Mchimbaji aula kwa kupata mawe ya Tanzanite ya thamani ya Tsh. Bilioni 7.8

Mchimbaji aula kwa kupata mawe ya Tanzanite ya thamani ya Tsh. Bilioni 7.8

Hata yule aliyepiga almasi shinyanga angeenda uza Belgium angepata pesa ndefu zaidi...
Any way waridhike na walichopata

Ova
Shida iliyopa arusha wanunuzi wote wa kihindi wameondoka ndio wangelipa pesa kufuru,wameondoka na bei imeporomoka sana toka gram 1.2m mwaka jana mwezi huu,
Sasa hivi gram ni laki 5 mpka 4 jiwe zuri
 
Kumbe ndio Tanzanite ilivyo. Kijijini kwetu ndani ndani huko nilishawahi ona mawe ya namna hii mahali fulani..

Na hadi hivyi sasa sijaona mtu akijihusisha kuchimba haya mawe, Mungu akinijalia mwezi ujao nitafika kuyahakiki...
 
Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila amesema kuwa leo wizara inamtabua mchimbaji mdogo wa madini ya Tanzanite, Saninniu Laizer kuwa bilionea baada ya kupata mawe makubwa mawili yenye thamani ya shilingi bilioni 7.8.

Mchimbaji huyo amepata mawe hayo mawili ambapo moja lina kilo 9.2 ambalo thamani yake ni shilingi bilioni 4.5 na la pili lina kilo 5.8 lenye thamani shilingi bilioni 3.3.

“Na utofauti wake ni kwamba mawe ya uzito huo hayajawahi kupatikana kwenye machimbo ya Tanzanite tangu machimbo yaanze na yamepatikana ndani ya ukuta wa Mirereni kwahiyo hii ni rekodi mpya ya kupata mawe yenye uzito huo,” amesema Prof. Msanjila.

Profesa Msanjila amesema kuwa sekta ya madini inauwezo wa kumfanya mtu kuwa bilionea kwa haraka, ameongeza kuwa kunahitaji kuwa uwekezaji wa dhati katika sekta hiyo.

Tunaongea kuhusu bilioni pesa ya madafu au ya dola ya marekani?
 
Shida iliyopa arusha wanunuzi wote wa kihindi wameondoka ndio wangelipa pesa kufuru,wameondoka na bei imeporomoka sana toka gram 1.2m mwaka jana mwezi huu,
Sasa hivi gram ni laki 5 mpka 4 jiwe zuri
Hivi mengi Matunda bado yuko huko mererani

Ova
 
Wale jamaa hawajaja kupinga.

Natania🚶🚶
 
Kumbe ndio Tanzanite ilivyo. Kijijini kwetu ndani ndani huko nilishawahi ona mawe ya namna hii mahali fulani..

Na hadi hivyi sasa sijaona mtu akijihusisha kuchimba haya mawe, Mungu akinijalia mwezi ujao nitafika kuyahakiki...
Hiyo sio tanzanite utakua umeona cheap gemstones ziko sehemu nyingi sana
 
Hiyo sio tanzanite utakua umeona cheap gemstones ziko sehemu nyingi sana

Mkuu kwa uelewa wangu sidhani kama itakuwa cheap germstome. Ipo ndani ya eneo letu porini huko kanda ya ziwa.

Nikifika nitakutumia picha kwanza uhakiki
 
Back
Top Bottom