Mchele kutoka nje na hatma ya wakulima wetu

Mchele kutoka nje na hatma ya wakulima wetu

Mchele kutoka nje Je tumejiridhisha kwamba uliopo nchini hautoshi?
Je uzalishaji wetu wa mchele ni kiasi gani, mahitaji kiasi gani na upungufu kiasi gani
Hizo tani elf 90 za mchele zitaingizwa kwa muda gani
Je wakulima walioko shamba kwa sasa mchele wao watauza wapi wakikutana na huo wa nje?

Mchele wa nje inaweza kuwa jambo jema ila nakumbuka wosia wa Mwigulu bungeni hivi majuzi alisema mambo ya dharura ni lazima kuwa nayo makini vinginevyo unaweza kubeba na Deal za watu.
Uje tu mana tuliyataka wenyewe.... 20kg elfu 60000 Mbeya
 
Sidhani kama uko sahihi. Kanuni za kibiashara zinaruhusu uuze e.g. kwa Juma kwa bei kubwa halafu ununue kwa Massawe kitu hicho hicho kwa bei ya chini. Na mzunguko unaendelea.
Yaani nchi au wakulima wanaweza kununua mahindi Iringa kwa bei ya chini kisha kuuza mahindi hayo Himo kwa bei ya juu ile margin wanayopata ndo faida. Vivyo hivyo Tanzania inaweza kuuza mchele Congo DRC kwa bei kubwa halafu Tanzania ikanunua au kuagiza mchele kwa bei ndogo kutoka Japan.
Ni suala la Fursa tu na kuangalia ni kipi cha kufanya ili upate faida.
"You produce what you don't eat and you eat what you don't produce".
Hiyo sasa ndiyo kilimo biashara. Ila Watanzania wamewadharau sana wakulima wanawafanya kama wanalima for charity
 
Ujuha huo, msimu wa mavuno umefika tena mnaingiza mchele wa nje.
 
Waziri wa viwanda na biashara na waziri wa kilimo wanagombea fito wakati wanajenga nyumba moja...😂🤣
Yaani hii nchi inaenda utadhani kila waziri anaserikali yake..😜😛
Naskia wote wameingiziwa 10% zao tayari.
 
Kwa kuwa Wakulima ni mbumbumbu ngoja waendelee kuhenyeka na kuvimbisha matumbo ya vikundi vya wahuni huko Mjini.

Bila kuungana na kuwa na chama chenye sauti Moja ya maamuzi mtaishia kuchezewa na Serikali Kila siku na kuwa maskini milele kama anayosema Mwigulu hapa [emoji116]
Screenshot_20230207-084644.jpg
 
Kuna jamaa alikuwa ametoka canada alikuwa anasema mcheelee kilo Moja elfu 4,nyama na maharagere bei sawaa,UNGA wa ugali bei kilo Moja elfu 2500 mka msifu saaana,bei inashuka sasa ya bidhaa muhimu akatafute cheap politics kwao singida.
 
Hiyo sasa ndiyo kilimo biashara. Ila Watanzania wamewadharau sana wakulima wanawafanya kama wanalima for charity
Wakulima ndio wameamua kujidharau,bila kuwa na chombo Chao Cha sauti wataisoma namba.

Mwaka huu mchele shambani tutanunua 20,000 Hadi 25,000 na hapo ndio mkulima atakoma
 
Mchele wa nje mnaujua lakini!?
Wenye hela zao wataendelea kula mchele bora na mtamu toka hapahapa ndani.
 
Hivyo vibanda vyenu vya kuishi ni telemka tukaze, ndiyo mtaweza kuwa na Maghala ya kuhifadhiwa chakula!? Yaani Wakulima siku hizi mmekua Chawa wa Walanguzi wa chakula sijui kwa nini!!!
Tatizo una taswira ya mkulima wa 1990,pole sana
 
Nadhani kilichofanyika ni kutafuta njia ya muda mfupi kutatua tatizo la mfumko wa bei sokoni.
Ni juzi tu tumelalamika kuwa Serikali imeshindwa kukabiliana na mfumko wa bei kwa maana imeonekana bei ya kilogram 1 ya mchele imefika 3,600.

Hii ina maana Demand iliyopo ya Mchele ni kubwa kuliko Supply iliyopo, kwa kuingiza mchele huo tani 90 ina maana yake Supply itaongezeka kuwa count balance Demand hivyo kuweza kupunguza bei ya mchele sokoni pengine kufikia shilingi 2,600 kwa Kilogramu 1.

Na sio kwamba hivyo vibali vya kuingiza mchele vitaendelea kutolewa, No. Wakulima wakishaanza kuvuna mchele Mwezi Juni - Julai mwaka huu Serikali itazuia kutolewa kwa vibali vya kuingiza Mchele kutoka nje hivyo kulinda Soko la ndani la Wakulima wetu.

Sio kila jambo linalofanywa na Serikali ni baya wakuu, Kumbuka huyo Mhe Rais kabla hajakubali kutoa kibali hicho cha kuingiza Mchele ina maana Wataalamu wa Uchumi na Kilimo watakuwa walimshuri na yeye kujiridhisha.

Kumbukeni Mhe Rais hana Nchi nyingine zaidi ya Tanzania, hivyo hawezi kuona Raia wake wana taabika na yeye kama Mkuu wa Nchi asichukue tahadhali kuwalinda.
 
Hakuna popote nilipokwambia mimi ni mkulima, nimekuzungusha tu kwenye angle upande wa pili naona wewe ndio una panic, kutegemea quality toka nje ya bei rahisi ni ndoto, hapo ni bora kujaza tumbo tu.

Jiandae kuota kitambi cha mchele kitumbo.
Hebu kuwa wazi tu kwa ku declare interest!!kwani TZ ndio nchi ya kwanzq Africa kuagiza mchele nje?miaka yote ZANZIBAR ndio chakula chao na maisha yanakwenda,nenda Rwanda,congo japo sawa ladha yake sio sio kama huu wa kwetu.
 
Bashe ni waziri wa wote maskini na matajiri kwa hiyo Kama bei imeshuka ni zamu ya wengine kupata nafuu mumuache Mtoto wa nzega apige kazi
 
Bashe anatakiwa ajiuzuru hiyo ndio gharama ya kukumbatia mafisadi

Yani alikuwa anatuona wajinga kabisa eti wakulima wanafaidika na nafaka kupanda bei

Mkulima gani anayefaidika wakati hao wakulima walishauza huo mpunga na mahindi tokea yakiwa shambani
 
Nadhani kilichofanyika ni kutafuta njia ya muda mfupi kutatua tatizo la mfumko wa bei sokoni.
Ni juzi tu tumelalamika kuwa Serikali imeshindwa kukabiliana na mfumko wa bei kwa maana imeonekana bei ya kilogram 1 ya mchele imefika 3,600.

Hii ina maana Demand iliyopo ya Mchele ni kubwa kuliko Supply iliyopo, kwa kuingiza mchele huo tani 90 ina maana yake Supply itaongezeka kuwa count balance Demand hivyo kuweza kupunguza bei ya mchele sokoni pengine kufikia shilingi 2,600 kwa Kilogramu 1.

Na sio kwamba hivyo vibali vya kuingiza mchele vitaendelea kutolewa, No. Wakulima wakishaanza kuvuna mchele Mwezi Juni - Julai mwaka huu Serikali itazuia kutolewa kwa vibali vya kuingiza Mchele kutoka nje hivyo kulinda Soko la ndani la Wakulima wetu.

Sio kila jambo linalofanywa na Serikali ni baya wakuu, Kumbuka huyo Mhe Rais kabla hajakubali kutoa kibali hicho cha kuingiza Mchele ina maana Wataalamu wa Uchumi na Kilimo watakuwa walimshuri na yeye kujiridhisha.

Kumbukeni Mhe Rais hana Nchi nyingine zaidi ya Tanzania, hivyo hawezi kuona Raia wake wana taabika na yeye kama Mkuu wa Nchi asichukue tahadhali kuwalinda.
Lazima tu wakulima watakutana na huo mchele
 
Lazima tu wakulima watakutana na huo mchele
Sio rahisi Mkuu

Leo hii tutachat hapa ni Mwezi February, hadi muda wakulima wanakuja kuvuna inakuwa tayari ni Julai, ambapo huo Mchele wa kibali unakuwa umeshaisha.
 
Back
Top Bottom