TANZIA Mchekeshaji Pembe afariki dunia

TANZIA Mchekeshaji Pembe afariki dunia

Nimeona youtube hii habari, nikarudi JF kuihakiki, kumbe ni kweli jamaa kavuta...

Anyway, faraja iwe kwa familia yake...
 
R.I.P Pembe, nyie ndio wasanii sasa mnachekesha bila kuvaa madela na mawigi au kupaka injofesi kama wanawake, mzee majuto, pembe, kingwendu, senga, bambo, mtanga na wengine sanaa mmeifanyia kazi hatuna cha kuwadai
 
Pumzika kwa Amani Pembe.
Mifumo mibovu inafanya mnaondoka pasipokufaidi kazi zenu ipasavyo. Wanadamu tuliishi kwa tabasam na faraja ya kazi zako. Daima kazi zako zitabaki milele.
 
Baaasi baba baasi utaua utaua tena ukienda na Imamu Husein na jambia lake yeye hadi baba ake mkwe ni kichapo tu
Hahaha yani wee acha tu. Yani mimi na Imaam Hussein tuko mstari wa mbele kuupigania, kuutetea na kuulinda uislamu halafu taka taka zinafanya mzaha baada ya kufanikisha wao kupata Tawfiq/Tawfeek ( the ability and opportunity to succeed) na kuwa na uhakika wa jannah na firdaus. Yani hawalioni hilo kabisa wakati watu tuna qauli thabeet za kutosha.

Malaria 2

Nyau de adriz

Mwamba hapo chini

images (1).jpeg
 
Apumzike kwa amani, alituburudisha vya kutosha.

Rungu lake liwekwe makumbusho, ikiwezekana lipigwe mnada, pesa ipatikane isaidie familia
 
Mzee Yusufu Kaimu mchekeshaji mkongwe maarufu kama Pembe afariki dunia alasiri ya leo jijini Dar es Salaam. Taarifa zimethibitishwa na Msanii wa Filamu, Vincent Kigosi “Ray” na taratibu za mazishi zinafuata.

=====

Mwigizaji na Mchekeshaji Mkongwe Nchini Tanzania, Mzee Yusuph Kaimu maarufu Pembe amefariki dunia jioni ya leo October 20,2024 katika Hospitali ya Temeke Jijini Dar es salaam alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Baadhi ya Waigizaji akiwemo Vicent Kigosi (Ray) na Mau Fundi wametoa taarifa za msiba huo na kusema taratibu za mazishi zitatolewa baadaye, @AyoTV_ imeongea pia na Katibu wa Chama cha Waigizaji Kinondoni, Jafari Makatu ambaye amethibitisha na kusema “Alikuwa anaumwa alilazwa Temeke Hospital, amefariki kama saa moja iliyopita, alilazwa kama siku tatu nne, na tulikuwa tumepanga kwenda kumuona Kesho baada ya kuambiwa anaumwa”
R. I. P
 
Ila sisi kama wanajamii tunahitaji kujiongeza sana eneo la wasanii kwa jinsi tunavyowatreat.

Huyu gwiji wa uchekeshaji nimeanza kumuona nikiwa bwana mdogo sana tena vidudu. Alikuwa akituchekesha kila ijumaa channel ya CTN.

Yeye Mzee Pembe,Mzee Small,TupaTupa,na Bi Chau. Hawa watu wametufanya siku zetu kuwa za furaha sana kwa vitu na vibweka vyao ambavyo walifanya bila ushawishi wowote ila tu kwa kuchagua kuwa sehemu ya watoa burudani katika jamii.

Cha ajabu watu hawa hufariki katika maisha ya ufukara na kujipapasa bila msaada wowote ule huku wakiwa hawana vyanzo vya mapato kutokana na kazi zao hizi ambazo wamezifanya kwa utashi na kujitolea kwa hali ya juu.

Nadhani ingekuwa ni busara sana kama taasisi au vijana tungekuja na ubunifu wa kimfumo ili hawa watu waweze kupata matunda ya kazi zao in the future ili iwe kama shukurani kwa zawadi yao ya furaha wanayotupatia bila kujua.

R.I.P Legendary Pembe.
 
Back
Top Bottom