Tofauti na nchi nyingi Kusini Kwa jangwa la Sahara zinazotegemea ufadhili na Tozo. Nchi ya Saudi Arabia Ina vyanzo vingi vya mapato ikiwemo HIJJA kila mwaka. Nani anaweza kutuwekea data za mchango wa HIJJA kila mwaka kwenye lato la Taifa hili kubwa duniani?
Hijja ni manufaa kwa dunia nzima,wanaonufaika ni dini zote zilizopo na wasio na dini,na makabila yote duniani.Na inaongeza ajira kwa watu wa dini zote na wasio na dini.Anayekwenda Hija anaongeza uchumi wa nchi anayotoka,kwa mfano yupo Kigoma,atapanda bajaji,kwenda stand ya mabasi,kule standi atakata tickets ya bus,atakula njiani,atafika Dar,atalala guest house,atakula kwa mama lishe,atakodisha Tax,kwenda sehemu mbali mbali,atakata ticket ya ndege,na matumizi mengine,mote humo watu wa dini tofauti na makabila tofauti,wanapata kipato na nchi inapata kodi.Fikiria wakiwa mahujaji mia tatu,ni kipato kikubwa,ndani ya nchi moja,bado hatujaweka idadi ya dunia nzima.
Bado kuna ibada ya UMRA,hii haina msimu,ni wakati wowote wa mwaka.
Aliyeleta ibada ya Hija,anatakiwa apewe pongezi.
Anayekwenda Hijja,atatumia huduma zote,bila kuuliza dini,kabila ya mwenye huduma,kuanzia usafiri,chakula,malazi,mavazi,zawadi atakazo nunua kuwaletea ndugu na jamaa.Hiyo ni kwenda na kurudi,alikotoka.
Wafugaji wa mbuzi,ng'ombe,Kuku nk,wakulima wa nchi mbali mbali,wanapeleka bidhaa zao Saudia,bila kuulizwa dini au kabila ya muuzaji.
Bado hatujagusia bidhaa za viwandani,kutoka sehemu mbalimbali,duniani.
Hijja ni uchumi wa dunia.Mleta uzi changamkia kupeleka bidhaa,fuga mbuzi,ng'ombe,kuku,lima mahindi,Michele,ngano, kahawa,chai nk,tafuta soko Saudia.