Mchimbaji mdogo Laizer akabidhi jiwe lingine la Tanzanite lenye uzito wa kilo 6.33 Serikalini

Mchimbaji mdogo Laizer akabidhi jiwe lingine la Tanzanite lenye uzito wa kilo 6.33 Serikalini

Uyu jamaa sio mchimbaji mdogo ana watalaam kutoka china ana fanya nao kazi mda Sana haya mawe washauza Sana apo kwa jirani sema kwa sasa mambo yamekuwa tyt!
Mambo ya uhujum uchumi yame watisha!
Kumuita mchimbaji mdogo ni siasa tu!
Unamaanisha yule jirani aliekuwa anaongoza kuuza madini ya tanzanite duniani?
 
safi upo sahihi, mimi ndo nipo huku mirerani, hili walilificha ili wakauze nje, na wangepata hela nyingi zaidi ya lile ka kwanza, sema tu muingiliano uliotokea huko chini ndo siri ikafichuka na serikali kuingilia kati. Na pia muelewe laizer sio kama yeye ndo anapata hela kubwa kuliko wote ni hapana,, laizer yeye ni mwenye mgodi, ila kuna wahudumiaji mgodi na hao huwa wana percent kubwa zaidi ya lizer,, unaweza kuta kwenye ile bilioni saba yeye laizer akaambulia tatu tu, na nne ikaenda kwa wahudumiaji,, ila hili jiwe la sasa lina mgogoro na watu wanne, ni stori ndefu nikielezea hapa, na sivuri kiusalama.
Hilo alipata pamoja na yale mengine. Sema hili walificha naona walitaka kulitorosha sema serikali ina masikio marefu.
 
Sipingani na Laizer ' Kuyaibua ' hivi haya Mawe ya Thamani, ila kwa Sisi ' Critical Thinkers ' tayari tumeshaanza kupatwa na Hofu juu ya Kitu fulani.
Leo umeongea kwaakili naamini usemi wa saa mbovu huwa inapatia majira sometimes.
 
johnthebaptist hivi kweli mtu anayemiliki mpaka"Mall" eneo sakina "Opposite" Seven Up bado ni mchimbaji mdogo?
Inategemea na level ya uwekezaji.. anatumia vifaa gani na ukubwa wa eneo lake. Madini unaweza ukashangaa umechimba hata kwenye ukubwa wa chumba cha kulala ukapata jiwe.
 
hayo mawe wanayapata tangu zamani, zaidi ya kilo hizo wanazotangaza, ila walikua wanayavunja vunja, wanagawana kila mtu apate,, na tanzanite one ndo alikua anayatoa mengi tu, ila huwa anayavunjavunja vipande vipande, kwa sababu za kibiashar, ni stori ndefu nikielezea sababu za biashara kivipi.
Tanzanite 1 yeye anapiga hadi kilo 50
 
Wala usipatwe na hofu hakuna figisu zozote hapo,uzuri wa tanzanite ukidumbukia kwenye mtaro basi ni ya kuchota tuu,kampuni ya tanzanite one ilikuwa inatoa madini zaidi ya hayo mkuu
Wanasemaga kuna mkanda..ukiupata huo we ni billionea mwanzo mwisho.. ndio mabilionea kina msuya waliuana sababu hiyo..huyo laizer ashukuru ulinzi umeimarishwa.
 
Huyo Mmasai atatuua kwa presha Tulishaanza kumsahau kaibuka tena, kama vipi akapekuliwe ndani kwake kama ana madini mengine Wayanunue yote wamalizane nae tupumzike na mambo ya kurushana roho🤪🤦🏃
 
Kwahi
Na ili kuwe na Mabilionea inabidi pia kuwa na Mafukara kama Sisi ili Mzani wa Kiuchumi na Dhana yake nzima Ukamilike na ndivyo ilivyo Kitaaluma.
Kwahiyo Leo wewe ni mchumi Kitaaluma? Maana jamiiforums unajitambulisha kwamba wewe ni usalama wa taifa (kachero) japo wapo ut wachumi 🤣🤣🤣🤣
 
Share kidogo mkuu
hayo mawe wanayapata tangu zamani, zaidi ya kilo hizo wanazotangaza, ila walikua wanayavunja vunja, wanagawana kila mtu apate,, na tanzanite one ndo alikua anayatoa mengi tu, ila huwa anayavunjavunja vipande vipande, kwa sababu za kibiashar, ni stori ndefu nikielezea sababu za biashara kivipi.
 
Mnatuchanganya tu hata hatujui tumwamini nani
 
Anakabidhi hilo jiwe kwani ni ofisi ya serikali? Sema anawauzia serikali lakini kwa kiki.
Kwani wewe ulitaka liuzweje ili isiwe kiki mkuu?
Alafu vipi zile habari za kupigwa kwenye bei ya hayo madini sijasikia likizungumzwa kwenye hili jiwe au tumsubiri Lema atoe neno tuunge mkono hoja?
 
Back
Top Bottom