Mcheza karate mahiri zaidi aliyetikisa mchezo wa karate Tanzania. Khalifa Kiumbe Moto (Chief Kiumbe)

Mcheza karate mahiri zaidi aliyetikisa mchezo wa karate Tanzania. Khalifa Kiumbe Moto (Chief Kiumbe)

ivi ile michezo ambayo anacheza kama boyka kwenye movie ni aina gani aiseee... yani kama ile haipo kwenye hayo mliotaja hayo naona yatakua hayana maana kabisa
 
Mkuu inafaa kufatilia karate ni mchezo wa aina gani. Hakuna mcheza karate anaeweza kupigwa na mtu asie mtaalam wa ngumi mtaani. Ndo maana kukaanzishwa kick boxer. Kwa kua ili karate iwe mchezo wa jukwaani inabidi uwekewe sheria nyingi sana. Watu kadhaa walipoteza maisha kutokana na mchezo huu. Tanzania kulikua na master zero ambae alifariki kutokana na madhara aliyoyapata baada ya pambano na jimmy Castro. Kuna Jimmy Castro alifariki baada ya kupata madhara ya pambano na Khalifa kiumbe moto. Ndo ikakatazwa kupigana karate kama karate. Ni kick boxer Au karate iwe kama maonyesho
je huyu anamuweza scorpion?
 
je huyu anamuweza scorpion?
Kiongozi kushinda Au kushindwa kwenye pambano ni kitu tofauti na uwezo. Unaweza kufanya makosa ukala kitasa Au kiki ya kukumaliza. Kitu nnachozungumzia kwa huyu bwana ni kua uwezo wake ni mkubwa sana. Amekua chini ya wakufunzi mbali mbali wakubwa nchini na nje ya nchi. Kwa uwezo aliokua na speed aliokua nayo kipindi Kile angeweza kupanda jukwaani na mpiganaji yoyote. Popote
 
mwana mwanza anaemkumbuka master clay,huyu alikuwa habari ya mjini bwana alikuwa mpole mstaarabu lakini shughuli yake haikuwa yakitoto

Habari ya mjini??..ahaa nimekupata sasa kumbe mjini mwanza? basi sawa
 
ivi ile michezo ambayo anacheza kama boyka kwenye movie ni aina gani aiseee... yani kama ile haipo kwenye hayo mliotaja hayo naona yatakua hayana maana kabisa
wansemaga inafanana sijui na kombat hata mi siujui naskiaga tuu
 
a82e0bd671fed1e87b8db88ee9c8b881.jpg
c0c156588bdbf46c0e26c7045af5f4b3.jpg
Sasa hiyo chifu kiumbe ndo kafikia hapo kuvaa miwani kama vioo vya mbele vya mandolini?
 
Kidogo naona anapata kuperuzi ulimwengu wa martial arts ulivyo
hongera sana...ila Shaurinj, Karate, combat, Taekwondo, Muai Thai, Kung Fu, Gurujuuu....hiyo
tuliisha stafu kitambu kirefu.
Majina yenyewe kuyaandika hujui. Itakuwa mchezo wenyewe?
 
Dhumuni na lengo sio kuoneshana umwamba wako mafundi na wametulia tu nia ni kukuza na kuendeleza mchezo ila watu wengi wajifunze
 
kwani aliyeko jela si huyu chief kiumbe, yule aliyekuwa na wolper, au sio huyu, nauliza tu
 
kwani aliyeko jela si huyu chief kiumbe, yule aliyekuwa na wolper, au sio huyu, nauliza tu
Sio huyu hata kidogo. Wengi wametumia jina hilo kutokana na kujifafanisha kwa kumpenda huyu. Alipokamatwa huyo unayemsema na kuona kwenye gazeti wengi tulistuka. Tukamtafuta sensei akasema nipo. Ni vijana walionipenda hao. Yani ni kama watu kujiita dame mkuu. .... mpaka huyu maarufi anaeimbwa kila siku hilo jina katoa hapo kwa huyu sensei
 
A
Je unamkumbuka khalifa kiumbe moto? Ndie mchezo karate, kick boxer na judo mahiri zaidi aliyewahi kutokea tanzania. Alivuma sana mwishoni mwa miaka ya tisini. Jina lake Ni Khalifa.... mjukuu wa mzee khalifani kiumbe. Msomi wa dini ya kiislamu aliyekua maarufu sana.

khalifa Kiumbe alikua na speed ya ajabu iliyompa haki ya kuitwa moto. Ndio sababu akabatizwa khalifa kiumbe moto.

Na Kila move aliyofanya Au pigo alilopiga jukwaani alisikika kwa sauti ya chini kama ya kufoka lakini yenye command akisema motooo. ..

Kutokana na speed aliyokua nayo na ukweli kua yeye ni mjukuu wa chief. Chief khalfani kiumbe wadau wakamwita chief kiumbe. Kumbuka kiumbe ni jina lake.
Na ni Kutokana na huyu ndipo wakatokea watu kadhaa waliojiita kiumbe moto, chief kiumbe na kadhalika.

Moja kati ya pambano ambalo halijawahi kitokea tena tanzania ni pombano lake na Jimmy Castro ambae alisalimu amri round ya saba baada ya kunyanyaswa vibaya jukwaani. Kiumbo khalifa alionekana mdogo. Lakini kama alivyowahi kusema. Puto kubwa linatolewa upepo na sindano ndogo sana. Huyu bwana alikua balaa. Huyu bwana alikua moto. Huyu bwana ni chief kiumbe. Motooo. .
db349b759b2ff7b1ba9c610e9239ef38.jpg
Alizicheza wapi? Aje Mtaani Aoneshe Kwa Vitendo Dhidi yangu halafu ndio utajua wapiga karate wapo wengi tu mahiri ila ni wa kimya kimya - no misifa. Try me
 
A

Alizicheza wapi? Aje Mtaani Aoneshe Kwa Vitendo Dhidi yangu halafu ndio utajua wapiga karate wapo wengi tu mahiri ila ni wa kimya kimya - no misifa. Try me
Ni kweli unayosema. Ila haikua tangazo la kutafuta pambano. Hatafuti sifa. Tuliomfahamu tumemkumbuka kwa kua ni mwalimu wetu. Kama una uwezo wa kimpiga uweke kwa mwenye uwezo unaolingana na wako. Asante sana
 
Back
Top Bottom