Mchango wa sherehe ya kumaliza Masters itakayofanyika ukumbini. Nini maoni yako kuhusu uchangishaji wa sherehe za namna hii?

Acha ujinga wewe ulishawahi kuwaona hao uliowataja wakichangiwa kwenye sherehe zao
 
Naamini huelewi maana ya 'common sense'. Vilevile, hujaelewa maana na kazi ya neno 'HATA' katika sentensi yangu.
 
Mara nyingi mjinga huwaona wengine kuwa wajinga. Kuwa makini kuonyesha ujinga wako kwenye maandishi.

Kumsherehesha mwenye sherehe ni kupitia zawadi tu kwa kuwa yeye mhusika anaandaa sherehe na kuwaalika rafiki wafurahi pamoja naye hatua aliyofika. Pongezi haiombwi kwa lazima. Unapofikia mafanikio fulani usiwape mzigo wengine wa kukupa furaha. Andaa unachoweza wajulishe wana. Wakiamua kuchangia ni maamuzi binafsi sio unachapisha makadi.

Kumsherehesha mhitimu kwa hatua aliyofikia kunapangwa na ndugu na marafiki kwa ghalama zao kuhakikisha siku yake ya kufurahia mafanikio inakuwa nzuri. Hapa jambo linaweza fanyika hata kama mhusika hakujiandaa.
 
Achange tu ili kuondoa gubu na chuki. Ila ni mambo ya ajabu kuchangisha pesa za graduation
 
Mm kuna mdada mtoto wake amemaliza std 7 anamfanyia sherehe mwezi ujao anataka nimchangie...yan nimecheka kimoyomoyo nimeshindwa hata kumjibu
Bora huyo kuliko mtu mzima na ndevu
 
Sasa hizo so called foundation wtu huwa wanatakatishia fedha kwa tafrifa yako!
Harusi sio foundation ni tafrija ya kawaida ambayo imetengenezewa utamaduni wa hovyo wa kuchangiana

Kuna vitu vya kuchangia ambavyo ni makundi maalum yasiyojiweza! Sio mtu kashiba anajiskia kuwashibisha halafu mumchangie Hell No!!!
 
Watu tunaopenda celebresheni mbona tunachanga chapuu kwa haraka...😃😃
 
Toa Hela kama hauna Nia ya kutoa futa Uzi , period
 
Yaani mm ni joho, then home full stop!
 
Huna hela tafuta hela lofa wewe yaani kuchangia elfu 50 unaona utafilisika

Elfu 50 nayo ya kupiga yowe lofa wewe
Tatizo siyo kiasi cha kuchangia, ishu unachangia kitu gani, kuna mambo ya kijinga siyo ya kuchangia. Pia unaposema nitafute pesa unajuaje kama sina hizo pesa? Au nimewahi kukuomba pesa?
 
Yeye ndiye kahitimu na anafurahi kwa kuhitimu, Kama ameamua kufanya sherehe hakupaswa kuomba michango! Aandae mwenyewe aalike watu wafurahi pamoja! Kama hawezi anaweza kufurahia akiwa nyumbani kwa gharama nafuu kabisa!
 
Nadhani umekosea kusoma kadi ya kuomba mchango, huenda jamaa anahitimu cheti.
Mtu anayepata masters hawezi kuwa mjinga wa kiwango cha kuandaa sherehe.
Wabongo hata maprofesa wana mambo ya kipuuzi sana, seuze Masters?
Utashangazwa sana, mkuu.
 
Huyo anatafuta mchango ajiajiri ajira hazipo tena.
 
Hio michango ya kijinga waliniunga kwenye group lao la WhatsApp la kuchangia harusi nikaleft. Haiwezekani jitu linaoa na kuacha kila siku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…