Mchina kazubaa wapi kwanini hatengenezi magari ya umeme?

Mimi natamani watengeneze gari ya umeme ya kawaida tuu, isiwe high tech kiasi hicho. Iwe tu gari ambayo inaweza kumtoa mtu point A kwenda point B na iwe na zile standard features za kawaida kwenye gari kama AC, mziki nk hiyo inatosha sanaa. Ila iuzwe kwa bei rafiki
 
Yapo mengi sana Tatizo watu wanahofia quality na ndio competitor mkubwa wa TESLA.
 
Kwann kama taifa tusinifunze kuzalisha aina mbadala wa mafuta ya kuendeshea gari pasipo kutegemea Muarabu hali malighafi tunazo tele zinaoza tu
 
Yes hayo ni Maoni yako.

Lakini wao soko lao halikulengi wewe mwenye pesa kidogo... ukitaka gari la hivyo nenda kwa Masoud Kipanya, anatengeneza gari za hivyo. Muunge mtanzania mwenzetu.
 
Kwann kama taifa tusinifunze kuzalisha aina mbadala wa mafuta ya kuendeshea gari pasipo kutegemea Muarabu hali malighafi tunazo tele zinaoza tu
Kuna dogo anaitwa Samson, juzi kati alikuwa anahojiwa na Power Breakfast ya clouds FM, dogo anaweza kutengeneza petrol, dizeli, kerosini na Jet fuel kwa kutumia taka taka za plastiki. Lakini alienda kuomba mkopo wa zile milioni 50 za fungu la vijana, akaambiwa na afisa moja kwenye ofisi moja ya serikali hapo Dodoma kubwa Ubunifu wako unakupotezea muda, bora ufanye kilimo hatuwezi kukupa pesa. Video hipo YouTube, dogo anaonesha hatua mpaka petrol inapatikana kwa kutumia vifaa vya kuunga unga vya kuokota.
 
Kuna vitu vinatia kinyaa sana πŸ˜•
 
Kama tumeshindwa kutengeneza toothpick na njiti za viberiti tutaweza kutengeneza mafuta?πŸ˜†
Acha dharau kijana... Wabunifu ni wengi sana shida serikali yetu ndio inakwamisha, wazee wamekaa maofisini ukiwapelekea idea, wana kwambia haiwezekani... Nenda YouTube katafute kipindi cha power breakfast cha clouds FM juzi kati walimuhoji dogo anayeitwa Samson anatengeneza petrol kwa kutumia takataka za plastiki, na alivyoenda serikalini kuomba mkopo wa vijana wa milioni 50 wakamwambia nenda kalime, achana na hii. Masoud Kipanya naona ndio ameamua kumshika dogo mkono
 
Aisee inaelekea hufuatilii mambo. Mchina sasa hivi ndiye anayeongoza kuuza magari ya umeme. Unaifahamu kampuni inaitwa BYD? Sasa hivi inaonekana ni tishio kubwa kwa Tesla maana imeuza magari mengi Ulaya.
 
Umelala.

Nani anaetengeneza magari ya umeme kwa wingi zaidi ya China duniani?

Si unaagiza tu kwa mtandao.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
weka gesi mdau
 
Aisee inaelekea hufuatilii mambo. Mchina sasa hivi ndiye anayeongoza kuuza magari ya umeme. Unaifahamu kampuni inaitwa BYD? Sasa hivi inaonekana ni tishio kubwa kwa Tesla maana imeuza magari mengi Ulaya.
Vipi bei zao no rafiki?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…