Mchezaji kutokea Mkoani Kigoma akutana na Leonel Messi uso kwa uso uwanjani

Yaani kwa kuwa anajitambulisha yeye ni Mtanzania lakini hata mamlaka hazitaki kuondoa utata bali kaitwa timu ya Taifa, wanaanza kushabikia ni Mtanzania.

Wajuzi naomba mnisaidie maswali haya.

Tanzania haina uraia pacha, je huyo mchezaji yeye inakuwaje anatoka Marekani kuja kuchezea timu ya Taifa? Anatumia passport ya Tanzania au USA mpaka sasa?

Kwa uzoefu tu, wale wakimbizi waliokuwa wakipelekwa USA na Canada wengi wao wakifika huko wanapewa uraia wa nchi hizo! Sasa huyu mchezaji yeye hakupewa huo uraia mpaka sasa?

Pia, ieleweke, Mtanzania wa kijijini si rahisi kuhamia USA na Canada. Lakini tunaambiwa wazazi wa mchezaji walihamia USA 2016 wakitokea Nyarugusu.

Ieleweke, ilikuwa rahisi kwa hao wazazi kuhamia USA kupitia mgongo wa kuwa wakimbizi na hata huko walipofika wanatambulika nchi walizotoka na siyo Tanzania kwa sababu Watanzania hawakuruhusiwa katika mipango ya kuwapeleka wakimbizi USA na Canada. Walichukuliwa nchi zilizokuwa na vita mfano Burundi, DRC, Rwanda.

kilichokuwa kikifanyika, baadhi ya Watanzania wa Kigoma walikuwa wanahonga wanaingia kwenye mfumo wa kusafirishwa kama wakimbizi lakini walikuwa wana idea na nchi hizo zenye vita mfano lugha, utamaduni, maeneo mana kuna interview.

Kama huyo mchezaji ni Mtanzania labda alipitia huu mfumo wa kujichomeka ni mkimbizi feki, lakini huko USA lazima alishapewa uraia na alitambulika nchi nyingine na siyo Tanzanka mama angejulikana ni Mtanzania amejichomeka kwa Warundi angerudishwa Tanzania hata baada ya kufika huko. Je huyo mchezaji anayo passport ya Tanzania?

Hoja hapa, tubadilike Watanzania turuhusu uraia pacha siyo vizuri kuvunja sheria kwa baadhi ya mambo. Hapa uraia pacha ungeruhusiwa tungempokea vizuri tu huyo Mrundi!
 
Duh Muha mtani wangu, nikiangalia picha yako ya Nyarugusu na hiyo ya Marekani nabaki kusema 'Mungu alakoze chane'
 
Huyu dogo wazazi wake ni wakongolee

Ila yeye alizaliwa kwenye kambi ya wakinbizi nyarugusu,hata shule alisoma kwa french.

Leo nilikuwa na mwanangu maskani mkongolee ben kampigia Whtsap call wakawa wanaongea kibembe.

Inshort alienda USA mwaka 2016 kama waendavyo wengine wakimbizi.

Pia bongo alikuja mwezi wa nne mwaka huu kukamilisha taratibu za malipo ili acheze timu ya taifa ya tanzania

Inshort ben kanunuliwa taifa staz,mchongo wote Mbwana Samatta anaujua yeye ndy codinator wa dogo na ndy alimpokea airport dsm mwezi wa nne.
 
Dogo ni mbembe na leo alikuwa anaongea na mbembe mwezio wasapcall.

Dogo alikuwa anasema ni bora achezee taifa staz kwasabb drc hawez kupata namba pia bongo kapewa kibunda cha kutosha samatta ndy kamtengenezea dili.

Stk kufunguka zaidi

Nikweli aliondoka 2016 nyarugusu camp
 
Thibitisha hilo kwa facts na sio blah blah.
 
Huyu alizaliwa kwenye kambi ya wakimbizi,maisha ya mtu hayana tafusiri hakuna ajuaye kesho yake
 
Huyu alizaliwa kwenye kambi ya wakimbizi,maisha ya mtu hayana tafusiri hakuna ajuaye kesho yake
Ndiyo maaana wakimbizi wote pale Nyarugusu wanaza kwenda Ulaya tu.
 
Naona uliyeandika hapa utakuwa wa kigoma. Huyu Ni sifa za Taifa Zima Ila zingekuwa mbaya ndio zingekuwa za wanakigoma pekee kwenye uzuri ama sifa Ni Taifa Kama Taifa na sio kigoma Kama kigoma
Mwandishi anaweza akawa Zitto Kabwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…