Mchimbaji mdogo Laizer akabidhi jiwe lingine la Tanzanite lenye uzito wa kilo 6.33 Serikalini

Mchimbaji mdogo Laizer akabidhi jiwe lingine la Tanzanite lenye uzito wa kilo 6.33 Serikalini

Wana apolo sasa hv wanamlia timing tu ili siku ikifika wamzamie kwake, bila shaka yapo mengi.
 
Inaweza ikawa anayo mengi ndani hii ni baada ya milango ya kupeleka nje kufungwa sasa amekosa chansi ya kusafirisha nje na soko kufunguliwa hapa nchini kaamua kuanza kuyatoa ,serikali fuatilieni huyu mtu.
Haya ni mawazo yangu tuu niko tayari kukosolewa.
Ujue yeye sio mchimbaji. Haingii ndani ya shimo mara kwa mara ila ana wasimamizi. Hilo jiwe haliwezi kuwa SIRI. Pale shimo likitoa mali watu wote walioko chini wanajua. Wasipojua watalipwaje? PIA MIGODI YOTE WANAPATA HABAR HASA JIWE KUBWA. Naskia likitema wachimbaji wanatolewa pembeni ili mwenyewe aje achukue yale makubwa na vile vodogovidogo anawaachia wale wachimbaji wanaitwa nyoka wakinyakuana.
 
Jiongeze kidogo ...kwanini ni kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu? Je huu sio utakatishaji fedha ili chama fulani kipate pesa ya uchaguzi?
Jiulize kwanini Laizer ambaye ni tajiri tayari? Huyu ana makandokando yake hivyo hawezi kupiga kelele kwenye kufanikisha dili
Huyu ni tajiri tayari hivyo hataonesha tofauti ya kabla na baada
Hii ni reincarnation ya deep green, Kagoda na Anglo gold
Ahaa
 
unachekesha kweli..katika makabidhiano jana uliona igp sirro, pamoja na mkuu wa majeshi, hio inakupa picha gani, huyu ni mzawa na mzalendo wa kweli na analindwa na serikali, nyie endeleeni kupiga soga huku wengine wakiendelea kuongezea ubilionea
Siasa ile mkuu wakuu wa vyombo vya ulinzi na mfanya biashara wapi na wapi
 
Ujue yeye sio mchimbaji. Haingii ndani ya shimo mara kwa mara ila ana wasimamizi. Hilo jiwe haliwezi kuwa SIRI. Pale shimo likitoa mali watu wote walioko chini wanajua. Wasipojua watalipwaje? PIA MIGODI YOTE WANAPATA HABAR HASA JIWE KUBWA. Naskia likitema wachimbaji wanatolewa pembeni ili mwenyewe aje achukue yale makubwa na vile vodogovidogo anawaachia wale wachimbaji wanaitwa nyoka wakinyakuana.
Ungejua madini yanavyochimbwa usingesema hivyo eti mgodi ukikaribia kutema wanatolewa wote[emoji2][emoji2][emoji2]
 
Huyu tayari alishatajirika sana na Mall kubwa walijenga yeye na mdogo wake pale sakina

Kwahiyo huyu si mchimbaji mdogo
 
Huyu Leiza, wampe mgodi wote tu, Kwanza hatoroshi madini,lkn pia hapendi kuwauzia wengine ispokuwa anaiuzia serikali pekee, Kwa nini asipiwe hiyo migodi akaiendesha yeye kama Mtanzania mzalendo?
Labda aendeshe mgodi wa kokoto,unafikiria kuendesha mgodi ni sawa na kuendesha gari....kuna migodi ya wachimbaji wadogo merarani inatumia 70m mpka 100m kwa mwezi mmoja
 
Hapana nielewe nipo kwenye hili game napambana,kipindi kile cha yale mawili kweli yalitoka 3 ila moja lilifichwa ila lilikuja kupatikana na aliekamatwa nalo alikaa ndani ila baada ya hayo mawe nadhan week 3 zilizopita alitoa tena madini mojawapo ni hili la leo
Hili lilikua kwenye production ya mwanzo na zile kilo 9,angalia block lilivyo..sasahivi wanatoa mawe hata nusu kilo haifiki ni kama mkondo umekata
 
Ni kwasababu haufahamu ni kiasi gani kampuni kama ile aliyoileta Mkapa ya Tanzanite1, wanayaibua kiasi gani hadi usawa huu! Hayo ya Laizer ni cha mtoto!
Wale kwa mwezi walikua wanapakua hata 50kg ...mana wafanyakazi walikua wanaiba mawe makubwa mtu mmoja anaweza toka na jiwe la 300m
 
Tukio hili liko mubashara Clouds tv na Channel ten.

Viongozi wengi wamehudhuria wakiongozwa na Dotto Biteko waziri wa madini.
Wengine ni Dr Mpango waziri wa fedha, CDF General Mabeyo, IGP Sirro na wengine wengi.

Mwenye mzigo si mwingine ni yule yule mchimbaji mdogo Laizer na uzito wa hii Tanzanite ni kilo 6.33

Maendeleo hayana vyama
Laizer ana siri ila hatak kusema uyu dogo ni either mshirikina au mwizi huwez kuwa mchimbaji mdogo wakat tayar ushalamba billion kadhaa
 
Back
Top Bottom