Mchawi kazi yake ni kuroga urudi nyuma, jilinde

Mchawi kazi yake ni kuroga urudi nyuma, jilinde

Kumpunguzia mwanadamu uwezo wa kufikiri yaani awe tegemezi asitumie akili yake kutatua shida.
Hakuna shida yeyeto duniani ambayo huwezi itatua kwa akili yako.Sema akili za wengi zimeisha chaji thus utegemea waganga na manabii kufikiri badala yao.
Mungu alimuumba mwanadamu akiwa kakamilika na wala haitaji msaada toka kwenye nguvu nyingine.
Kama unaamini uwepo wa viumbe majini/mapepo ina maana unajua kwamba wanaweza kuleta athari kwa binaadamu mfano kumsababishia maradhi, je kwa kutumia akili tu ya tuliyopewa na Mungu ni vp utaweza kuondoa hiyo changamoto kwa maana hilo tatizo la kiafya lililosababishwa na jini/pepo? Kumbuka huo sio uchawi ni athari za hao viumbe.
 
Ilikuaje mkuu?

Nakumbuka ilikua ni mwaka jana mwezi wa pili wakati niko on board nikiingia shift yangu Engine Room hafla tu niko kwenye routine zangu za kila siku nikiingia watch nikakutana na hali iliokua tofauti na mazingira yale,ilikuja harufu kali mule ndani na haikuchukua sekunde mbili moto ulitokea bila kujua chanzo ni nin na tulikua watu wawili. Tulijitahidi sana kupambana nao ukatushinda ilibidi tutoe report kwa watu wa bandari na kilichofuata ni kujitosa majini hili tukio lilinifanya machozi yanitoke na kutolisahau maana hio siku bahar nayo ilikua imechafuka na upepo mkali almanusura tuingie kwenye mvungu wa meli ilioko karibu yetu.
 
Maandiko yote Biblia takatifu na Quran tukufu ndio jibu kwa KILA muamini na ni hakika imeeleza namna ya kukabiliana na hivyo viumbe. Pili ukizijua Siri za hivyo viumbe yaani codes zake mfano nini ukukinga usidhurike hawawezi kukudhuru. Shida kuu ni ukosefu wa maarifa jinsi ya kujinusuru.
 
Sio kweli, hakuna mtu mzuri kam mchawi
Mzuri ufafanuzi,
Ila nijuajo Hakuna mtu mwema na mwenye roho nzuri tabia njema kwenye Jamii na anaesali kama mchawi na jambazi. Hawa watu ni wema Sana mchana ila usiombe usiku uingie anga zao, hawana mchezo wala huruma.
 
Mchawi ni mtumwa na mateka wa shetani uyatenda Yale kwa kufuata maagizo. Asipoyatenda upewa adhabu so lazima atende atake asitake. Ni hadi tu pale atakapopata Neema ya wokovu na kuamua kusaliti kambi ambapo bila imani thabiti adhabu yake ni kifo.
 
Nakumbuka ilikua ni mwaka jana mwezi wa pili wakati niko on board nikiingia shift yangu Engine Room hafla tu niko kwenye routine zangu za kila siku nikiingia watch nikakutana na hali iliokua tofauti na mazingira yale,ilikuja harufu kali mule ndani na haikuchukua sekunde mbili moto ulitokea bila kujua chanzo ni nin na tulikua watu wawili. Tulijitahidi sana kupambana nao ukatushinda ilibidi tutoe report kwa watu wa bandari na kilichofuata ni kujitosa majini hili tukio lilinifanya machozi yanitoke na kutolisahau maana hio siku bahar nayo ilikua imechafuka na upepo mkali almanusura tuingie kwenye mvungu wa meli ilioko karibu yetu.
Pole sana ndio mambo ya ulimwengu hayo.
 
Maandiko yote Biblia takatifu na Quran tukufu ndio jibu kwa KILA muamini na ni hakika imeeleza namna ya kukabiliana na hivyo viumbe. Pili ukizijua Siri za hivyo viumbe yaani codes zake mfano nini ukukinga usidhurike hawawezi kukudhuru. Shida kuu ni ukosefu wa maarifa jinsi ya kujinusuru.
Mimi nikadhani kwamba Mungu alishatupa akili tunaweza kutatua matatizo yetu yote kwa kutumia uwezo wa akili tulizopewa na Mungu ndio maana wewe unasema uchawi unatufanya tuwe wajinga tusitumie akili zetu.
 
Nina jamaa zangu hawakauki kwa waganga lakini nimewazidi maendeleo mara elfu,wamechoka wamechakaa .
Kuna wengine wao hawakauki makanisani kila kukicha kazi ni kubadili makanisa lakini maisha yao hayaeleweki.
Sikatai uchawi upo na Mungu yupo ila usipofanya kazi kwa bidii kila siku utasema unarogwa ....,unaamka saa 4 asubuhi,unachagua kazi,kazi hutaki kufanya hata uende kuchukua uchawi kwa shetani kuzimu hautoboi ng'ooo.
Kwahiyo mafanikio yapo kwenye kufanya kazi kwa bidii?
 
Ushirikina ni chanzo kikuu cha kuzalisha negative energy kwenye Jamii na Jamii ikishakuwa negative Hakuna maendeleo. Lengo kuu la uchawi ni kuwafanya watu wawe masikini na kutokana na umasikini tabia zote chafu uzaliwa. Ukahaba, wizi, roho mbaya, matusi, ukorofi, vurugu nk.
Ndo maana wenzetu waliua wachawi wote Ili kupata Jamii bora
Kwahiyo afrika ni masikini kwa sababu ya uchawi?
 
Ili kuupunguza uwezo wa kufikiri wa mwanadamu Ili awe masikini Ili amuabudu shetani, umasikini ndio chanzo cha tabia zote chafu ngono,ulevi, vurugu,matusi,wizi nk,fanya study washirikina wengi thinking capacity zao zipo chini sana sawa na kuku hata maeneo yenye imani hizo yapo duni Sana kimaendeleo kuliko Jamii zisizoamini. Uchawi ni negative power.
Unaufahamu vp msemo wa pesa ni ibilisi?
 
Naungana na wajumbe waliotangulia..😊
 
Unaufahamu vp msemo wa pesa ni ibilisi?
Pesa ni nguvu na unaweza ukaitumia vizuri au vibaya kwenye kuitafuta hio nguvu au kwenye matumizi baada ya kuipata hiyo nguvu.ibilisi ni kiwakilishi cha matendo maovu kuelekea kuitafuta pesa au kuitumia vibaya pesa
 
Sasa kwanini unasema umasikini ni chanzo cha tabia mbaya kama ulevi ngono n.k wakati inajulikana pesa ndio kishawishi kikubwa cha kufanya hayo mambo?
 
Kwenye ushirikinq naomba kujua Siri ya kuku kishingo aisye na mavyoya shingoni
Following
Nilikuwa nafuga kuku huko kusini sasa nikaweka mbegu za kuku kishingo; walifanya vizuri sana lakini jamaa moja akaniambia usifuge hawa kuku hawana soko huku watu hawanunui. Kumuuliza kwanini hakuwa na jibu
 
90%, uchawi imechangia, ukielewa kwann ulaya waliwaua wachawi ndipo wakapata maendeleo.Unaweza ona athari za uchawi kwenye ustawi wa Jamii.
Unazungumzia mtu mmoja mmoja au taifa zima? Maana mimi sizungumzii maisha ya mtu mmoja mmoja.
 
Sasa kwanini unasema umasikini ni chanzo cha tabia mbaya kama ulevi ngono n.k wakati inajulikana pesa ndio kishawishi kikubwa cha kufanya hayo mambo?
Masikini ufanya yote hayo Ili apate pesa.Kumbuka umasikini na ujinga uendana.
 
Masikini ufanya yote hayo Ili apate pesa.Kumbuka umasikini na ujinga uendana.
Ni sawa tu na mwenye pesa anaweza kufanya yote hayo kwa sababu ana pesa, kuna watu wanakuwa wachamungu ila wanapopata pesa na Mungu wanamsahau kwa maana wanajiingiza kufanya hayo matendo maovu.

Kijumla umasikini ni mbaya unaweza ukawa chanzo cha hayo mambo ila pia pesa pia ni mbaya wanasema pata pesa tujue tabia yako.
 
Pesa ni kama kisu inategemea na matumizi yako.kisu kinaua,kinakata mboga jikoni
 
Back
Top Bottom