Well said Brother. Ukuu wa Mungu hauna maswali. Unyenyekevu wetu ni muhimu sana. Katika masual ya elimu ya Mungu, nimejifunza kuwa kuna vitu viwili vinachangia watu kufa kabla ya wakati, vitu hivyo ni upumbavu na uovu. Ili ukae sawa na Mungu yakupasa kuacha uovu/kutubu pamoja na kuacha upumbavu.
Bible inatufundisha kuwa kama vile uovu unavyoweza kuchangia mtu kufa kabla ya wakati upumbavu pia huchangia. Epuka uovu, pia epuka upumbavu
17 Usiwe mwovu kupita kiasi; Wala usiwe mpumbavu; Kwani ufe kabla ya wakati wako?
Mhubiri 7:17
Hekima ni ulinzi nayo humhifadhi aliyenayo.
11 Hekima ni njema, mfano wa urithi; Naam, nayo ni bora kwao walionao jua.
Mhubiri 7:11
12 Kwa maana hekima ni ulinzi, kama vile fedha ilivyo ulinzi; na ubora wa maarifa ni ya kwamba hekima humhifadhi yeye aliye nayo.
Mhubiri 7:12
3 Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha; Bali wajinga huendelea mbele wakaumia.
Mithali 22:3
Epuka kuwa na imani inayoambatana na upumbavu.