Mchina amenakili Range Rover Evoque na kuiita yake Land Wind

Mchina amenakili Range Rover Evoque na kuiita yake Land Wind

Lazima tuheshimiane tu mjini hapa na hii hali ya kufunga mkanda chini ya JPM.Waache wachina wafanye yao wote tuendeshe magari mazuri,alianza na Pikipiki wakati mjapani anauza bei kubwa Honda na Yamaha yeye akapindua sasa kaja na Luxury Cars.Kwenye Mabasi ndiyo usiseme Scania wanaisoma namba sasahivi.Shikamoo Mhe.Xi Jinping
Deng Xiaoping ndo shikamoo zaidi. Huyu bwana ndiye aliyeleta fikra mpya kwa wachina. Pamoja na nia njema ya Mao Zedong, fikra zake zilikua mgando. Deng kwa kuwa aliwahi kuishi Europe, akachukua falsafa za Ulaya akaziharmonize kuendana na sera zao za Kisoshalist. Hivyo akaruhusu uwekezaji, huyu ndiye aliyesababisha Wachina kutoka na kujifunza Technolojia nje ya China. Kwa kifupi huyu ndiye MZEE RUKSA wa TAIFA LA CHINA!
 
Prado-PARDO
SAMSUNG-SINGSUNG
Nokia-Nokla
Adidas-Adibas
Toyota-Tayota
Land cruiser-cruiserland
Yeezy - yeazy

ongezea

.............................
Ha ha ha ha. Mkuu mchina kwa fix hajambo. Ukiangalia kwa woga utafikiri majina ni sawa kumbe kapiga fix.
Philips-Philibs, Sony-SQny,
 
Ili mradi wewe uliyenunua uko comfortable inatosha mkuu. Huwezi kuwaridhisha walimwengu. Kuna watu hawataki hata kusikia gari za Toyota.
Hahaaa mkuu si kwa range kichina.

Ingekuwa gari nyingine ya kichina isiyo ya kukopi sawa.
 
Kati ya Scania, Benzi na Mabasi ya kichina, yapi yametawala barabara? Full luxury
Hiki ndicho nilicho maanisha.

Yutong, zong tong, howo-ni mchina katika identity yake.

Ila utakapo nunua yutong yenye logo na jina benz kwa 200ml ukataka ule sahani moja na benz ya mjerumani ya 800ml, utagundua unajikopesha furaha.
 
Nimeshakusoma mkuu, ndio maana nikakutolea mfano toka mwanzao, mchina aliona fursa kwenye simu. watu wengi walikua wanapenda BlackBerry ila uwezo hawana, wengine iphone akaona aje na simu za kiwango cha chini kabisa zenye muonekano kama wa BlackBerry na iPhone tena zina laini mbili na zingine hadi TV kwa bei ya kutupa, zilinunuliwa sana kwa sababu kuna daraja la watu wanazimezea mate hizo simu bora ila uwezo hauruhusu, hapo ndio walipata pakutokea.

Hali kadhalika haya mabasi aliyoyaleta, yanamuonekano mzuri baadhi yao yanazidi hata Scania (Andare, Marcopollo na Torino) achilia mbali uimara, lakini watu wameyakimbilia kwa matokeo ya muda mfupi. Hii ni kutokana na bei yake kuwa ya chini.

Tukija kwenye hili la Vogue, tunajua fika wachache wanaoweza kumudu hizo bei, licha ya kuzipigia chepuo sana...
Mchina ameiona hiyo fursa, wengi watazinunua tu. Watu hawtajali kama ni ya kichina, alimradi ina fleva kama ya Vogue shida zingine weka kule. Yeye hii yake anaiita Land Wind, utamshtakia wapi?

Nimependa hiyo kauli ya kujikopesha furaha!!!!
 
Lazima tuheshimiane tu mjini hapa na hii hali ya kufunga mkanda chini ya JPM.Waache wachina wafanye yao wote tuendeshe magari mazuri,alianza na Pikipiki wakati mjapani anauza bei kubwa Honda na Yamaha yeye akapindua sasa kaja na Luxury Cars.Kwenye Mabasi ndiyo usiseme Scania wanaisoma namba sasahivi.Shikamoo Mhe.Xi Jinping
Nakushauri umuache SCANIA aitwe SCANIA! Never bet against it!
 
watu wanapenda boxer ila bei ghal had vifaa lkn kuna kinglion 150 yan boxer ilivy na yenyew iko hvy hvy daa
 
Mkorinto. That's purely jealous. What special you have done since you're born? Either you like or not. Hawa wenzetu ni tishio. Maisha si kula na kulala tu mjomba make sure you do something constructive to keep your history long.
 
Back
Top Bottom