Mchezo Mchafu: Kuna kina mama huwatuma mabinti kuingia vyumba vya wapangaji wa kiume, fumanizi la video hufanyika ni aidha utoe pesa ama unaenda jela

Kuna mchezo mpya siku hizi kina mama hasa wenye nyumba za kupanga huwa wanawafundisha mabinti wawe wanaingia vyumba vya wapangaji wa kiume kwa gia ya kuomba kuomba kuangalia tv, kuomba kuwafanyia usafi, kuomba kuingiziwa nyimbo au muvi, n.k. (mbinu kibao) sambamba na mitego ya kuwapandisha hamu ya kuwataka kimapenzi.

Mabinti hawa wengine wametolewa vijijini huko, ukiwauliza miaka washafundishwa waseme wana miaka 19 na hawasomi, siku ya tukio utaambiwa wana miaka 16 na wanasoma.

Wakiingia vyumbani, mama mwenye nyumba anastua marafiki zake kama wawili waje, wengine wanaleta kabisa mtendaji wa mtaa ama polisi ambao washanogewa na pesa za huu mchezo mchafu.

Wakiingia ndani humo hupewi hata nafasi ya kujieleza kila mtu anasema umelala na binti mwenye umri chini ya miaka 18, utajieleza kwamba mlikuwa mnacheki tu tv ila wao watakomaa umelala na binti mdogo, utajitetea alikwambia ana miaka 19 hapo utaoneshwa cheti (hata cha mchongo) kazaliwa 2007.

Hapo kuchomoka uwe na zaidi ya laki 3, kama una ka usafiri ama una vaa vizuri na una kazi tegemea kucheua milioni.

Wengine hutumia mbinu hii kuwatupia jela vijana waliopishana nao kauli
Dah!! aisee umakini unaitajika sana
 
Siku hizi hata siwapi kazi ke kwa ofisi yangu ,Toka mlinzi ,cleaner mpaka mawakili it's a male zone ,Huwa na avoid instances za kijinga Kama hizi .
Kingine eti msichana anionbe Hela sijui hajala au amepotea au simu ampigie mamake amtumie nauli Huwa sifanyi .
Sitaki mind games nnzaoona siku hizi , usaidizi kwangu umeishia kwa jinsia yangu tu labda mke na watoto wangu wangu wa kike ,sawia pia ukipatana na wa kwangu ww mwanaume usimsaidie hata maji anitafute mie au ke wenzake .
Cheka na Ile jinsia nyingine utajipata kizimbani ukiuma Chuma
Umeshakuwa mkubwa umepakia maarifa mengi kichwani

Wahanga wengi huwa ni vijana under 30 hawa bado bado wanaelekea kwenye utu uzima kiakili.
 
Kuna mchezo mpya siku hizi kina mama hasa wenye nyumba za kupanga huwa wanawafundisha mabinti wawe wanaingia vyumba vya wapangaji wa kiume kwa gia ya kuomba kuomba kuangalia tv, kuomba kuwafanyia usafi, kuomba kuingiziwa nyimbo au muvi, n.k. (mbinu kibao) sambamba na mitego ya kuwapandisha hamu ya kuwataka kimapenzi.

Mabinti hawa wengine wametolewa vijijini huko, ukiwauliza miaka washafundishwa waseme wana miaka 19 na hawasomi, siku ya tukio utaambiwa wana miaka 16 na wanasoma.

Wakiingia vyumbani, mama mwenye nyumba anastua marafiki zake kama wawili waje, wengine wanaleta kabisa mtendaji wa mtaa ama polisi ambao washanogewa na pesa za huu mchezo mchafu.

Wakiingia ndani humo hupewi hata nafasi ya kujieleza kila mtu anasema umelala na binti mwenye umri chini ya miaka 18, utajieleza kwamba mlikuwa mnacheki tu tv ila wao watakomaa umelala na binti mdogo, utajitetea alikwambia ana miaka 19 hapo utaoneshwa cheti (hata cha mchongo) kazaliwa 2007.

Hapo kuchomoka uwe na zaidi ya laki 3, kama una ka usafiri ama una vaa vizuri na una kazi tegemea kucheua milioni.

Wengine hutumia mbinu hii kuwatupia jela vijana waliopishana nao kauli
Si muache ushamba kuingiza visichana magetoni?
 
Back
Top Bottom