Mchele kutoka nje na hatma ya wakulima wetu

Mchele kutoka nje na hatma ya wakulima wetu

Kati ya maamuzi yaliyo fanywa vyema na kwa wakati sahihi ni hii kuagiza mchele. Let market determine demand. Hali ni mbaya huku mtaani.
Serikali iwapangie bei wafanya biashara. Isije kuwa ni hii hii ya 3000+
 
Una uhakika gani kama huo mchele unaoletwa ni makapi? Nyinyi mchele mnao wauzia Wakenya na Wasomali ni makapi?

Wewe kijana wa Moo mbona unaleta story za kufikirika! Unataka kusema hakuna mamlaka ya chakula na dawa nchini kwa ajili ya kuchunguza ubora wa huo mchele!
Kwani wakati tunalishwa kitumbo hapakuwepo na mamlaka ya chakula na dawa?

Bado naona umekurupuka, unataka quality kwa bei rahisi, hiyo kitu haipo.
 
Shida ni kwamba wakulima wameahindwa kuungana kuwa na chama Cha kuwatetea na kuwa na Nguvu ya kula ya veto na uamzi kwenye kura..

Wakulima wamekuwa wanachezewa na Serikali, yaani imagine Serikali inasikiliza watu wa Mjini wanaolalamika huko kwenye Twitter ambao hata hawazidi 30% ya watu wote..

Matokeo yake wakulima wataishia kuwa maskini Kila siku Kila mwaka.
 
Kati ya maamuzi yaliyo fanywa vyema na kwa wakati sahihi ni hii kuagiza mchele. Let market determine demand. Hali ni mbaya huku mtaani.
Serikali iwapangie bei wafanya biashara. Isije kuwa ni hii hii ya 3000+
Sasa wewe unasema "let market determine demand" halafu wakati huo huo unasema " Serikali iwapangie bei wafanyabiashara".....una maana gani??
 
Itakuwa ngumu kivipi???Wewe zalisha kwa wingi uwezavyo,nunua kwa wingi uwezavyo,kama faida ipo kuna shida gani?
Mkuu, kuna mkulima ana kahawa yake anataka kuuza Uganda kwenye bei nzuri,
Anazuiwa kuuza, analazimishwa kuuza kwenye chama cha ushirika,

Lakini mkulima wa mahindi, na mchele anaruhusiwa kuuza popote,
Kama ruhusa itolewe kwa wakulima wote,

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
 
Fungua masoko yote acha market iamue bei, kama serikali inataka kumsaidia mkulima imwondolee/ kumpunguzia kodi zote na impe ruzuku za mbolea na vifaa vya kilimo,wakulima wakishindwa watafute kazi nyingine wafanye
 
Tatizo lilianza pale bei ya mchele ilipopanda, solution ikawa kuruhusu mchele wa nje kuingia. Kwa hiyo wanaoumia ni wakulima kwa sababu mchele utakapoingia utashusha bei ya mchele masokoni
Sasa c ndio biashara wwe unataka bei iwe juu kama ilivyo ili iweje kwa wananchi wa kawaida,lete mchele mama ili bei za vyakula iweze kuwa salama.
 
Mchele wa plastic huo.

Kansa kwa sana. Nunua mchele wetu wa kuzalisha wenyewe.
Mbona ni rahisi sana kutofautisha mchele wa plastic na Mchele halisi? Atakayeleta mchele wa plastiki kama hautakuwa umezuiliwa bandarini atakutana na walaji ambao wanaufahamu. Watu wameshajanjaruka wanajua hata kutofautisha fedha feki na fedha halali; sembuse mchele?
 
Mara nyingi mchele wa nje hauna ladha nzuri. !! Walete tu !
 
Una uhakika gani kama huo mchele unaoletwa ni makapi? Nyinyi mchele mnao wauzia Wakenya na Wasomali ni makapi?

Wewe kijana wa Moo mbona unaleta story za kufikirika! Unataka kusema hakuna mamlaka ya chakula na dawa nchini kwa ajili ya kuchunguza ubora wa huo mchele!
Mkuu; Walitunyanyasa sana na bei zao; sasa wameanza kupanic. Wanatoa kashfa na kuuhafifisha mchele kutoka nje eti ili ss walaji tuuone ni mchele duni haufai. Watakaa sana.
 
Mara nyingi mchele wa nje hauna ladha nzuri. !! Walete tu !
Mtu hali ladha; Nakumbuka kuliwahi letwa mchele kutoka Japan na watu waliupenda -ulikuwa ni msafi na hauna chuya. Sasa huu wa kwetu ambao wanaoupigia chapuo umejaa mchanga, umevunjika-vunjika n.k. Hata hivyo michele yote (wa nje na wa ndani) itakuwepo sokoni halafu na sisi walaji tutaishindanisha kwa ubora na bei.
 
Kabisa !
 
Huwa zinawatosha wao wenyewe huko serikalini sasa wangefanya hivi toka mwaka jana hiyo habari ya inflation ya chakula si isingefikia kuwa janga kama ilivyo kwa sasa.

Ajabu yenyewe bei ya chakula itaanza kushuka kabla ya huo mchele wa kuagizwa kufika, kutokana na hofu za walioficha stock zao kuanza kuona madhara ya ongezeko la supply mbeleni na kujiwahi kwa kuuza wao kwanza.

Free market ni kuruhusu wazalishaji wauze wanapotaka na kuachia suppliers pia kununua wanapotaka. Watu washindane kushusha bei za production.

Kilichokua kinaendelea kwa kuzuia importation hakikuwa na lengo la kuwatetea wakulima, bali kuwalangua wananchi na kuongeza ugumu wa maisha kwa sie wenye kipato kidogo.
 
Kati ya maamuzi yaliyo fanywa vyema na kwa wakati sahihi ni hii kuagiza mchele. Let market determine demand. Hali ni mbaya huku mtaani.
Serikali iwapangie bei wafanya biashara. Isije kuwa ni hii hii ya 3000+
Mkuu; usiwe na presha. Huko sokoni, ikiwa Supply ni kubwa kuliko Demand;
bei itashuka tuu. Kumbuka walaji wapo daima siku zote i.e. mchele unahitajika siku zote. Na endapo mfanyabiashara ataona hailipi akae pembeni i.e atakuwa thrown out of the competitive market chap akafanye huduma nyingine.
 
Hata ukiwa mchele wa chuma walete tu!
Kweli aisee watu walishachoka na hizi bei za kupaa za mchele eti ni wa humu nchini na Haupatikani.
Sasa wameanza kugwaya na kuzua maneno ya kashfa eti ni wa plastiki. Mm nasema hata ungekuwa wa kuchongwa, Uletweee.
 
Back
Top Bottom