Anaendelea......
"Yanga inayotembeza bakuli uwanjani kupata Bukubuku bado ilikuwa inapambana na kushika nafasi 2 za juu Ni spirit yao na maisha yao, Uliona walivyolihandle suala la Fei!? Ni kipenzi chao na alikuwa ndiye tegemeo la timu ila kilichofuata!? Wakaungana fasta kumgeuka!
Wana umoja kwenye nyakati nyingi mno! Kwao kumpoteza mchezaji wao kipenzi ni maisha... Watampiga nongwa weee kisha wataendelea na maisha yao! Si ajabu keshokutwa Fei akarudi pale na wakaishi naye kama hakuna lililowahi kutokea.
Jana wameita siku ya Supu sivyo!? Wamesajili wanachama na mashabiki wengine kuhuisha sajili zao! Wangeweza kuuza hao ng'ombe wa Supu ila wameamua kula na mashabiki wao.
Ni timu inayoishi kijima sana katikati ya nyakati za kibepari! Suala mnaloona ni dogo wao hulifanya kuwa kubwa na la tofauti.
Wakati fulani ni ngumu kuwaelewa ila amini umoja hujengwa na vitu viwili tu duniani! STAREHE na MATESO! Suala la bond hiyo kudumu ni kila mmoja anavyoupalilia upendo huo. Timu yao ina vinasaba vya uswahili/uafrika... Sigara 1 wanaweza kuvuta watu 6 alaf fresh tu!"