Hiki ndicho nilicho maanisha.
Yutong, zong tong, howo-ni mchina katika identity yake.
Ila utakapo nunua yutong yenye logo na jina benz kwa 200ml ukataka ule sahani moja na benz ya mjerumani ya 800ml, utagundua unajikopesha furaha.
Nimeshakusoma mkuu, ndio maana nikakutolea mfano toka mwanzao, mchina aliona fursa kwenye simu. watu wengi walikua wanapenda BlackBerry ila uwezo hawana, wengine iphone akaona aje na simu za kiwango cha chini kabisa zenye muonekano kama wa BlackBerry na iPhone tena zina laini mbili na zingine hadi TV kwa bei ya kutupa, zilinunuliwa sana kwa sababu kuna daraja la watu wanazimezea mate hizo simu bora ila uwezo hauruhusu, hapo ndio walipata pakutokea.
Hali kadhalika haya mabasi aliyoyaleta, yanamuonekano mzuri baadhi yao yanazidi hata Scania (Andare, Marcopollo na Torino) achilia mbali uimara, lakini watu wameyakimbilia kwa matokeo ya muda mfupi. Hii ni kutokana na bei yake kuwa ya chini.
Tukija kwenye hili la Vogue, tunajua fika wachache wanaoweza kumudu hizo bei, licha ya kuzipigia chepuo sana...
Mchina ameiona hiyo fursa, wengi watazinunua tu. Watu hawtajali kama ni ya kichina, alimradi ina fleva kama ya Vogue shida zingine weka kule. Yeye hii yake anaiita Land Wind, utamshtakia wapi?
Nimependa hiyo kauli ya kujikopesha furaha!!!!