Mchango wa Hijja kwenye Uchumi wa Saudia

Sasa kama ni utalii tatizo lipo wapi? Mbona wazungu hawaambiani wasije afrika kutalii kutakuza uchumi wa afrika?
Hawatokuwa radhi mayahudi na manaswara mpaka muige Mila zao (Albaqara)


Hao ni wapumbavu tu, wakinywa malaria siku 3 tu wanamkumbuka Mungu, ila Sasa nguvu ya kutype kwenye keyboard ndio inawapa jeuri
 
Serengeti na Rubondo kwa ajili ya wazungu,sisi wacha twende macca na israel tukakuze uchumi
 
Hi argument no ya kifala Sana.
Ibada na Utalii ni vitu viwili tofauti Sana.
Unawezaji kulinganisha mtu aliyekesha nightclub na aliyekesha kanisani au msikitini!?
 
Kaa hapo hapo usitoke.
 
Ufalme wa saudi arabia hauna njaa mpaka wategemee hijja mkuu, hizo gharama zote huwa zinaishia kwenye matumizi na ufalme unachangia na kutoa huduma nyingine bure.

Kabla ya corona hajj ilikuwa inachangia kama USD bilioni 40 kwa mwaka ilipokuja corona mahujaji walipungua kwa zaidi ya asilimia 50, wakati wao kwa mafuta tu wanaingiza zaidi ya USD bilioni 400 kila mwaka sasa hiyo $40 bilioni si pesa ya kubrashia viatu?.

Tukirudi kwenye mada hii hajj ni ibada imewekwa tangu enzi za nabii ibrahim amani iwe juu yake na watu wakienda kwa wanyama na wengine kwa miguu kwa tabu kubwa, sasa kama makusudio yalikuwa ni uchumi ile enzi ya kwenda na punda kwa makusudio mafuta yakiisha hijjah ndio isaidie basi kwa taarifa ni kwamba saudi kingdom wana mafuta ya kuzalisha miaka 400 toka sasa.

Si vyema kupotosha watu kwa makusudio ya kuuchafua uislamu, na kuwafanya wao ni mazuzu wanatumika kiuchumi kwa kisingizio cha ibada.

"Na watangazie watu {ibada ya} hija, watakujia kwa miguu na juu ya kila ngamia aliyekonda, watakuja kutoka katika kila njia ya mbali.."

Quran 22:27

Karibu kwa mjadala.
 
Nawe ni Mwafrika
Ahsante sana kwa kututukana wote wakiwemo na wazazi wako.
Ndio najua kuwa nawe ni mtu wa hovyo huwezi kuja na wazo la kuanzisha Hija yako ili watu wa ulimwengu waje kwako
Siku ukipata akili na kuacha kuwa wa hovyo utatukomboa kwa kuleta Hija Tanzania.
 
Unaweza kunisaidia ni mwaka gani serikali ya Saudia iliweka Sheria ya hija? Ilikuwa chini ya Mfalme gani?
 
Unaweza kuziorodhesha nguzo zote tano kwa mpangilio wake?
 
Hakuna trillions of USD kutokana na hajj kama kuna data leta hapa, bali saudi arabia inafadhili waislamu duniani kote wanasoma bure kwenye vyuo vikuu na wanalipwa mishahara, umewahi kuona wapi?.

Ukiachana na hayo kuna ofa ya mahujaji wengi kuja bure saudi arabia kwa kujibu tu baadhi ya maswali, bali kuna misaada mingi inakuja kwenye kaya za waislamu kutoka ufalme wa saudi arabia.

Nasaha zangu ukizungumzia saudi economy usidhani unaongelea zimbabwe mkuu, wao hawaishi kwa kutegemea vimilioni 10 vyenu vya kupandia ndege na kuishi hotelini msimu wa hijja.
 
Hijja ni manufaa kwa dunia nzima,wanaonufaika ni dini zote zilizopo na wasio na dini,na makabila yote duniani.Na inaongeza ajira kwa watu wa dini zote na wasio na dini.Anayekwenda Hija anaongeza uchumi wa nchi anayotoka,kwa mfano yupo Kigoma,atapanda bajaji,kwenda stand ya mabasi,kule standi atakata tickets ya bus,atakula njiani,atafika Dar,atalala guest house,atakula kwa mama lishe,atakodisha Tax,kwenda sehemu mbali mbali,atakata ticket ya ndege,na matumizi mengine,mote humo watu wa dini tofauti na makabila tofauti,wanapata kipato na nchi inapata kodi.Fikiria wakiwa mahujaji mia tatu,ni kipato kikubwa,ndani ya nchi moja,bado hatujaweka idadi ya dunia nzima.
Bado kuna ibada ya UMRA,hii haina msimu,ni wakati wowote wa mwaka.
Aliyeleta ibada ya Hija,anatakiwa apewe pongezi.
Anayekwenda Hijja,atatumia huduma zote,bila kuuliza dini,kabila ya mwenye huduma,kuanzia usafiri,chakula,malazi,mavazi,zawadi atakazo nunua kuwaletea ndugu na jamaa.Hiyo ni kwenda na kurudi,alikotoka.
Wafugaji wa mbuzi,ng'ombe,Kuku nk,wakulima wa nchi mbali mbali,wanapeleka bidhaa zao Saudia,bila kuulizwa dini au kabila ya muuzaji.
Bado hatujagusia bidhaa za viwandani,kutoka sehemu mbalimbali,duniani.
Hijja ni uchumi wa dunia.Mleta uzi changamkia kupeleka bidhaa,fuga mbuzi,ng'ombe,kuku,lima mahindi,Michele,ngano, kahawa,chai nk,tafuta soko Saudia.
 
Kama siyo lazima kwanini iwekwe kati ya nguzo 5 za Uislam!?
 
Kama siyo lazima kwanini iwekwe kati ya nguzo 5 za Uislam!?
Wewe kafiri Huna akili ..Hijja ni moja kati ya nguzo za uislamu ila ...kama kumudu gharama za hijja inakuwa lazima kwake ila kama hana uwezo kwake inakuwa sio lazima
 
Wewe Pimbi hizi dini zilizoletwa na majahazi zimefubaza akili yako.Hijja ni utalii kama utalii usiwe mjinga na mpuuzi.Wacha kukuza uchumi wa waarabu.
Zuia na wazungu wasije hijja huku Serengeti maana watakuza uchumi wa tz
 
Usihakikishe kitu usichokifahamu. Hijja haikuanza na Mtume Muhammada SAW, yeye aliikuta ila alikujabadilisha baadhi ya mambo wakati wake kama vile kuondoa masanamu kwenye Kaaba.

Je waliokuwa wanahiji hayo masanamu ya Kaaba walikuwa waislamu ama imani zingine ?

Kwani uislamu na quran alipewa nani kama sio mtume Muhammad, useme kabla ya Muhammad waislamu walikuwepo wanaenda hadi Kuhiji kwenye Kaaba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…