Mchengerwa aagiza Mchakato wa uanzishwaji wa Mamlaka ya Uendelezaji wa Jjiji la Dar uanze

Dar es salaam ianzishwe mara ngapi, Dar imebanana mno, hayo ilibidi yakafanyike Dodoma, ingesaidia kupunguza msongamano wa watu na changamoto zisizo za lazima. Watu wakienda kujenga mabondeni watasema serikali haihusiki...💀
 
Jiwe alikuwa mwehu yule.

Alikuwa anatafuta gia ya kutaka kukipatia hadhi ya jiji kile kile Kijiji bjs cha Chato.

Alikuwa mshamba na mjinga sana yule jamaa.
Sijaelewa ilikuwaje Dar ikawa jiji ilihali haikuwa kuwa Wilaya wala Manispaa?
 
Hayo ndiyo maamuzi sahihi CCM acheni kukurupuka katika maamuzi nchi si mali ya kiongozi bali ni mali ya Raia.
 
Kwenye hili nakubaliana na Mchengerwa,jiji la Dar es Salaam lipo tofauti na majiji mengine. Majiji mengine wamechukua lile eneo la mjini ndiyo imepewa hadhi ya jiji na kuziacha zile halmashauri za pembezoni kuwa manispaa na halmashauri za miji lakini Dar es Salaam yote ni mjini hivyo huwezi kuifanya wilaya ya Ilala tu ndiye iwe jiji halafu uiache Kinondoni, Oysterbay,Masaki n.k eti ziwe katika manispaa hii siyo kweli.

Tena napendekeza liundwe jiji kama ilivyokuwa awamu ya kwanza na ya pili kwamba halmashauri ya jiji iwe moja na iwe na kanda za Ilala,Kinondoni, Temeke,Ubungo na Kigamboni lakini Mkurugenzi ni mmoja tu hao wa kanda waitwe vyovyote lakini bosi wao ni mmoja tu isiwe kama jiji lilovunjwa na Magufuli ambapo wilaya zote zilikuwa manispaa na jiji likawa lipo kisanii tu lisilo na jukumu wala nguvu yoyote kwa sababu kila halmashauri ilikuwa ndiyo wenye ardhi,shule,vituo vya afya n.k.
 
Dar ilishapitia hatua zote hizo kabla wengi wenu hamjazaliwa.

Wakati nchi unapata uhuru Mkoa wa pwani kwenye eneo la Mzizima ndio kilikuwa na watu wengi 30,000.
 
Hizo Wilaya za Dar ziwe majijini, halafu kuwe na Greater Dar es Salaam halafu hizo nyingine ziwe miji ndogondogo.
 
Kumbe wakati inaamuliwa Jiji la DSM kuvunja, Makamo wake hakupendezwa au yeye hakuwa sehemu ya Serikali?

Kuanzisha tena Jiji la DSM pamoja na uwepo wa Faida zake, lakini ni gharama Kwa Serikali.

Ni mzigo Kwa Wananchi
 
Jiji wakati wa awamu ya tano lilivunjwa kwakuwa lilikuwa linahang tu halina vyanzo vyake binafisi wala eneo la kiutawala na lilikuwa linategemea manispaa kuingiza kipato.

Lilikuwa mzigo tu. Hawa wanasiasa wanatuchanganya na Dana Dana zao kila siku.

Kwa staili hii ya kupiga hatua moja na kurudi nyuma maendeleo tuyasikie kwa wengine tu.

Huyo mchengerwa apambane na mwendokasi kwanza wateja wapo ila mabasi hakuna.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…