo halijaandikwa?
 
Ndugu yangu una cheo gn kwenye umoja wenu wa NETO? πŸ˜‚
Au ww ndo yule jamaa aliyekuwa anabwabwaja pale mkutanoni πŸ˜‚
 
Yn mtu amekaa kitaa tangu 2015 kusubiri ajira ya Ualimu afu unakuja kupambanishwa na aliyemaliza juzi πŸ˜‚ kosa n lako ww uliyemaliza 2015
Utumishi shikilieni hapo hapo, msiachie, hakuna ajira bila usaili πŸ”₯
 
Hicho unachokitaka (wahitimu wa zamani wapendelewe) huo ndio upendeleo, haufai.
Mchakato wa sasa haubagui mhitimu yoyote, vigezo vya msingi vyote ni sawa, yule atakayeonyesha uwezo wa juu zaidi katika usahili ndiye atakaye ajiriwa kwanza.
Waalimu wanataka na aliyemaliza juzi juzi nae akae mtaani miaka 10 kama wao πŸ˜‚

Hii roho mbaya sijui imetoka wapi hawa ndo wanakwenda kupiga makofi wanafunzi, bora wafanyishwe usaili wapate 0% waendelee kukaa mtaani tuu kuliko kwenda kutesa wanafunzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…