Mchumba kakataliwa kisa shepu

Mchumba kakataliwa kisa shepu

Unapotaka kuoa suala la ndugu lina uzito wake ya nini kuoa au kuolewa wakati hukubaliki na ndugu? Ukipata tatizo ndugu watakutenga na kejeli juu kwamba tulimwambia hakusikia! Ndo maana mchumba anatambulishwa ili ndugu jamaa na marafiki watoe comments kama ndugu wana walakini na mke mtarajiwa ni bora ukaachana nae!

Ni kweli, ila wawe na sababu yenye mashiko, sio shape. Kama huyu mwenzetu amefikia hatua ya kumpeleka kwa ajili ya kumtambulisha, maana yake kaipenda hiyo shape. Wangetoa kasoro za tabia kuhusu huyo dada labda ningesema kweli anatakiwa awape na ndugu zake nafasi katika kuchagua atakayekuja ishi naye. Hapo kwangu awapuuze tu.
 
wazazi wetu wengi walipangiwa ndio maana ndoa zao zimedumu mpaka sasa!!

Tunaendana na nyakati, mambo yamebadilika. Iwapo wazazi wataafiki, basi ni jambo jema zaidi, ila pia wasipo afiki, mwanaume mwenyewe atumie busara zake mwenyewe, maana yeye ndiye wa kuishi na huyo mwanamke! Na ni wazazi hasa wa kushirikishwa, sio madada. Madada zetu wengi hawajagi na sababu za msingi za kumkataa wifi yao mtarajiwa. Watasema, oh! sijui mweupe, sijui kabila fulani hatumtaki, oh! mwembamba nk.
 
Mwanamke screen saver shape hata kwa wachina zipo ... by bi Khadja Kopa
 
Mkuu we ndo mwamuzi waambie we ndo umemchagua huyo slander wako.Ila bonge lina raha yake bwana ukifika home unajua kabisa huyu ndiyo Mother house,hao vimbaumbau unaweza uliza eti mama mwenye nyumba nimekuta kumbe ndiye yeye unaemuuliza,au house girl unaweza jua ndo Mother house alafu mother house ndo house girl,kwa hiyo wanawake wenye miili mikubwa ni heshima ya nyumba.Dada zako wanalijua sana ilo,kwa hiyo za kuambiwa changanya na zako.Kama umempenda huyo mwambie aongeze msosi kidogo maana hakuna mwembamba.
 
Jamani wana Jamiiforums wenzangu nimebaki njia panda. Nilienda kumtambulisha mchumba wangu kwa wifi zake (dada zangu) juzi jumatatu huko kwetu sinza mida ya jioni baada ya kutoka kazini kwa kuwa tunafanya kazi ofisi za karibu pale posta.

Ila walichonijibu ni kuwa nitafute mwingine kwa kuwa huyu hana shape hawajampenda. Huyu mchumba angu yeye ni slander (mwembamba). Jamani naombeni ushauri wenu nifanyeje sasa nimebaki njia panda.

hilo neno ni kwa lugha gani mkuu?
 
Shepu kitu gani mjomba. Mashine inalipa? kama inalipa basi hilo ndo la muhimu
 
Yani mm mtoto mwembamba acha tu, nawapenda sana. Kwa kuwa wewe ndio unamuoa na wewe ndio umempenda wasijupe presha, kama mmekubaliana hao wifi zake hawana ishu
 
Yani mm mtoto mwembamba acha tu, nawapenda sana. Kwa kuwa wewe ndio unamuoa na wewe ndio umempenda wasijupe presha, kama mmekubaliana hao wifi zake hawana ishu

wembamba are easy to carry and roam with through the room!!!!
 
Kwa hiyo wewe ndugu zako ndio wanakufanyia maamuzi

napata wasi hiyo ndoa yako itakuwa inaendeswa kwa remote na wifi yetu atapata kazi ya ziada

Pole zake
 
Una miaka mingapi? Jee wazazi hawako hai? Naheshimu maamuzii y dada zako Lakini kumbuka raha shida na matamu ya huyo mdada unayajua wewe na hii ni furaha yako wewe na maisha yako, wao uliwachagulia wanaume wakuwaoa au waku date nao? Kama mwanamme kua na maamuzii ya kiume ulikwenda kuwaonyesha hukutaka rai zao Kama anafaa au laa... Na ukiwapa nafasi hii basi watalupangia zamu mpaka ya kulala na mkeo... Take care.....


"The truth is hard to swallow when you're choking on your pride."
 
Na ww wakileta mashemej wakatae ili iwe ngoma droo
 
Back
Top Bottom