Mchanganuo tozo za LUKU kuanzia August 20-2021

Hapo hata me nimeshangaa how comes tunakopa na bado tunawekeana tozo
Kama una kadi ya chama, peleka pale TRA wanakuondolea tozo. Tumekopa 2.7t kwaajili ya barabara na elimu, hivyo kuna msamaha wa tozo kwa wenye kadi ambapo kimsingi mkopo utafidia.[emoji4]
 
Amang'ana ghenu!

Naomba niende kwenye maada moja kwa moja,

Wakuu naomba kuelimishwa/kufafanuliwa kuhusu hili Tangazo la TRA na TANESCO kupitia maswali ninayotaka kuuliza hapa kwa sababu kuna vitu Tangazo halijaweka wazi pengine ndo ikapelekea mimi kutokuliewa vilivyo na kuibua mswali kichwani mwangu,

Maswali yangu ni kama ifutavyo

1) Swala la wapangaji kuhusu hii kodi ya majengo likoje? Na wao ni wahusika wa kulipa hii elf1 kila mwezi kama sivyo TANESCO na TRA wanaliweka vipi?

2) Nyumba moja inazo Luku zaidi ya mbili, hili nalo likoje? Jengo moja litakuwa linalipiwa kodi zaidi ya elf2?

3) Je kuna maelekezo yoyote tukilipa hiyo wenye nyumba wawarudishie hicho kiasi walicholipa? Kama yapo kuna utaratibu gani umeweka kwa hizo hela kurudi kwa wapangaji!

Nb, Nimepita kwenye moja ya page zao kwenye mitandao hakuna majibu ya maswali yangu.

Hata kama sio wao watajibu naomba mwanaJF alieliewa Tangazo majibu yako tafadhali.
 
TRA wafunguka anayetakiwa kulipa kodi ya majengo kupitia Luku, kati ya mpangaji na mwenye nyumba
Udaku Special / 1 hour ago

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kuwa kodi ya majengo kwa njia ya ununuzi wa umeme ambayo itaanza kutumika Agosti 20, 2021 inatakiwa kulipwa na wamiliki wa majengo na sio wapangaji kwenye majengo hayo.

Hayo yameeleza na Lazaro Lucas katika mahojiano na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) ambapo ameongeza kuwa kwa sasa kuna changamoto wa kutofautisha mnunuzi wa umeme kama ni mwenye nyumba au mpangaji, hivyo kwa mwanzoni mpangaji anaweza kukatwa kodi hiyo kimakosa.

“Hiyo kodi inapaswa kulipwa na mwenye jengo lakini kwa mwanzo kumekuwepo na changamoto ya kujua ni yupi mwenye jengo ni yupi mpangaji kwa hiyo mwanzoni [mpangaji] unaweza ukapata ‘bill’… mwenye jengo afike ofisini aseme nyumba zangu ni moja, mbili, tatu, ili wenye zile mita ziondolewe,” amesema Lucas.

Lucas ameongeza kuwa mwenye jengo anaweza kulipia kodi ya nyumba za wapangaji taslimu shilingi 12,000 kwa kila nyumba ya kawaida kwa mwaka na namba za mita za wapangaji zitaondolewa kwenye mfumo, au kodi hiyo itahamishiwa kwenye mita yake.

Aidha, TRA imesema kuwa endapo mwenye jengo hatowasilisha taarifa za wapangaji TRA, wapangaji wanaweza kupeleka malalamiko yao kwamba wanatozwa kodi ya jengo kimakosa.

Viwango hivyo kwa sasa ni shilingi 12,000 kwa kila jengo la kawaida ndani ya kiwanja kutoka shilingi 10,000 iliyokuwa ikitozwa awali, na shilingi 6,000 kwa kila sakafu ya ghorofa kutoka 5,000. Hata hivyo kwa upande wa halmashauri za wilaya na miji midogo nyumba za ghorofa bila kujali idadi ya sakafu zitatozwa shilingi 6,000.

Kwa utaratibu huo kila mnunuzi wa umeme atakatwa shilingi 1,000 kwa mwezi kwa nyumba ya kawaida na shilingi 5,000 kwa mwezi kwa kila sakafu ya ghorofa. Kwa wanaotumia mita za ankara watalipa kodi hiyo kwa pamoja katika Ankara zao za mwezi.

Source : Swahili Times
 
IMG-20210819-WA0146.jpg
 
Baada ya miaka 10 hakika Tanzania itang'ara kiuchumi.
kwa sasa tufunge mkanda ili tuijenge nchi yetu.
Mjenga nchi ni mwananchi, shimee wananchi wenzangu.
 
Back
Top Bottom