Mchele kutoka nje na hatma ya wakulima wetu

Mchele kutoka nje na hatma ya wakulima wetu

Oya walioficha mchele uzeni fasta, mchele wa buku buku upo kwenye meli 😀
 
Sio rahisi Mkuu


Leo hii tutachat hapa ni Mwezi February, hadi muda wakulima wanakuja kuvuna inakuwa tayari ni Julai, ambapo huo Mchele wa kibali unakuwa umeshaisha.
Unadhani hawataomba tena?
 
"Msije kutuletea tena ule wa Thailand Nusu kilo manakula watu 18 na unabaki kiporo cha chai"🙌.......pitia Account za Instagram na Facebook za ITV zilizopost hii taarifa usome maoni utajifunza vitu vingi sana. hiyo ni moja ya comment
Kwann usije babuuuu.....huo mchele nautafuta balaa usawa huu
 
Tatizo lilianza pale bei ya mchele ilipopanda, solution ikawa kuruhusu mchele wa nje kuingia. Kwa hiyo wanaoumia ni wakulima kwa sababu mchele utakapoingia utashusha bei ya mchele masokoni
Wanao nufaika na mchele wa 4000 kwa kg sio wakulima ni walanguzi na wafanya biashara tuu.
Hata hivyo fanya hesabu rahisi gawanya kilo hizo kwa nusu ya watanzania uone ni kidogo kiasi gani?
 
Mchele kutoka nje Je tumejiridhisha kwamba uliopo nchini hautoshi?
Je uzalishaji wetu wa mchele ni kiasi gani, mahitaji kiasi gani na upungufu kiasi gani
Hizo tani elf 90 za mchele zitaingizwa kwa muda gani
Je wakulima walioko shamba kwa sasa mchele wao watauza wapi wakikutana na huo wa nje?

Mchele wa nje inaweza kuwa jambo jema ila nakumbuka wosia wa Mwigulu bungeni hivi majuzi alisema mambo ya dharura ni lazima kuwa nayo makini vinginevyo unaweza kubeba na Deal za watu.
Tunatakiwa kujua kwa Nini sisi tuwe na Michele wabei kubwana wa nje uje kwa bei ya chini?
Kwa Nini hatuwezi kuzalisha Michele wa bei ya chini ili pia wananchi wasiumie na bei kubwa na tuweze kuuza nje kma huo unaotoka huko?

Waziri wa viwanda anatakiwa kutuambia ni kwa nini?
 
Acha ujinga wewe,Mimi mpunga nimeuza February hii unasema hatuna mpunga!!..na si peke yangu,mmeshupalia walanguzi walanguzi...yaani wakulima hatuwezi kuhifadhi mazao yetu!!?
Madalali ndio wenye mpunga wakulima wapo shamba mnafikiria sisi tunatoka Yemen hatuijui nchi yetu na tabia za wakulima wetu.
 
Bei ingepanda kwa shilingi 50 tu au 100 tungesema ni kawaida. Wewe mchele unapanda bei kwa 100% yaani kutoka 2000 kwa kilo hadi 4000 halafu unasema nini hapo?!

Hapa suluhu ni mchele kuingizwa tena tani nyingi hadi kilo iuzwe 1000 ili watu wapate chakula. Watu wanakula kwa hofu sana. Food security ipo very low yaani kwasasa tunawasi wasi sambamba na wakimbizi wa huko sudani au watu wanaoishj taifa lenye ukame mkali.
 
Kila kitu kina faida na hasara, tunaangalia kipi kitachukua asilimia kubwa kati ya hivyo yani faida na hasara.
Watanzania takribani milioni 60 wote wanataabika kwa kupanda kwa bei za vyakula wakiwemo wakulima unaowazungumzia. Je hao wakulima ni asilimia ngapi ya watanzania wote? Je tuwaangalie wakulima labda elfu 10 waliopo shambani wasipate hasara huku watanzania 99.99% wakiishi kwa mlo mmoja kwa taabu?
Wakulima walime mazao mengine tusikwazane.
 
Tatizo lilianza pale bei ya mchele ilipopanda, solution ikawa kuruhusu mchele wa nje kuingia. Kwa hiyo wanaoumia ni wakulima kwa sababu mchele utakapoingia utashusha bei ya mchele masokoni
Yaani unaacha kuwaonea huruma raia ambao hawana hatia wanaishi mjini na kutegemea chakula kitokea shamba unawaonea huruma hawa wachuuzi wanao nunua mchele kwa bei ya chini na kuuza mipakani kwa bei ya juu kisha uhaba umetokea wameenda kuuficha mchele ili mfumuko wa bei uwafaidishe.

Naomba tu upambane na hali yako but mchele uigizwe tena mara 100 ya mahitaji ili tukomeshe huu mfumuko wa bei maana tunashindwa kuwaza maendeleo tunawaza tutakula nini leo au familia itakula nini.
 
Hiki kilio sio cha wakulima bali madalali na walanguzi,wakulima chakula washamaliza kuuza tokea mwaka jana, sasa hivi wapo mashambani wanalima.
Yaani hapa mkulima anachezeshwa muziki kwa lazima na hawa madalali na walanguzi.

Muda sio mrefu wakulima wataanza kuvuna.. kutokana na uagizaji wa mchele kutoka nje,kwa hiyo bei ya mpunga/mchele itakuwa chini sana.

Hapa bado mkulima ataumia pia.
 
Yaani hapa mkulima anachezeshwa muziki kwa lazima na hawa madalali na walanguzi.

Muda sio mrefu wakulima wataanza kuvuna.. kutokana na uagizaji wa mchele kutoka nje,kwa hiyo bei ya mpunga/mchele itakuwa chini sana.

Hapa bado mkulima ataumia pia.
Kwangu mimi naona sawa ,ila serikali watakadilia kiwango cha chakula cha kuagizwa let's say kwa miezi miwili au mitatu kwani naamini baada ya miezi hyo hali ya chakula itatengemaa.

Labda watokee wahuni wengine upande wa serikali watumie hili tatizo kupiga hela ila kwangu serikali ipo sawa kabisa,kwani walanguzi/dalali wanawaumiza sana walaji.
 
Kwa Bei ya 3,600? [emoji3][emoji3] kiberiti kilikuwa kinatingishwa [emoji44] acheni tule wa plastic na ninyi mtakula wa kuzalisha wenyewe na familia zenu, tatizo wakulima wetu hawajifunzi au sijui NI wasahaulifu maana kwa awamu ya nne walifanya hivi hivi Tena walimjibu mbovu mpaka Raisi, ulipoletwa mchele wakaanza kulalamika hakuna soko, nashukuru Serikali haikujibu kitu walishusha wenyewe Sasa wajiandae Yale Yale yanajirudia.
Hapa tatizo sio wakulima,tunawaonea sana wakulima. Tatizo ni hawa watu wa kati..madalali na walanguzi, tena humo humo wamo hadi wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa.
 
  • Thanks
Reactions: nao
"Msije kutuletea tena ule wa Thailand Nusu kilo manakula watu 18 na unabaki kiporo cha chai"🙌.......pitia Account za Instagram na Facebook za ITV zilizopost hii taarifa usome maoni utajifunza vitu vingi sana. hiyo ni moja ya comment
Comment za Facebook? Yaani maoni ya vil.aza ndio unachukulia ni facts?
 
Back
Top Bottom