Mchina kwa wizi kashindikana katoa F 35 ya US kama ilivyo kwa jina la J 35

Wizi kawaida si ndio maana hata US alikuwa anawinda ndege za russia hadi kuzibeba zikianguka. Hakuishia hapo submarine ya russia iliyozama akaandaa mission kuwa anafanya ocean exploration kumbe anataka kuibeba kutoka chini
 
Ishi sio ku copy ni kuiba Tech ulizoumiza kichwa wewe yeye anapita nayo
Concepts na capabilities wamekuwa wakitoa test beds na prototypes kwa ajili ya hiyo ndege na lengo hasa ni watoe variant ya kutua kwenye aircraft carriers zao. Carriers zenyewe wanazo na bado wanaunda leo uje kudai wamekopi uko ni kutukana dedication ya engineers wa Kichina.

Watu wamewekeza mabilioni ya dola, wana wanasayansi maelfu, wana facilities za kutosha, wana vyuo vinafanya research hawalali, wana aerospace departments na kampuni kama Shenyang na Chengdu wote hao unaona hamna kitu bali wameiba.

Ina maana Waturuki wana akili na resources kuliko Wachina?
 
Sioni cha ajabu hapo maana kuna ndege nyingi zenye mfanano na hiyo J 35. Kuna Su- 57 ya urusi, KF-21 ya Korea kusini.

Ila tukiongelea quality hiyo F-35 ya China ni bora kuliko hiyo ya Marekani kwa wazee wa military aviation mtanielewa
 
Bora ata hao wanaweza copy and paste. Sie wabongo hiyo ya copy and paste inatushinda tulivyokuwa maboya
 
Hizi F-35 zimeua kabisa soko la Rafale ya France huko Ulaya magharibi , wateja wa Rafale kwa Sasa ni India, Ugiriki,Serbia na baadhi ya nchi za kiarabu.


Nchi za ulaya(Germany, France Spain) walijipanga Sana kuunda 6th gen fighters zao ila sidhani kama Uncle Sam ataruhusu hilo kirahisi bila kuwawekea vizingiti.

 
Ndio ujinga wa Marekani anafigisu sana kwenye biashara hata Abram battle tank zake alivyokuwa anasua sua kuzipeleka Ukraine kwa kuhofia soko lake wakati huo HIMARS anailinda vibaya isiingie mikononi mwake Russia ikiharibika inapanda ndege karakana US.
 
Mpaka sasa Rafale ni successful jet maana Dassault hawakuiunda wakiwa na mategemeo sana na foreign operators. Rafale ilizaliwa kutokana na ubishi wa Eurofighter Typhoon ambapo wengine wote kwenye consortium hawakuwa na mpango na ndege inayotua kwenye aircraft carrier ila France ilisisitiza. Na kupishana kwingine ikabidi France ijitoe iwaache Spain, UK, Italy na Germany.

Kinachoifanya Rafale isiuze sana ni bei yake, Ufaransa ilikuwa peke yake hivyo production cost per unit ni kubwa. Ila kinachoifanya Rafale iuze ni kwamba haina usumbufu mwingi wa kidiplomasia hapo unaongea na Ufaransa tu akikubali unapewa ndege. Uzuri inajitosheleza kwenye weapon systems kama MICA missiles.

Kwahiyo sikubali kwamba F-35 inaua soko la Rafale sababu hazina role moja wala sio class moja. Na wala Marekani hana uwezo wa kuzuia consortium ya Ulaya kuunda 6th gen. aicraft.
 
Mchina anatengeneza hadi Iphone ila kwa jina lingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…