Mchango wa diaspora wa kike katika jamii ya kitanzania...

Kama mmefikia kupangia budget hela ya wabeba box walioko nje ya nchi basi Tz iko pabaya sana. Sioni uwiano wa watu walioenda nje kwa juhudi zao leo wabebeshwe mzigo wa kusaidia taifa zima.
 
Kama mmefikia kupangia budget hela ya wabeba box walioko nje ya nchi basi Tz iko pabaya sana. Sioni uwiano wa watu walioenda nje kwa juhudi zao leo wabebeshwe mzigo wa kusaidia taifa zima.

Mkuu Bufa..wewe kama mtanzania unavyoishi hapa kuna mengi unayoyafanya kwa ajili ya tanzania, na ma diaspora pia wananafasi katika kuendeleza nchi..

unawakumbuka watu kama kina dr.livingstone. akina john craft, akina bwana rebman na wengineo je, walikuja africa for there own benefit? na siyo kwa ajili ya nchi zao?
 
Last edited by a moderator:
Kuna mdau mmoja hapa MMU machachari kweli kweli, katika hoja na misimamo yake...nadhani anaishi hapa hapa tz, let me ask her, lara 1..do u think dar es salaam is where u deserve to be? is dar city enough for u? do u think life in dar is almost the same as life conducted in other cities like new york and london..kuna du wakibongo anaweza kuwa mjanja ndani london au newyork kama alivyo dar? hata kama kaishi huko miaka kibao?
 
Last edited by a moderator:
Mie kwa kweli sifagilii kabisa kitendo cha binadamu yeyote kujiona yupo above the rest. Acha wanawake. Ila culprits wa tabia hii mbaya ni wanawake. Na hutokana na inferior egos na kukosa kumuamini Mungu. Haiwezekani from nowhere ujione you are a notch above the rest. Yaani sipendi hii tabia kabisa. Kama unamjua Mungu utajua kiukweli we are all equal before the Good Lord.
 

Sipendi hii kitu inayoitwa diaspora, wengi wakija huku huwa wanajidai wamesharabu tamaduni za kizungu kabisa na wengine hata Kiswahili hujifanya kinawapa shida.
 
Last edited by a moderator:
Naomba nami nitoe mchango wangu kwenye mada hii japo umepoint baadhi tu ya watu wawe washirika wakuu, mimi naomba niwe mshirika wa kawaida. Mtoa mada umezungumzia mchango wa wadada wanaoishi u.k na u.s.a na kujiona kwao masuperior. Mimi naona usuperior ni tabia ya wanawake/ wadada hasa anapokua amefanya jambo ambalo mwenzake hawezi kufanya au bado hajafanya. Chukulia mfano wa wadada wanaotokea mikoani wakaja DSM huwakoga sana wenzao ambao bado hawajafika dar tena wengine warudipo vijijini kwao hujifanya hata kilugha wamesahau na kuongea kiswahili tu tena kile cha mtaani na si fasaha.

Kwa mtazamo wangu wadada wanaoishi nje ya nchi wana mchango mkubwa sana nchini kwetu. Wengi wao wanasaidia sana ndugu zao na kwa bahati mbaya baadhi ya ndugu wanamissuse hiyo misaada. Kumbuka mwanamke huwa hasau kwao hata kama anashida kiasi gani lazima atasaidia wakwao.

Mimi hii naichukulia in a positive way ni kweli kuna baadhi ya wadada wanafanya kazi mbili mbili kama ambavyo huwa tunasikia lkn hii yote ni kwa sababu nyumbani kwao wanamtegemea karibu ukoo mzima na wengi tunaamini mtu akienda ulaya basi huyo atakua anapesa ie tunaamini wazungu wote anaosalimiana nao basi humkesh hii ni myth iliyozoeleka huku kwetu. Kuna wachangiaji wanasema pengine wengine kazi yao ni kuzoa kinyesi cha wazungu , mimi nadhani kazi ni shughuli yoyote halali inayomuwezesha mtu kuwa na kipato. Hii ni dharau tu, ambayo sijui tunaitoa wapi. Si wote wnazoa kinyesi wapo wengi wanafanya kazi nzuri tu.

Sasa ile hali ya kujikweza na nini ni tabia ya mtu . Mtu huyo hata angeishi China bado angejikweza tumewaona wagnapi wameenda china na wanajiona superior. Ile hali ya wadada wengi kusema watu wengine wanaenda ulaya kulala na mbwa hii ni kashfa hakuna kitu kama hicho jamani. Binafsi napenda kuwa positive in everything, wala kuishi ulaya sio mafanikio/kushindwa la hasha mafanikio popote japo ulaya kuna opportunities nyingi .

Nisiwachoshe naconlude kwamba madiaspora wanachangia pato la taifa kwani ukielimisha m/ke mmoja umeelimisha taifa. Niombe radhi kama utajisikia nimekukwaza mpendwa. Natoa rai jamani tutoke twende na nchi za wenzetu tuone wanishije ili tuepuke kuamini myth.
 
Rafiki hii ni tabia ya wanawake wengi hasa anapokua nacho labda ndivyo tulivyoumbwa . Nakubali unyenyekevu ndio jibu la mambo yote lkn hatuwezi kuepuka hili. Tuwapende tu na tuchukuliane nao. Tena hata kwenye makusanyiko ya kiroho bado type hizi za wadada utakutana nazo.
 

aaah wapi..!! vibaka wapo sana, msitembelee miji mikubwa tu kuna miji mingine ukienda.... Jamani.. Jamani utasema bora hata ya mkaa mbagala mara elfu.

Msishangae kwanini walioko nchi za ulaya na kwingineko wanashindwa kuwasaidia ndugu zao?

Jamani wengine wanapokuwa huko wanapata hela ya kula tu ilimradi siku isogee wakirudi makwao mbwembwe nyingii..
 
Last edited by a moderator:

maendeleo ni juhudi binafsi za mtu
kukaa nje haimaanishi kwamba ndio mtu ana
maendeleo,unaweza kaa nje na bado ukawa
choka mbaya tu kuliko hata waliopo tz,so juhudi na malengo
ndio siri ya mafanikio,na si kuishi nje!!! figganigga umenisoma!!mia

well said my dia, kwanza wanaonufaika huko ni wachache na hawana mbwembwe,
kuna wengine mmmh... ukiwaona hadi wanatia huruma waweza sema walifukuzwa nchini kwao.. But wakirudi home huwa wana pretend kama walikuwa na good life, kumbe hamna lolote!
 
Last edited by a moderator:
well said my dia, kwanza wanaonufaika huko ni wachache na hawana mbwembwe,
kuna wengine mmmh... ukiwaona hadi wanatia huruma waweza sema walifukuzwa nchini kwao.. But wakirudi home huwa wana pretend kama walikuwa na good life, kumbe hamna lolote!

ndiyo usuperiority huo..
 
Walioko ulaya kufanya mwembwe wakija nyumbani haina tafauti na mbwembwe za wachaga wakienda Mamndenyi wakati wa sikukuu. Hata walioko daslaamu nao wanashindwa kusaidia ndugu zao. Weeh huwezi kuzaa watoto tisa ukitegemea tukulipie ada zao afu tushindwe kupanga nyumba zenye ac lol. Mtu amejinyima mwaka mzima, akanunua na viwalo vya holiday. Na hata akicheck in sea cliff for breakfast, yuko holiday na sio mikogo.

Wakati mwingine watu wanajinyanyapaa. Mtu amechoka anataka kukaa mahali apumzike ukimchangamkia anakupa cold shoulder ili tu usivute kiti. Manake waswahili na sie, unakuta mtu anaibia kukaa na ex wake wapeane updates wewe unajikaribisha.
Msishangae kwanini walioko nchi za ulaya na kwingineko wanashindwa kuwasaidia ndugu zao?

Jamani wengine wanapokuwa huko wanapata hela ya kula tu ilimradi siku isogee wakirudi makwao mbwembwe nyingii..
 
Last edited by a moderator:
King'asti kwani kule Mamndenyi kuna kitu chochote basi
au ni mbwembwe zao tu.

 
Last edited by a moderator:
Kama mmefikia kupangia budget hela ya wabeba box walioko nje ya nchi basi Tz iko pabaya sana. Sioni uwiano wa watu walioenda nje kwa juhudi zao leo wabebeshwe mzigo wa kusaidia taifa zima.

Bora watakusikia manake boksi linazidi kuwa zito ukizingatia summer ndio kwanza imeanza na joto limezidi. Mutuonee huruma jamani mgongo unazidi kuniuma kwaajili ya kupiga boksi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…