ha haaaa, kuna siku na mimi zali huwa zinanitembelea......
siku moja nikakutwa na zali la kutembelea USA. Nikiwa huko siku moja nimechukua taxi kwenda sehemu, dereva alikuwa mweusi...
tumeenda kidogo simu yangu ikaita, nikaanza kuongea kiswahili.... yule dereva akaniangalia, nilipomaliza akaniuliza natokea wapi, nikasita, akaniambia najua unatoka East Africa maana umeongea Kiswahili. akaniambia yeye anatokea Sudan na ana PhD. nikamshangaa kwa nini yupo pale na anaendesha taxi. Akaniambia yaani Sudan ikiwa stable nitachukua next flight kurudi home...... nilimwelewa kuwa anakaa kule sababu tu home hakuko stable.....
tuliongea mambo mengi mno ambayo siwezi kuyaweka hapa sababu najua kuna wengine yanaweza yakawagusa......
hapa ninachotaka kusema, pengine sisi tunaweza kuwaona wenzetu kuwa wanajisikia, kumbe wenzetu wanatuonea wivu sana sisi ambao tunaishi na tunaweza kuishi nyumbani.....
(huu ni mtazamo wangu mimi jamani)
cc.
figganigga