Mchumba kakataliwa kisa shepu

Mchumba kakataliwa kisa shepu

mpe lita 5 za mafuta anywe kila siku, atanenepa
 
Hivi kweli maisha ya leo dada anakuchagulia mke kweli ,dunia hii ni pana sana kwanza sikutegemea mada kama hii ulete hapa kuomba ushauli kwa mwanaume aliyeiva hili ni dogo sana wala lisingempa shida hata kidogo yeye angebaki na mchamba wake halafu wadada zake wakachukua hamsini zao,kwani wao waume zao uliwachagulia acha kabisa upoyoyo oa mke uliyempenda wala siyo anayependwa na dada zako ebo!
 
mambo mengine ni ya aibu tuu kwahiyo dada zako ndo wanakuchagulia mke wakati unampeleka kumtambulisha hulikuwa hujamwangilia shepu au ulimchukua ucku uzuri wa mwanamke siyo shepu ni bali ni tabia shepu hata mbuzi anayo bhana
Mkuu sio vizuri kuvunjana mbavu bhana....nimecheka sana aiseeee
 
....Labda dada nao wanataka kumchangamkia wifi yao, hivyo lazima awe na shape ya uhakika shurti #Figurenumber8 #Takolauhakika na #mguuulioshiba, vinginevyo hakuna ndoa.



Wanaoa dada zako au unaoa wewe?
 
Last edited by a moderator:
Mke wangu mm lkn wamkatae wao haya majanga sasa! DEMBA nakuomba chemba tafadhali
 
Last edited by a moderator:
Kwani dada zako ndo wanamuoa huyo binti??? Na je kigezo cha mwanamke ni shepu,hao dada zako wana shepu????? Aiseee hakianani.mi nkimwona mwanaume anayumbishwa,hana nsimamo,anamuliwa na ndugu nakasirika mpaka basi aagrrrrrr
 
mimi nikajua ni wazazi wamemkataa kumbe ni dada???
 
Kwani dada zako ndo wanamuoa huyo dada au wewe?Halafu wanaume wa hivi nawachukia nyieeee!!!Yaani mnaendekeza kusikiliza maneno maneno ya ndugu yasiyo na kichwa wala miguu!!!Ningewaona wana point endapo mmoja angesema anamfahamu mchumba wako ni changudoa mzoefu lakini eti mwembamba??Afu na wewe mwanaume mzima unakuja kuleta hii mada tukusaidie ushauri kweli??We akili za kufikiri huna? Basi mtafute Asha boko umuoe uwaridhiishe dada zako!! Nya........

Hunishindi mimi,wanaume wa namna hiyo huwa nawaita zuzu,hana maamuzi,jambo dogo hadi akawasimulie marafiki,ndugu,mchungaji,waumini,wazee wa kanisa,tena ukiwa na mwanaume wa namna hiyo utazeeka kabla ya umri,so jui mijinaume minginw okoje,they can't stand for their positions,mi.mwanaume wa hivyo hata simtaki
 
sio suala la kupotezeana muda mkuu...nipe mbinu za kuwashawishi dada zangu ili tufikie muafaka bila kununiana aisee!!

Swala sio kuwashawishi,just be a man of principles,toa maamuzi,anaekubali na akubali,Asiekubali atajiju
 
Wao hawajaolewa bado ila wanafanya kazi mmoja ni lecturer chuo kimoja kikubwa mwingine ni senior tax officer TRA!!

Wasomi halafu ovyoooo,ndo maana hawajaolewa,mbona sababu zao za kumkataa huyo binti ni very poor hata mtoto wa chekechea hawezi kuzitoa,duuh mawazo yao ni ya miaka ya 47 aisee
 
Back
Top Bottom