Mchezo wa Simba na Yanga kuchezwa tena, Mashabiki kurudishiwa tiketi zao

Mchezo wa Simba na Yanga kuchezwa tena, Mashabiki kurudishiwa tiketi zao

Mechi inarudiwa vipi wakati sheria inaitaka TFF kuipatia Yanga SC pointi tatu maana walifika uwanjani muda wa mchezo na Simba SC hawakutokea. Yanga SC nitawashangaa wakicheza huu mchezo.
Kila muwamba ngoma huvutia kwake,hata Simba pia wanadai point tatu.
Bandiko hili la serikali linatoa maelekezo,mojawapo ya mawlekezo ni mechi kurudiwa.
Kama Yanga ama Simba watagoma basi adhabu itawahusu.
 
Kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za FIFA Serikali hazipaswi kuingilia mambo ya soka au kuyaendesha mashirikisho ya mpira wa miguu ya nchi husika.
Hiyo ina maana kwamba hapa kwetu Tanzania, Serikali hairuhusiwi kuingilia maamuzi ya TFF.
TFF walipaswa kuikatalia Serikali iliposema mchezo wa Yanga na Simba usogezwe mbele kwa masaa 2 maana kanuni na taratibu haziruhusu.
Kutokana na hili sakata, Yanga wanapaswa kupewa point 3 na magoli 3 sababu wao wapo sahihi kikanuni. Nitawashangaa sana Yanga kama watakubali kurudia mechi hiyo. Nawashauri Yanga, ikiwa TFF itakataa kuwasikiliza kuhusu kupewa point 3 basi waiandikie FIFA barua ya malalamiko halafu tuone moto wake.
Yanga msikubali kuchezeshwa hii ngoma ya TFF na Serikali, komaeni mpewe points zenu 3 na magoli 3 sababu wenye makosa siyo ninyi, ni hao TFF na Serikali. Ninyi mlifuata kanuni na taratibu kama zinavyosema.
Kateni rufaa, andikeni barua FIFA watu waadabishwe, heshima irudi. Hao TFF wamejisahau sana hao akina Wallace Karia na wenzake.
Yanga chomeni utambi FIFA, hii ni nafasi yenu adimu ya kurudisha heshima ya soka la bongo.
Hivi unaweza kutaja mkuu baadhi ya hukumu tunazoweza kupewa na Fifa na namna zitakavyoikomoa Tff?
 
Kufikia sasa Yanga SC ndio imebeba hatima ya mpira kwa Tanzania aidha ifungiwe au lah! Yanga SC wakilisogeza hili CAF au FIFA, mpira utaanza kusahaulika.

Mimi sio shabiki wa vilabu hivi ni shabiki wa Kagera Sugar lakini TFF imekuwa na mambo ya hovyo yanayokera, nashangaa watu kulichukua hili kwa mapenzi kuliko mtazamo wa kiuhalisia.
Sasa kama mpira wa Tanzania tukifungiwa Yanga aliyepeleka malalamiko yeye anafaidika vipi au Fifa watamchagulia ligi nchi nyingne awe anashiriki wakati sisi tumefungiwa au Fifa watatengua urais wa Karia pale Tff na kuwapa Yanga nafasi kuweka mtu sahihi .....hebu tuambie mkuu wananchi tufanye maamuzi maana tumechoka
 
Unadhani hiyo kanuni ina apply kila mahala?
Mfano kuna threat ya kiusalama imebainika masaa mawili kabla ya mchezo, napo tutadai masaa 24 kuahirisha mchezo?
Hilk tishio la kiusalama lilikuwepo? Kama lili kuwepo muda umesha pita, hatustahili kufahamu sasa ili kwa wakati mwingine tuwe na tahadhari ya kutosha?
 
Hilk tishio la kiusalama lilikuwepo? Kama lili kuwepo muda umesha pita, hatustahili kufahamu sasa ili kwa wakati mwingine tuwe na tahadhari ya kutosha?
Wewe unawezaje kuchukua tahadhari juu ya hatari yoyote inayoweza kulikumba Taifa?
 
Wale wapumbavu waliokuwa wanasema serikali HAIUSIKI Na TFF mmeona?.
Tunaishukuru Yanga kwa kugoma siku ile kuna ujumbe umeshaifikia taasisi ya tff, serikali ilishashindwa kwenye michezo ndio maana timu ya taifa inafungwa kila leo
 
Si mlisema serikali HAIUSIKI Na michezo wala TFF?.
Tunaishukuru Yanga kwa kugoma siku ile kuna ujumbe umeshaifikia taasisi ya tff, serikali ilishashindwa kwenye michezo ndio maana timu ya taifa inafungwa kila leo
 
Muone huyu nae, hapa duniani kitu pekee ambacho hakihusiani na elimu(maarifa) ni swala la kufanya mapenzi tu, kwakua hata panzi, mbwa, kuku, Bata wanafanya bila hata kufundishwa.

Soka linahitaji watu wenye weledi na Elimu.
Kama ni hivo ulivyosema basi hata mapenzi yanaitaji elimu..acha akili za ubuyu,inamana we hauwezi kung'amua mambo mpaka upate elimu??

mambo mengine tujaribu kushirikisha maarifa yetu zaidi pasina kusingizia elimu. ebu nambie A'level inasaidia vipi wewe katika soka???

mambo ya kipaji hayaingiliani kabisa na mambo ya kusoma soma ndo mana. Messi, Ronaldo, mbwana samata na hata akina Ryan gigs (mchambuzi sasa hivi) hawana hizo elimu za kwako..

kikubwa tunadharauliana wabongo kwa vile, tunachukuliana poa na link kati ya wasomi na wasio wasomi.
 
Back
Top Bottom