Mchanganuo tozo za LUKU kuanzia August 20-2021

Mchanganuo tozo za LUKU kuanzia August 20-2021

Bado kodi ya bahari kwa wakazi waliopo pwani ya bahari ya Hindi..harafu wakishindwa kufikiri majibu yao ni peleka mbadala au nenda burundi sio kwamba wao watoke wawaachie wanaofikiri vizuri nchi hii inaongoza kwa kodi kero kwa Wananchi kila kukicha...
 
Ukinunua Umeme utalipia Kodi nne:
1. VAT - 18%
2. Ewura - 3%
3. REA - 1%
4. Kodi ya Jengo (Tsh 1000- Tsh 5000)

Awamu ya sita, tozo ziendelee!
Hamna namna, taifa la wabishi kulipa kodi ni lazima utumie njia hizi..
Nampongeza mama ktk hili, ishu ni inayokusanywa iene ktk kusudia la maendeleo ya wananchi na sio kufaidisha wachache...
 
Hapa inabidi waongeze Kodi kwa ajiri ya kutunisha mfuko/bodi ya mikopo Ili vijana wetu wawe na uhakika wa kupata mikopo ya Elimu ya juu
Yaani watu wachamgishwe ili fulani akasome?? Haiwezekani mama sio mjinga! Tafuteni sponsorship
 
Wakati wa Magufuli watanzania tulilalamika hakuna mzunguko wa fedha mtaani kwa sababu matajiri wamebanwa sana kulipa kodi na wengine kufunguliwa kesi za uhujumu wa uchumi kwa kukwepa kodi. Aliita serikali inayojari wanyonge.

Machinga, Mama ntilie, wakulima, wajasiriamali na wapangaji hawakuguswa. Lakini bado tukalalamika hakuna hela mtaani.

Zama hizi za SSH anawaomba Watanzania wote tuchangie nchi kupitia tozo za Mwigulu ili mzigo wasitishwe matajiri pekee bado tunalalamika.

Kweli uongozi ni kazi ngumu. I'm out !
 
Kuna wapumbavu wanaamini kutokulipa kodi au kulipa kodi ndogo zaidi ndio maendeleo kwa wananchi...hamna nchibiliyoendelea ambayo wananchi wake wanalipa kodi ndogo...hamna, na hayo maendeleo yanachangiwa ktk hizi tozo...
 
Asilimia inategemea na kiasi utakacholipia kwenye manunuzi ya luku ukinunua wa pesa ndogo percentage itakua kubwa kama makato ni ya mara moja mfano;
Umeme wa 5,000/= ukikatwa 1,000/= ni sawa na 20%
Mtani najikuta sielewi tu hii kitu kwa kweli.

Hivyo hiyo hela inakatwa kwa mara moja nikimaanisha unaponunua tu mnamalizana papo hapo au ndo wanakata kidogo kidogo?
 
Back
Top Bottom