Mchakato wa ajira za ualimu mwaka 2025 si wa haki, umekaa upendeleo

Uwezo wako wa Akili n mdogo mnoo yani mnoo.
Kwa maswali yanayoulizwa Utumishi unadhani yana Mfavor aliyemaliza zamani au karibuni.
 
Hayo ni matokeo ya waliofanya written na baadae oral interview. Je waliofanya oral interview wametumia kigezo Gani kubatilisha kufanya kwao mtihani?? Wamejuaje kama wasingepata matokeo ya hovyo au wangefanya vizuri??
Hy n written, acha wenge
 
Kaka kama umefeli mtihani acha kulia lia huku njia iliyotumika ndio sahihi kapisa na yauwazi, hakuna njia nyingne halali zaid ya hii kama wewe nikilaza ukategemea kwenda kufelisha watoto wetu umefili kabla ya kuwafelisha
Mtihani Gani huo unaouongelea?
 
Huyo jamaa unapoteza muda kujibizana nae kwa hoja huyo kaamua kukaa upande wa kuwaponda walimu kwa kila kitu kisa yeye kasomea kada tofauti na elimu
Yn nyie waalimu bhana πŸ˜‚ yn mtu akisapoti nyie kufanyiwa usaili mnaanza kumuona n adui wenu πŸ˜‚ mzee Mm sio niliyeleta usaili kwa waalimu kwahy kama unanichukia bc hayo n matumizi mabaya ya chuki πŸ˜‚
 
Tatizo kubwa mlilonalo Walimu baada ya kumaliza chuo mlibweteka kusubiri ajira za TAMISEMI hamjawahi kujihangaisha kujua habari za usaili na mbinu zake ndio maana leo kwenye usaili wa kuchujwa unategemea ukutane na swali la What is Geography.

Kuna wengine walikuja kulalamika wametolewa maswali ya form one humu.

Kuna wenzenu Miaka ya nyuma usaili wa TRA walitolewa maswali ya ripoti na Makininia na watu walipasua leo wapo kazini.

Kifupi Walimu mnatakiwa mjue ukiitwa usaili jiandae sana na umuombe sana Mungu wako.

PSRS ni kimbilio la watoto wasio na connection leo watu wameajiriwa sehemu ambazo hawakuwahi kuwaza kama watapata huko nafasi.

Malalamiko hayajawahi kuwa solution hata siku moja, Mtu anaenda kwenye usaili anapata ZERO (0) maana yake huyu hajui chochote kinachoendelea kwenye hii Dunia sasa atamfundisha mtoto wa nani?

Badirisheni Mtazamo wenu mjue Dunia ya leo Ajira ni ushindani sio za bure tena.
 
Kama huna Cha ku comment Bora uache tu mkuu. Unajua unatia hasira kiasi Gani??
. MIMI mwenyewe nilipita huko huko utumishi na nikatoboa mkuu...

. Yawezekana unahasira kwa sababu imesoma NOT SELLECTED, yani walimu usaili mmoja tu makelele kibao, kuna watu wameanza kukandwa tangu 2017 huko!!!

1. Kukandwa ni lazima mkuu
2. Not selected utaziona sana kwenye pdf mkuu
3. Sitakubali Mtoto wangu afundishwe na mwalimu aliye score zero kwenye usaili..
 
Safi sana
 
Badirisheni Mtazamo wenu mjue Dunia ya leo Ajira ni ushindani sio za bure tena.
Unalaumu pasipo na kosa.., Kama Wakufunzi na Wauguzi bado hawatoshi na wapo wengi kitaa na kila mwaka kama Taifa tunatumia mapesa mengi kuwapa watu ujuzi.., Hapo issue sio wale ambao wana ujuzi na ujuzi wao unahitajika bali watunga Sera.....

By the way Ajira haijawahi kuwa Bure bali ilikuwepo kwamba inahitajika na iliweza kumpatia mtoa ajira faida na kile kidogo kumpa mfanyaji kazi, ila issue ya sasa ni kwamba Nguvu kazi sio issue tena kama zamani...; Hivyo kama dunia inabidi tuje na mfumo unaoweza kuwapa basic needs majority ya watu...

Kama walivyosema; Absolute Poverty Anywhere is a threat to Society Everywhere.... Na huko tunapoendelea kuelekea tunazidi kutengeneza matabaka ya walionacho na wasionacho...
 
Kuna uzi humu kada wa labaratory technician aliwahi kulalamika kuwa wametolewa maswali ya maabara za shule sio hospital mkaja na hoja kuwa madoctor wanalialia kisa wamezoea vya zoa zoa leo hii mnaponda na walimu the same

Kifupi nyie mnajiona mko juu sana kuliko kada zingine na mnaona walimu ni mafala na masikini basi hamjibu hoja za msingi

Nimekuuliza kwenye geogaraphy kuna swali linasema "according to elton's theory guidance and councelling should done....

Swali kama hilo huwezi kulijibu bila kumsoma huyo mtu sasa kama inatokea vyuo baadhi au programme uliyosoma haikuwa na hiyo course ya guidance and councelling wakulaumiwa ni nani? Je wewe unaonaje
 
Kuna masomo waombaji ni wachache, ndio hao waliofanya oral pekee
 
Hawana akili,mtu umekaa miaka zaidi ya mitano mtaani halafu bado unakimbilia hizo ajira! Miaka mitano na kuendelea bado haijakupa street rules za kuingiza hela?? Uliishi vipi na ushindwe sasa??
Siyo kila mtu anaweza
 
Kuna masomo waombaji ni wachache, ndio hao waliofanya oral pekee
But swali lake anauliza kuwa je wangechujwa kwa pepa wana uhakika gani kama miongoni mwao asinge score zero kama za masomo mengine kama tulivyoona

Means mtu wa kiswahil kapigwa written kascore 0 hatimae hakwenda oral huyo wa mathe nae wana uhakika gani asingepata 0?
 
MLISEMA WALIMU NI KAZI MBAYA... Sasa hivi mnaililia... Waacheni walimu wainjoi
 
Yn nyie waalimu bhana πŸ˜‚ yn mtu akisapoti nyie kufanyiwa usaili mnaanza kumuona n adui wenu πŸ˜‚ mzee Mm sio niliyeleta usaili kwa waalimu kwahy kama unanichukia bc hayo n matumizi mabaya ya chuki πŸ˜‚
Wee jamaa unajiona wamaana sana na bora kuliko mwingine kila la kheri mkuu na hongera kwa kutokuwa mwalimu maana sisi walimu ni mazwazwa sana ila maengineer na ma IT ni vichwa sana kama wewe
 
Kabisa na siku zote tunaona wanaitwa watu hata 20 Kwa ajili ya interview na wanakula below 50% na nafasi zinatangazwa upya. Huu ubaguzi wa Nini Kwa kada Moja?
 
Lengo la hizi interview ni kuchuja watu kwa sababu waombaji ni wengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…