PreGE2025 Mchengerwa achukizwa na maamuzi ya RC Chalamila, ahoji ametoa wapi mamlaka?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
RC ana tabia ya kukurupuka,
Wa Dar aibu ni yenu wote,
 
Hapa Mohamed Mchengerwa kajivua nguo hadharani....yupo uchi.
Tunaomba ajibu maswali yafuatayo:
1. Wakati Bashungwa anatoa ruhusa magari ya kawaida yapite mwendokasi yeye alikua wapi?

2. Kama gari la tani 30 linaharibu barabara na inaanza kuvunjika, sasa uimara na ubora wa barabara hiyo uko wapi?

3. Ina maana wizara yake ilishindwa kusimamia ujenzi wa barabara ya viwango?

4. Kumsema kiongozi mwenzie hadharani anadhani ni sahihi?

5. Tukisema wewe Mchengerwa ni bogus tutakuwa tunakosea?
 
Hao tumbili waliotegeshewa wakachomoa ndiyo kina nani hao?
Jf ina vimbwenga hii? 😁😁😆😆
 
Hao tumbili waliotegeshewa wakachomoa ndiyo kina nani hao?
Jf ina vimbwenga hii? 😁😁😆😆
Nenda you tube ,mkuu ,utawaona Tumbiri nyumbani kwake Chalamila Iringa na ndizi zake akitaka watega Tumbiri ili awakamate ila wakachomoa.

Ni kipindi ambacho alikua hajateuliwa kuwa mkuu mkoa Mwanza kama sikosei
 
Asante Mh.Waziri
 
Unaongea na Dereva wa loli usiweke uchawa mbele kwenye mambo ya msingi na kama unabisha nenda Rwanda ukaone.
Dereva wa roli yaani Rwanda wana bara bara bora kuliko ile ya Iringa au mlima Kitonga naomba ufafanuzi hapa kidogo..
 
Sijaelewa wao ilitakiwa waelezane huko kwenye vikao vyao kama mtu kakosea kuliko kuja public huyu anaongea hili na yule lile inakua kama hawapo pamoja..
 
Muheshimiwa Waziri nimatumaini yangu kuwa kesho ama ndani ya mwezi huu brt itaanza kuserereka kwenye barabara alizoruhusu zitumike kwakuwa bado kulikuwa hamna hizo mwendo haraka.
Unafiki tu huo ni alikuwa wapi mala tu baada ya hilo tamko kutolewa leo karibia miezi 6 ndio anaibuka?!!!
 
mkiachiwa mnaweza kuuendesha huo mradi? sio mnalilia vitu hamviwezi. Tuwape ili muache mabasi yamejaa matope na mifumo ya tikiti haifanyi kazi?
 
Ninacho ongelea ni uimara wa barabara ndio maana huwezi kuona mizani zimejazana barabarani kama huku kwetu.
Kaka unaona bara bara zao ni imara kwa sababu truck zinazoingia Rwanda ni chache na pia nyingi hawazidishi mizigo kama huku..
 
Kaka unaona bara bara zao ni imara kwa sababu truck zinazoingia Rwanda ni chache na pia nyingi hawazidishi mizigo kama huku..
Trucks za mashariki ya DRC nyingi zinapitia hapo ukiangalia upende wa Tanzania kuanzia Nyabugombe hadi Rusahunga ni mabonde matupu hata ile Barabara ya Tabora Manyoni kupitia Kigwa teyari imeshakuwa na mabonde na imeshabonyea.
 
Kwani kinachozuia kuanza usafiri wa mwendokasi mbagala ni nini haswa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…