PreGE2025 Mchengerwa achukizwa na maamuzi ya RC Chalamila, ahoji ametoa wapi mamlaka?

PreGE2025 Mchengerwa achukizwa na maamuzi ya RC Chalamila, ahoji ametoa wapi mamlaka?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa ametengua ruhusa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila, kuruhusu magari binafsi kupita kwenye barabara za mabasi yaendayo haraka (mwendokasi).

Video: Habari Digital
RC ana tabia ya kukurupuka,
Wa Dar aibu ni yenu wote,
 
Hapa Mohamed Mchengerwa kajivua nguo hadharani....yupo uchi.
Tunaomba ajibu maswali yafuatayo:
1. Wakati Bashungwa anatoa ruhusa magari ya kawaida yapite mwendokasi yeye alikua wapi?

2. Kama gari la tani 30 linaharibu barabara na inaanza kuvunjika, sasa uimara na ubora wa barabara hiyo uko wapi?

3. Ina maana wizara yake ilishindwa kusimamia ujenzi wa barabara ya viwango?

4. Kumsema kiongozi mwenzie hadharani anadhani ni sahihi?

5. Tukisema wewe Mchengerwa ni bogus tutakuwa tunakosea?
 
Kwani yeye mchengerwa kuaribu uchaguzi S/ za mtaa tz nzima ayo mamlaka alipewa na nani?

Uyu rafiki yangu Chalamila tangu akiwa RC Mbeya mpaka yupo dar na Mchengerwa akili zao zipo na tofauti gani?

Tofauti ni moja tu ,mmoja ni waziri na mkwe wetu , mwingine wenda yupo pale kuonesha taswira ya mwendazake.

Ogopa mtu anaeweza waita Tumbili ambao hawafugi nyumbani kwake nakutaka kuwakamata kwa mikono yake kwa kuwadanganya na ndizi mbivu ila wakachomoa.

Chalamila nje ya uongozi mtu poa sana ,ila sasa akisha kuwa ndani ya cheo sijui akili anapelekaga wapi .

Shida kuna watu wanataka endeleza midundo ya mwendazake kwa sababu alikua nao ila hawajui asilimia 85 ya watz walimchoka sana .
Hao tumbili waliotegeshewa wakachomoa ndiyo kina nani hao?
Jf ina vimbwenga hii? 😁😁😆😆
 
Hao tumbili waliotegeshewa wakachomoa ndiyo kina nani hao?
Jf ina vimbwenga hii? 😁😁😆😆
Nenda you tube ,mkuu ,utawaona Tumbiri nyumbani kwake Chalamila Iringa na ndizi zake akitaka watega Tumbiri ili awakamate ila wakachomoa.

Ni kipindi ambacho alikua hajateuliwa kuwa mkuu mkoa Mwanza kama sikosei
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa ametengua ruhusa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila, kuruhusu magari binafsi kupita kwenye barabara za mabasi yaendayo haraka (mwendokasi).

Video: Habari Digital
Asante Mh.Waziri
 
Unaongea na Dereva wa loli usiweke uchawa mbele kwenye mambo ya msingi na kama unabisha nenda Rwanda ukaone.
Dereva wa roli yaani Rwanda wana bara bara bora kuliko ile ya Iringa au mlima Kitonga naomba ufafanuzi hapa kidogo..
 
Sijaelewa wao ilitakiwa waelezane huko kwenye vikao vyao kama mtu kakosea kuliko kuja public huyu anaongea hili na yule lile inakua kama hawapo pamoja..
 
Muheshimiwa Waziri nimatumaini yangu kuwa kesho ama ndani ya mwezi huu brt itaanza kuserereka kwenye barabara alizoruhusu zitumike kwakuwa bado kulikuwa hamna hizo mwendo haraka.
Unafiki tu huo ni alikuwa wapi mala tu baada ya hilo tamko kutolewa leo karibia miezi 6 ndio anaibuka?!!!
 
Wanataka kumkabidhi mwarabu barabara mbichi Kuna haja gani ya kukopa hela kutengeneza barabara ambazo hazina magari ya kupitia hapo. Kwa nini wasijaze magari kwenye hizi barabara zilizopo na wakipata faida hiyo faida itengeneze barabara nyingine. Hapa naona wanataka kutingiza kwenye madeni wake wamkabidhi mwarabu bure amwage magari na apate faida sisi tuje tulipe madeni Bure tu...
mkiachiwa mnaweza kuuendesha huo mradi? sio mnalilia vitu hamviwezi. Tuwape ili muache mabasi yamejaa matope na mifumo ya tikiti haifanyi kazi?
 
Ninacho ongelea ni uimara wa barabara ndio maana huwezi kuona mizani zimejazana barabarani kama huku kwetu.
Kaka unaona bara bara zao ni imara kwa sababu truck zinazoingia Rwanda ni chache na pia nyingi hawazidishi mizigo kama huku..
 
Kaka unaona bara bara zao ni imara kwa sababu truck zinazoingia Rwanda ni chache na pia nyingi hawazidishi mizigo kama huku..
Trucks za mashariki ya DRC nyingi zinapitia hapo ukiangalia upende wa Tanzania kuanzia Nyabugombe hadi Rusahunga ni mabonde matupu hata ile Barabara ya Tabora Manyoni kupitia Kigwa teyari imeshakuwa na mabonde na imeshabonyea.
 
Kwani kinachozuia kuanza usafiri wa mwendokasi mbagala ni nini haswa?
 
Back
Top Bottom