Mchele kutoka nje na hatma ya wakulima wetu

Unafikiri ni wakulima basi ndo hufanya hivi ni walanguzi na madalali
 
Nimecheka sana kwa hiyo mchele unaopelekwa nchini ni makapi lakini mchele wanauza wao nje ya nchi sio makapi 🤣🤣🤣
Hapo ndio unapouona ubinafsi wa Mtanzania
 
Kama hamtaki mchele wa nje why huwa mnalalamika mfumuko wa bei? Ila hii nchi no wonder JPM alikua anafanya maamuzi anavyojiskia sababu hamueleweki mnataka Nini.

Juzi tu hapa mmelalamika kivipi mchele upande bei ilihali vita ipo Ukraine? Hapo hapo Tena mnalalamika mchele wa bei rahisi kuingizwa!! Sasa mnataka nini?
 
Kwani wizara ya elimu haikuwepo hadi vitabu vya ngono vimeingizwa mashuleni ndio wanakuja kujua?
Kwanza hakuna kitabu Cha ngono kinatumika mashuleni acheni kupotosha. Pili ni shule Gani ya Kitanzania inatumia hivyo vitabu vya wimpy kid? Yaani kitabu kilichopo IST pekee ndio ulitaka serikali ikijue? Ingekua kinatumika Kila shule mfano Mabala the farmer n.k.obviously serikali ingezuia mapema maana ipo public.

Mifano haifanani kabisa maana kila mtanzania anakula mchele ila ni 0.0000000001 wanasoma kitabu hiko Cha kiingereza.
 
Mchele wa kwetu ni mchele bora sana ukilinganisha na huo wa kutoka nje.Mtanzania hawezi kuzalisha mchele mbovu kwa ladha na harufu na wakati yeye mwenyewe ni mtumiaji wa zao hilo.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]Utafikiri ulishawahi kula huo mchele wa nje na ukafurahia ladha yake.Wenye pesa zetu tutaendelea kula mchele bora wa ndani kwa bei yoyote.
 
Ungejiuliza pia ni sababu zipi zinawapelekea watu wa mataifa mengine kununua mchele wa Tz wa gharama kubwa na kuacha mchele wa nchi zingine wa gharama ndogo ili hali hupo?.
Ukipata jibu ndiyo utaelewa huo mchele unaofurahia ni nini!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…