Mzee Kimamingo
JF-Expert Member
- Mar 31, 2024
- 1,861
- 4,462
Uwezo wako wa Akili n mdogo mnoo yani mnoo.Saili za utumishi wewe huzijui kwa sababu yamkini wewe ni mwalimu au ni mgeni kabisa! Lakini utumishi toka ianzishwe imewafanya vijana wengi kuajirika sehemu ambazo zililikuwa hazifkiki kwa watoto masikini! Kwa hiyo hoja zako hazina mashiko kabisa! Maana wasio na ajira muda mrefu sio walimu peke yake kumekuwepo na kada zingine hawajaajiriwa toka miaka ya nyuma na wapo wengi sana! Umewahi kuona utumishi wanatangaza kazi kwa kulimit miaka ya kumaliza chuo????kwa uzoefu wangu waliomaliza miaka ya nyuma ndio wengi wanapata kazi utumishi sio kwa sababu ya upendeleo ila ni kwa sababu wana uzoefu na kazi hivyo maswali mengi wanayafaulu kwa sababu maswali yanaulizwa ya kada husika!
Kwa hiyo hoja yako kuwa wangekatia waliomaliza mwisho 2018 alafu wawashindanishe haina mashiko maana hata ukichukua wajinga 1000 ukawafanyia usaili lazima yupo atakayeongoza tu! Mimi nilidhani mtu aliyemaliza miaka ya nyuma ana chance kubwa ya kufaulu usaili kwa sababu ana uzoefu na kazi lakini pia hata kujieleza ni tofauti na mtu aliyemaliza mwaka jana!
Hoja yako kuwa wengine wanafanya usaili wa kuandika na wengine usaili wa mahojiano haina mqshiko, kwanza unaonekana wewe ni mbinafsi na una wivu sana, na inaonekana hujui lengo la mithani ya utumishi! Lengo la mithani ya utumishi ni kutafuta watu sahihi miongoñi mwa wengi!
Kazi ya usaili wa mchujo ni kuchuja watu wabaki wachache hivyo hata wakikatia 90% hawana lawama na hamna sheria inayowakataza kukatia hapo maana ni mchujo!
Kuna kada wanahitajika watu 5 wanaomba watu 10 wewe unahisi kuna haja ya kuwa na mthani wa mchujo au written?????? Lakini wanahitajika watu 5 wanaomba watu 1000 plus utawapataje sasa hao watano lazima utumie hizo njia zote! Mchujo, prct nk ili ubaki na wachache ili uhojiane nao! Hiyo application ipo pia kwenye topic za geography walimu mlitufundisha alafu nyie wenyewe hamtaki kufanyiwa!
Tuache malalamiko yasiyo na maana mtoto wako anaposoma mwambie asome kozi ambazo hazina ushindani mkubwa sokoni! Haiwezekani mwalimu kakomaa na madynamic na principle za newton unataka ulingane naye wewe uliyesoma mambo ya ngoswe na mìchomekeo kibao! Tuache utane
Jinsi unavyosoma kozi ngumu na yenye watu wachache hata kwenye usaili ipo hivyo hivyo! Kuna kada wasailiwa wanaitwa watano na wanahitajika 4 hadi raha sana!
Kozi yangu iliyonipa ajirà, walikuwa wanahitajika watu wawili na tulioitwa usaìli tulikuwa watano tuliofika siku ya usaili tulikuwa 4! Wakati pembeni unaona kada nyingine wanahitajika 2 walioitwa usaili 200+ wewe unafikiri kosa la nani hapo???
Tuwe wazalendo! Utumishi wapo fair 100%
Kwa maswali yanayoulizwa Utumishi unadhani yana Mfavor aliyemaliza zamani au karibuni.