PreGE2025 Mchengerwa achukizwa na maamuzi ya RC Chalamila, ahoji ametoa wapi mamlaka?

PreGE2025 Mchengerwa achukizwa na maamuzi ya RC Chalamila, ahoji ametoa wapi mamlaka?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Mimi nafkiri ifike wakati wamrudishe yule mzee Aggrey Mwanri na apewe huu mji. Kuteua Machizi huku kunatuumiza sisi mbeleni, mtu anaropoka na ana mikwara utadhani kitu gani bana!

Huyu Mr. Mchengerwa sio mtata na ni mara chache sana mpaka kumchana mtu hadharani namna hii. RC ajitafakari, na akiwa kwenye kujitafakari wahusika wamlete Mwanri wampe hili jiji huenda atafanya vizuri. Alikuwa na uwezo sana!
 
Ni ukosefu wa uelewa kuzuia barabara ambayo haitumiki kwa makusudi yaliyo lengwa, huku foleni ikipoteza pesa
nyingi ambazo serkali inadhani sio zao.
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa ametengua ruhusa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila, kuruhusu magari binafsi kupita kwenye barabara za mabasi yaendayo haraka (mwendokasi).

Video: Habari Digital
Kwani yeye mchengerwa kuaribu uchaguzi S/ za mtaa tz nzima ayo mamlaka alipewa na nani?

Uyu rafiki yangu Chalamila tangu akiwa RC Mbeya mpaka yupo dar na Mchengerwa akili zao zipo na tofauti gani?

Tofauti ni moja tu ,mmoja ni waziri na mkwe wetu , mwingine wenda yupo pale kuonesha taswira ya mwendazake.

Ogopa mtu anaeweza waita Tumbili ambao hawafugi nyumbani kwake nakutaka kuwakamata kwa mikono yake kwa kuwadanganya na ndizi mbivu ila wakachomoa.

Chalamila nje ya uongozi mtu poa sana ,ila sasa akisha kuwa ndani ya cheo sijui akili anapelekaga wapi .

Shida kuna watu wanataka endeleza midundo ya mwendazake kwa sababu alikua nao ila hawajui asilimia 85 ya watz walimchoka sana .
 
TOKA MAKTABA:

Jumatano , 23rd Oct , 2024


Barabara za Mwendokasi Zianze Kutumika​

Na Mwandishi wetu

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila ameagiza barabara za mwendokasi ambazo zinasubiri mabasi ya BRT mwendokasi zianze kutumika kwanzia leo ili kuokoa foleni kwa muda wa asubuhi na jioni.

barabara.jpg

Ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya usiku katika wilaya za jijini Dar es Salaam ambapo maagizo hayo yakiwa ni utekelezaji wa ushauri kutoka kwa Waziri wa Ujenzi mheshimiwa Innocent Bashungwa ambapo aliagiza kwamba barabara za mwendokasi zinazosubiri mabasi kutumika ili kupunguza foleni.

“Mheshimiwa waziri Innocent Bashungwa ametoa maelekezo kwa sababu kuna baadhi ya barabara kwa sababu mabasi bado hayajafika sasa tuangalie utaratibu wa kuingiza mabasi na kuingiza mabasi madogo kwa mfano barabara ya kutoka Mbagala jijini Dar es Salaam.

Naomba niweke clear hapa sio barabara zote ni barabara ambazo bado hazijapata mabasi.” amesema Albert. Chalamila.


Sambamba na hilo mkuu wa mkoa wa DSM Albert Chalamila, ameagiza wakandarasi wote waliopewa tenda za ujenzi wa miundombuni ya serikali jijini Dar es Salaam kuhakikisha wanafanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha inakamilika mapema kabla ya mvua kuanza kunyesha na kuepuka kisingizio cha kutokamilisha miradi kwa sababu ya mvua.

Ziara hiyo ya mkuu wa mkoa inakuwa ni ziara yake ya kwanza ikiwa ametangaza ziara ya usiku ya siku tano kukagua miradi ya maendeleo katika wilaya za jiji la dar es Salaam
Source : EATV
 
1742580541932.jpeg

Waziri wa TAMISEMI mheshimiwa Mohamed Mchengerwa - Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam nilikustahi ... lakini nimekusamehe.
 
TOKA MAKTABA:

Jumatano , 23rd Oct , 2024


Barabara za Mwendokasi Zianze Kutumika​

Na Mwandishi wetu
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila ameagizqa barabara za mwendikasi ambazo zinasubiri mabasi ya mwendokasi zianze kutumika kwanzia leo ili kuokoa foleni kwa muda wa asubuhi na jioni.

barabara.jpg

Ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya usiku katika wilaya za jijini Dar es Salaam ambapo maagizo hayo yakiwa ni utekelezaji wa ushauri kutoka kwa Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa ambapo aliagiza kwa barabara za mwendokasi zinazosubiri mabasi kutumika ili kupunguza foleni.

“Mheshimiwa Innocent Bashungwa ametoa maelekezo kwa sababu kunabaadhi ya barabara kwa sababu mabasi bado hayajafika sasa tuangalie utaratibu wa kuingiza mabasi na kuingiza mabasi madogo kwa mfano barabara ya kutoka Mbagala jijini Dar es Salaam.

Naomba niweke clear hapa sio barabara zote ni barabara ambazo bado hazijapata mabasi.” Amesema Albert. Chalamila.


Sambamba na hilo mkuu wa mkoa wa DSM Albert Chalamila, ameagiza wakandarasi wote waliopewa tenda za ujenzi wa miundombunu ya serikali jijini Dar es Salaam kuhakikisha wanafanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha inakamilika mapema kabla ya mvua kuanza kunyesha na kuepuka kisingizio cha kutokamilisha miradi kwa sababu ya mvua.

Ziara hiyo ya mkuu wa mkoa inakuwa ni ziara yake ya kwanza ikiwa ametangaza ziara ya usiku ya siku tano kukagua miradi ya maendeleo katika wilaya za jiji la dar es Salaam
Source : EATV
Wanatuamisha upepo tu ht mm nlimsikia Bashungwa akitoa pendekezo shida iliyopo ni kupita magari makubwa kuhus madogo na yale ya abiria mbona sio tabu.

My country Tz🤣😂🤣😂
 
Wanatuamisha upepo tu ht mm nlimsikia Bashungwa akitoa pendekezo shida iliyopo ni kupita magari makubwa kuhus madogo na yale ya abiria mbona sio tabu.

My country Tz🤣😂🤣😂

TOKA MAKTABA :
Maelekezo kibao kutoka kwa waziri, viongozi wa CCM n.k hadi RC ana changanyikiwa


MCHENGERWA: CHALAMILA SHUGHULIKA NAO NITAKUULIZA WEWE🥴​


View: https://m.youtube.com/shorts/a3tzsqlXxEk
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa ametengua ruhusa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila, kuruhusu magari binafsi kupita kwenye barabara za mabasi yaendayo haraka (mwendokasi).

Video: Habari Digital
Ka mkwe hako. Na kenyewe kana kibesi na utukufu
 
Wanataka kumkabidhi mwarabu barabara mbichi Kuna haja gani ya kukopa hela kutengeneza barabara ambazo hazina magari ya kupitia hapo. Kwa nini wasijaze magari kwenye hizi barabara zilizopo na wakipata faida hiyo faida itengeneze barabara nyingine. Hapa naona wanataka kutingiza kwenye madeni wake wamkabidhi mwarabu bure amwage magari na apate faida sisi tuje tulipe madeni Bure tu...
Udini tuu umekujaa mbn migodi yote ina milikiwa na wazungu umenufaika nini?...Mwafrika huna cha kumkwepa mtu mweupe awe mzungu au mwarabu au mchina kaongezeka sahv kwny ukoloni huu mamboleo lazima ujae kwny 18 zao...
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa ametengua ruhusa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila, kuruhusu magari binafsi kupita kwenye barabara za mabasi yaendayo haraka (mwendokasi).

Video: Habari Digital
Amemchokoza mkwe wa Rais 😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom