Mchimbaji aula kwa kupata mawe ya Tanzanite ya thamani ya Tsh. Bilioni 7.8

Mchimbaji aula kwa kupata mawe ya Tanzanite ya thamani ya Tsh. Bilioni 7.8


Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila amesema kuwa leo wizara inamtabua mchimbaji mdogo wa madini ya Tanzanite, Saninniu Laizer kuwa bilionea baada ya kupata mawe makubwa mawili yenye thamani ya shilingi bilioni 7.8.

Mchimbaji huyo amepata mawe hayo mawili ambapo moja lina kilo 9.2 ambalo thamani yake ni shilingi bilioni 4.5 na la pili lina kilo 5.8 lenye thamani shilingi bilioni 3.3.

“Na utofauti wake ni kwamba mawe ya uzito huo hayajawahi kupatikana kwenye machimbo ya Tanzanite tangu machimbo yaanze na yamepatikana ndani ya ukuta wa Mirereni kwahiyo hii ni rekodi mpya ya kupata mawe yenye uzito huo,” amesema Prof. Msanjila.

Profesa Msanjila amesema kuwa sekta ya madini inauwezo wa kumfanya mtu kuwa bilionea kwa haraka, ameongeza kuwa kunahitaji kuwa uwekezaji wa dhati katika sekta hiyo.

Serikali imenunua mawe hayo kutoka kwa mchimbaji huyo na yatawekwa katika makumbusho ya taifa
Hizi juhudi za serikali ya awamu ya tano kuboresha mazingira kwa wachimbaji wadogo wadogo zinaonesha mafanikio Sasa sector ya madini inakua kwa Kasi na kuongeza Pato la taifa Viva Magufulu 2020-2025
 
Siku ya juzi viunga vya mererani kulishuhudiwa maajabu ambayo hayajatokea kwa miaka 15

Baada ya mchimbaji mdogo anayejulikana kwa jina la Laizer kunyan kuibuka na madini ya Tanzanite yenye uzito wa Kg 15

Kwakuwa njia za kihuni za kutoroshea madini nairobi zimethibitiwa ilibidi BOT iingilie kati na kununua madini hayo kwa thamani ya Bilion 7

Hongera Magufuli uliahidi kuzalisha mabilionea ahadi zako zimeanza kutimia

Hongereni pia wana Arusha kwa kuongeza idadi ya mabilionea

Tafakari kabla ya kuandika. Huenda iko siku mkeo atajifungua utamshukuru mtu badala ya Mungu
 
Kule pemba kuna mmoja nasikia amekamatwa na karafuu ya magendo gunia 30
Sijui kweli?
 
Kwa hiyo dhamani ni sawa mawe hayaangaliwi ukubwa tu Bali na quality ndo maana bei hutofautiana
Kwa uzito wa mawe hayo kulipwa 7.7 Billion bado kapunjwa kodogo, mi nilitaka kumpa 10 Billion ambapo London stock market wali pledge kunilipa 15 Billion
 
Huko makumbusho ya taifa hiyo tanzanite inaenda kuyeyuka na kuwekwa fake.

Si tuliambiwa BOT itaanzisha utaratibu wa kuhifadhi madini na vito,why makumbusho ya taifa?

BTW:Kuna uwezekano tanzanite kubwa zaidi ya hiyo ilishawahi kupatikana sema jinsi hii biashara ilivyokuwa kabla ya 2015 ilikuwa siyo rahisi hata kujua nani kapata nini.
 
Hahahaa hapa ndio kwenye msingi wa habari nzima, kutaka kuleta mantiki kuwa ukuta wa mirerani umekua wa faid, kwahio huo ukuta uko hadi chini kabisa huku alikokuta huo mzigo?
Nadhani anachota kuelezea Prof. Msanjila ni kwamba kama huo ukuta usingekuwepo, uwezekano wa hayo mawe kupitishwa na kuuzwa kinyamela na kwa magendo ulikuwa mkubwa sana na hivyo kuikosesha nchi kodi husika na hivi sasa sifa kuwa mawe makubwa kama hayo yanapatikana MERERANI NCHINI TANZANIA SIYO INDIA AU AFRIKA YA KUSINI kama ilivyokuwa hapo nyuma.
 
Ukiliangalia vizuri hili jiwe utaona limekatwa nasio kwa maana ya uhujumu bali ni security ya biashara iliofanyika jamaa katoa mzigo Zaid ya huu kwa ninavyoona
IMG_20200624_142223_125.jpg
 
Mungu ameshainua mtu wake.Mungu ni mwema
Sasa nashauri Serikali kupitia Wizara ya Madini na Kituo cha Uwekezaji wamsaidie huyu Bilionea mpya kuiwekeza hiyo bilioni saba ili izae Zaidi na izalishe ajira kwa wana Mererani na Simanjiro kwa faida ya Tanzania yetu au siyo wana JF?
 
Kitakachomtafuna huyo bilionea ni umasikini wa akili!

Ni kishauri kitukimoja,kama haumjui mtu..funga doma achakuropoka..huyo ni tajiri muda mrefu sana..hapa mererani anashimo analohudumia zaidi ya miaka 10,na anawahudumia wafanyakazi 400,usilete akili zako za madaftari then unakuja kujaji watu wengine
 
Ila huyo laizer ingawa kanizidi hela, mbona amekaa kishamba sana, hela inafuata watu washamba washamba..dooh
 
Ni kishauri kitukimoja,kama haumjui mtu..funga doma achakuropoka..huyo ni tajiri muda mrefu sana..hapa mererani anashimo analohudumia zaidi ya miaka 10,na anawahudumia wafanyakazi 400,usilete akili zako za madaftari then unakuja kujaji watu wengine
mzee una uzoefu hapo mererani.nataka nije kutalii
 
Sasa nashauri Serikali kupitia Wizara ya Madini na Kituo cha Uwekezaji wamsaidie huyu Bilionea mpya kuiwekeza hiyo bilioni saba ili izae Zaidi na izalishe ajira kwa wana Mererani na Simanjiro kwa faida ya Tanzania yetu au siyo wana JF?
hahaaa[emoji2][emoji2][emoji2]
 
Back
Top Bottom