Huyu ndio Mwana Kigoma
Makali ya Bernad Kamungo yalianzia hapa katika uwanja huu wa Nyarugusu, kwenye ardhi ya mkoa wa Kigoma.
Alizaliwa January 1, 2002, Kasulu kijiji cha Nyarugusu.
View attachment 2711820
...........
Hapa ni Kigoma Kasulu,
Huu ndio uwanja wa Nyarugusu ambapo makali ya Bernard Kamungo yalianzia hapa, kwasababu yeye alizaliwa hapa Kigoma, ni Mwana Kigoma.
View attachment 2711823
..........
Uwanja wa Nyarugusu Kasulu, uwanja uliomkuza na kumlea MwanaKigoma Bernard Kamungo.
View attachment 2711827
................
Bernard Kamungo, namba 30 BHN
Hapa sasa alikua amefika Marekani kutokea Kigoma, Nyarugusu
View attachment 2711830
................
Kwa mara ya kwanza Tanzania ikaanza kung'aa nchini Marekani kupitia michezo, Bernard Kamungo akaanza kuipeperusha bendera ya Tanzania na kugonga vichwa vya habari nchini Marekani. Huyu ni mwana Kigoma.
View attachment 2711832
................
Wachezaji tisa wa Tanzania wanaocheza nje ya Nchi kwenye picha moja.
» Bernard Kamungo (jezi no 5)
'Mwenye bleach' kutoka katika klabu ya
FC Dallas ya ligi kuu Nchini Marekani inakuwa mara yake ya kwanza kuitwa Taifastars
. Mtoto wa Kigoma
View attachment 2711834
..................
Bernard Kamungo (Mtoto wa Kigoma, shujaa wa Lake Tanganyika) akiwa na Mbwana Samata katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania.
View attachment 2711837
..............
Huyu ndio mwanakigoma na Mshambuliaji wa Kimataifa wa timu ya Tanzania anayekipiga katika klabu ya
FC Dallas inayoshiriki Ligi Kuu ya Marekani, Bernard Kamungo ameendelea kuwa gumzo kutokana na uwezo wake ambapo aliifungia timu yake goli katika sare ya 4-4 dhidi ya
Inter Miami CF anayochezea Lionel Messi.
Kutoka kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu mkoani Kigoma alikocheza soka mtaani hadi kucheza soka nchini Marekani, safari yake inaonekana kama filamu ya michezo yenye mabonde na milima.
Kamungo alisajiliwa Dallas FC mwaka 2022 ambapo yeye na familia yake walihamia Texas, Marekani mwaka 2016.
Nyota huyo ameendelea kuwa na msimu mzuri ambapo Januari 2023 aliitwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania.
Kutoka kigoma Tanzania Hadi marekani na kuwa mfalme wa
FC Dallas
Kutoka kucheza chandim Hadi kucheza na Lionel Andrés Messi, na kuonesha upinzani mkubwa walipokutana uwanjani.
Anaitwa Bernad Kamungo mshambuliaji wa
FC Dallas na timu ya Taifa ya Tanzania.
View attachment 2711841