Mchele kutoka nje na hatma ya wakulima wetu

Mchele kutoka nje na hatma ya wakulima wetu

Una uhakika gani kama huo mchele unaoletwa ni makapi? Nyinyi mchele mnao wauzia Wakenya na Wasomali ni makapi?

Wewe kijana wa Moo mbona unaleta story za kufikirika! Unataka kusema hakuna mamlaka ya chakula na dawa nchini kwa ajili ya kuchunguza ubora wa huo mchele!
Watz kwa kutunga maneno wanaongoza duniani, hapo Zanzibar mchele ni 1900 kwa Kg, wao huagiza nje
 
Hapa ndipo utapata vyakula vya GMO ambavyo wengi hawa vitaki

Kuna miaka huko nyuma walikula mahindi ya njano

Wakati wa shida utakula chochote kikubwa uhai
Kwani vyakula vya gmo vina ubaya gani?
Thibitisha
 
Mchele wa plastic huo.

Kansa kwa sana. Nunua mchele wetu wa kuzalisha wenyewe.
Kwa Bei ya 3,600? [emoji3][emoji3] kiberiti kilikuwa kinatingishwa [emoji44] acheni tule wa plastic na ninyi mtakula wa kuzalisha wenyewe na familia zenu, tatizo wakulima wetu hawajifunzi au sijui NI wasahaulifu maana kwa awamu ya nne walifanya hivi hivi Tena walimjibu mbovu mpaka Raisi, ulipoletwa mchele wakaanza kulalamika hakuna soko, nashukuru Serikali haikujibu kitu walishusha wenyewe Sasa wajiandae Yale Yale yanajirudia.
 
Watz kwa kutunga maneno wanaongoza duniani, hapo Zanzibar mchele ni 1900 kwa Kg, wao huagiza nje
Sasa kama ni hivyo, mbona huku bara tunataka kuagiza mchele kutoka nje halafu watu fulani wanapiga kelele? au historia inataka kujirudia enzi za Mrema(RIP) akiwa waziri wa mambo ya ndani na sukari? Utajiri wa haraka-haraka. Aisee; leteni huo mchele chap achana na hawa walanguzi bhana.
 
Ukiona hivyo jua Kuna bossy nmoja ana meli inaleta mzigo zaidi ya tano elfu 40 ndio wamepush push hadi kupata mzigo kupata kushushwa.

Ila bora iwe soko huria tuu. Maana watu sahivi wanajiongezea bei kama serikali walivyoongeza bei ya mafuta
Hakuna Cha boss Wala Nini hawa wakulima wa mchele wanajisikia Sana ukija mchele wa nje kwa wingi akili zitawakaa, majibu tunayoyapata huko madukani ni ya ajabu Sana hebu uje haraka kwa kweli
 
Hakuna Cha boss Wala Nini hawa wakulima wa mchele wanajisikia Sana ukija mchele wa nje kwa wingi akili zitawakaa, majibu tunayoyapata huko madukani ni ya ajabu Sana hebu uje haraka kwa kweli
Yani tunausubiri huo mchele kwa hamu kubwa sana ili manyanyaso yaishe. Mchele unalimwa hapa-hapa Tz lakini bei na majibu ya hao wauzaji utadhani wanalima wao.
 
Kama tunaruhusu mchele wa njee, basi turuhusu wakenya na waganda waje kuuza cv zao kwa kazi za Tanzanian.

Haiwezekan mwalim English medium mtanzanua namlipa 600,000 kizungu makengeza, wakati walimu waganda nlikuwa nawalipa 250,000
Tunazungumzia mchele ambao ni chakula hayo ya CV ongea na Waziri wa Elimu
 
Kwenye hili naungana na serikali,maisha yamekuwa magumu sana,kuagiza bidhaa kutoka nje kutaleta unafuu bila shaka!
Wanapoleta mchele kutoka nje wasisahau na Maharage,kwani wali huenda pamoja na Maharage🤪.

Kwa akili zetu kwa kweli tuneshindwa kujilisha wacha tulishwe🙌🙌
 
"Msije kutuletea tena ule wa Thailand Nusu kilo manakula watu 18 na unabaki kiporo cha chai"🙌.......pitia Account za Instagram na Facebook za ITV zilizopost hii taarifa usome maoni utajifunza vitu vingi sana. hiyo ni moja ya comment
Kwani mkuu si utakuwa ni uamuzi wako kuununua?kama vipi wewe endelea kununua wa 4000 huo watakula wengine.japo sio kama huo uliousema kwqni zanzibar ndio mchele wao mkuu
 
Kwanini mchele tu? Mbona kwenye bomu la sukari wasiruhusu? Bidhaa za viwandani utasikia tunalinda viwanda vya ndani why not wakulima? Anayeona chakula ni ghali aende shamba akalime chake?
Kama hujui kitu kaa kimyaa!!Sukari kila mwaka lazima karibu tani laki 2 zinatoka nje.Wakulima wangapi wamefaidika na bei hizi za mchele na mahindi?zaidi ya wafanya biashara?!!
 
Serikali iliporuhusu Wasudan na Wakenya wanunue mahindi mpaka vijijini .. mlisema mama anawajali Wakulima! .. Soko. huria!
Leo mama huyohuyo anaagiza mchele ...Soko Huria,mnalia !
Tilieni Dawa iwaingie...na Ndio muwajue Wanasiasa!
 
Hiki kilio sio cha wakulima bali madalali na walanguzi,wakulima chakula washamaliza kuuza tokea mwaka jana, sasa hivi wapo mashambani wanalima.
...Wakulima wa mahindi wameaminishwa kuwa Serikali inawapenda ,Kwa kupanda Kwa Bei ya mahindi..subiri Kenyq walete mahindi Toka Brazil ,utaona gunia lamahindi litauzwa elfu 30,000/
Changamoto za wakulima Tz haziwezi tatuliwa kwamihemko ya msimu ya Wanasiasa!
Siku Watanzania ...wakulima ,watakapo vua minyororo ya utumwana ujinga ndipo Watawalawatakapo Anza kutumia akili kutatua matatizo ya wakulima na Kilimo!
 
Nashauri mchele wa nje uje ili ubalansi bei, iwe between 1800-2500,Then sasa tutengeneze mizania mipya ya kiasi gani kiruhusiwe kutoka nje na kiasi gani kiwe hakiuzwi nje. Kilichotokea nadhani hesabu za kuuza nje zilizidi kiasi kinacho takiwa kuelea ndani ya nchi.
 
Mchele wa nje inaweza kuwa jambo jema ila nakumbuka wosia wa Mwigulu bungeni hivi majuzi alisema mambo ya dharura ni lazima kuwa nayo makini vinginevyo unaweza kubeba na Deal za watu.
Msoga gang, a. k. a Wazee wa ma deal. Shame on you,CCM.
 
Acha ujinga wewe,Mimi mpunga nimeuza February hii unasema hatuna mpunga!!..na si peke yangu,mmeshupalia walanguzi walanguzi...yaani wakulima hatuwezi kuhifadhi mazao yetu!!?
Hivyo vibanda vyenu vya kuishi ni telemka tukaze, ndiyo mtaweza kuwa na Maghala ya kuhifadhiwa chakula!? Yaani Wakulima siku hizi mmekua Chawa wa Walanguzi wa chakula sijui kwa nini!!!
 
Back
Top Bottom