Mchungaji Anthony Lusekelo, aionya Serikali ya Rais Samia juu ya amani ya Tanzania

Katika hali ya kushangaza, siku zote mzee wa Upako huwa upande wa serikali.
Lakini leo ameamua kuvunja ukimya na kuinyoshea serikali kidole tena kwa ukali kuwa ijihadhari isije kuharibu amani ya Tanzania.

Wakati akitoa angalizo hilo, amewataja kwa majina akianza na Kassim Majaliwa waziri mkuu, Rais Samia na Mpango.

Amewakumbusha kuwa sio vyama vya upinzani pekee huleta machafuko bali hata Serikali huwa ni chanzo cha machafuko.

Ameonya kuwa uonevu ukizidi hata askari taratibu huungana na raia kinyume cha watawala kwani hata wanao onewa ni jamaa zao na maaskari.

Zaidi ameionya serikali kujiepusha na kuingilia mambo ya kidini kwani hata wakizifuta imani za dini ziko mioyoni mwa watu na sio kwenye usajili wa kiserikali.

Amekumbusha kuwa miaka ya 80 serikali ilijaribu kufuta usajili wa makanisa hata kuwafunga wengine lakini ilishindwa na tena wakristo waliungana.

Amesema watu wa imani moja huungana wakati wa kuonewa hivyo wajihadhari na jambo hilo.

Amesema kwasasa serikali ina matatizo makubwa kisiasa, corona nk kwa hiyo isiongezee mzigo wa kidini haitabaki salama.
Zaidi msikilize hapo chini kwenye link.

View attachment 1897536
Yes, nakubaliana na wewe Mch. Lusekelo...

Hawa watawala walevi wa madaraka sasa wameanza kuingia mahali pasipo...

Wameanza kuingia mpaka ndani ya makanisa na misikitini eti kwa kisingizio cha kudhibiti watu...

They are unknowingly designing their own burial ceremony....!!
 
Katika hali ya kushangaza, siku zote mzee wa Upako huwa upande wa serikali.
Lakini leo ameamua kuvunja ukimya na kuinyoshea serikali kidole tena kwa ukali kuwa ijihadhari isije kuharibu amani ya Tanzania.

Wakati akitoa angalizo hilo, amewataja kwa majina akianza na Kassim Majaliwa waziri mkuu, Rais Samia na Mpango.

Amewakumbusha kuwa sio vyama vya upinzani pekee huleta machafuko bali hata Serikali huwa ni chanzo cha machafuko.

Ameonya kuwa uonevu ukizidi hata askari taratibu huungana na raia kinyume cha watawala kwani hata wanao onewa ni jamaa zao na maaskari.

Zaidi ameionya serikali kujiepusha na kuingilia mambo ya kidini kwani hata wakizifuta imani za dini ziko mioyoni mwa watu na sio kwenye usajili wa kiserikali.

Amekumbusha kuwa miaka ya 80 serikali ilijaribu kufuta usajili wa makanisa hata kuwafunga wengine lakini ilishindwa na tena wakristo waliungana.

Amesema watu wa imani moja huungana wakati wa kuonewa hivyo wajihadhari na jambo hilo.

Amesema kwasasa serikali ina matatizo makubwa kisiasa, corona nk kwa hiyo isiongezee mzigo wa kidini haitabaki salama.
Zaidi msikilize hapo chini kwenye link.

View attachment 1897536
Huyu Mtumishi wa Mungu huwa ana hekima sana. Hapa amesema point moja ya msingi sana kwamba

"....akitokea kiongozi mmoja wa dini huko anafanya chokochoko, mumushughulikie yeye, tena ni rahisi tu kumzunguka, kwa kutumia viongozi wenzake wale wale wa dini!
 
Huyu Mtumishi wa Mungu huwa ana hekima sana. Hapa amesema point moja ya msingi sana kwamba

"....akitokea kiongozi mmoja wa dini huko anafanya chokochoko, mumushgulikie yeye, tena ni rahisi tu kumzunguka, kwa kutumia viongozi wenzake wale wale wa dini!
Kuna vitu vingi muhimu aneongea mkuu
 
Lusekelo nadhani ni mjumbe wa kamati ya Amani inayo ongozwa na sheki wa mkoa wa DSM, sasa kwa nini anaanza kulopoka wakati wana chombo chao ambacho kingejadili jambo hilo na pia kuishauri mamlaka?
inaonekana Lusekelo ana jambo lake analo lijua zaidi yeye.
huu ni unafiki na uzandiki ulio pindukia.

Waziri Simbachaweni anapaswa akemee vikali matamshi kama haya yanayo tolewa na viongozi wa dini maana hayana lengo zuri hata kidogo.
kiongozi kama huyo anapo tamka maneno bila kutafakari kwa kuwa yeye kashiba nyama choma ni hatari sana.
Upumbavu wako utakuisha lini? Lusekelo ana haki yake binafsi ya kutoa maoni na siyo lazima apitishe maoni yake katika kikundi cho chote!
 
Wanaoshangaza zaidi wapinzani, hasa CDM, kwa ukinyonga wao ambapo sasa wanamshabikia mtu kama Lusekelo! Miaka mitano ya JPM wamefanyiwa ukatili mkubwa mno, hawa wahuni hawajawahi kukemea, walikuwa busy kupokea hongo ndogo ndogo!! Leo hii Serikali mpya imesema itakuwa inahakiki haya makanisa uchwara kila baada ya miaka 5, hawa wahuni wanajifanya kuanza kuikosoa Serikali, eti CDM nao washahamia upande wa hawa watu na kuwaunga mkono!! CDM kwa tabia hizi hakuna mtu atawachukulia serious, lazima muwe na msimamo na mjifunze kupiga mstari, siyo kila siku mnaendeshwa na matukio tu
Fahamu kuwa hapo hoja inaungwa mkono na siyo mtu! Watu wanasema hata saa mbovu huwa sahihi angalau mara moja ndani ya saa 24.
 
Hadi mzee wa upako ameonya kweli hali ni tete. Huenda nchi yetu ikawa kama sudani sasa.
Iko hivi, Mzee wa Upako anaweza kuwa ni mmojawapo kati ya viongozi watano (5) wa kiroho wanaoongoza kwa kuwa na hekima na nia njema sana, nchini kwetu. Huyu mtu mimi siku zote huwa ninamkubali sana
 
Naye aambiwe aache kuwaonea na kuwanyonya ndondocha.
Anzisha uzi wako sasa hapa tunajadili alichokisema ni kweli au uongo? Nakukumbusha tuu kwamba kuanzia kesho ukinunua umeme wa buku 5 hapo ulipo hata kama ni kibanda cha kuchajia simu na kuuza pipi unakatwa buku ya kodi ya pango... mama ameupiga mwingi weeee sasa anabutua na kupiga minazi [emoji12][emoji12]
 
Hawa wezi wa sadaka waliojipachika majina ya viongozi wa dini wanajifanya wao hawagusiki.
 
Mzee Antony Lusekelo anapaswa akemewe kwa matamko yake ambayo kimsingi yana lengo la kuchochea uvurugaji wa amani ya nchi.
Leo ktamka yeye hatujui ni kwa masilahi ya nani!
kesho akitamka Padri kesho kutwa akitamka Sheki, n.k watawavuruga Watanzania na matokeo yake sisi sote tutazama.
Inapo fikia suala la mtu kuchezea Amani ya Nchi yetu kamwe tusioneane aibu wala tusimchekee mtu lazima akemewe Vikali, lazima atambue kuwa Yeye LUSEKELO hayupo juu ya MANI YA NCHI YETU.
Kamwe asijaribu kuleta uchochezi halafu anawapaka mafuta kwa mgongo wa chupa.
Amani ya nchi yetu ina thamani zaidi kuliko yeye.
Aache mara moja kauli za kufitinisha watanzania na Serikali yao, aache mara moja kutoa kauli za mifarakano, aache mara moja kauli zisizo na tija kwa taifa.
nashauri tena huyu mchungaji akemewe vikali na waziri wa Mambo ya ndani lkn pia Akemewe vikali na Kamati ya Amani.
 
Hawa wahuni wanaojiita viongozi wa dini JPM aliwadekeza sana, huyu alimjengea hadi barabara ya lami waumini wake wapite, kila mara alikuwa anawaalika ikulu na kuwapa upendeleo wa juu, na hiyo yote ni kutokana na uoga wake na kutojiamini, akipenda kusifiwa na kila mtu!! Wale wa upande mwingine ilikuwa ni kuwalisha ubwabwa na kuwahonga misikiti, miezi hii mitano wamepotezewa tayari wameanza mayowe! Ni wengi wataibuka, vikiwemo vyombo vya habari kama Clouds ambavyo vimekuwa yatima kwa sasa ambavyo mbeleko walilolitegemea lipo Chato milele. Kila utawala na namna yake ya kutawala. Itatuchukua siyo chini ya miaka 3 sumu na propaganda alizosambaza JPM nchi kuisha
Wewe eume neemeka kipindi kipi maana kila mtu na wakati wake, najua na wewe nafasi hiyo unayao au uliwahi kuipata
 
Mzee Antony Lusekelo anapaswa akemewe kwa matamko yake ambayo kimsingi yana lengo la kuchochea uvurugaji wa amani ya nchi.
Leo ktamka yeye hatujui ni kwa masilahi ya nani!
kesho akitamka Padri kesho kutwa akitamka Sheki, n.k watawavuruga Watanzania na matokeo yake sisi sote tutazama.
Inapo fikia suala la mtu kuchezea Amani ya Nchi yetu kamwe tusioneane aibu wala tusimchekee mtu lazima akemewe Vikali, lazima atambue kuwa Yeye LUSEKELO hayupo juu ya MANI YA NCHI YETU.
Kamwe asijaribu kuleta uchochezi halafu anawapaka mafuta kwa mgongo wa chupa.
Amani ya nchi yetu ina thamani zaidi kuliko yeye.
Aache mara moja kauli za kufitinisha watanzania na Serikali yao, aache mara moja kutoa kauli za mifarakano, aache mara moja kauli zisizo na tija kwa taifa.
nashauri tena huyu mchungaji akemewe vikali na waziri wa Mambo ya ndani lkn pia Akemewe vikali na Kamati ya Amani.
 
Mzee Antony Lusekelo anapaswa akemewe kwa matamko yake ambayo kimsingi yana lengo la kuchochea uvurugaji wa amani ya nchi.
Leo ktamka yeye hatujui ni kwa masilahi ya nani!
kesho akitamka Padri kesho kutwa akitamka Sheki, n.k watawavuruga Watanzania na matokeo yake sisi sote tutazama.
Inapo fikia suala la mtu kuchezea Amani ya Nchi yetu kamwe tusioneane aibu wala tusimchekee mtu lazima akemewe Vikali, lazima atambue kuwa Yeye LUSEKELO hayupo juu ya MANI YA NCHI YETU.
Kamwe asijaribu kuleta uchochezi halafu anawapaka mafuta kwa mgongo wa chupa.
Amani ya nchi yetu ina thamani zaidi kuliko yeye.
Aache mara moja kauli za kufitinisha watanzania na Serikali yao, aache mara moja kutoa kauli za mifarakano, aache mara moja kauli zisizo na tija kwa taifa.
nashauri tena huyu mchungaji akemewe vikali na waziri wa Mambo ya ndani lkn pia Akemewe vikali na Kamati ya Amani.
Hivi una akili kweli?
Mtu anatahadharisha unataka akemewe?
Ccm nyie ni wagonjwa sana
 
Tutayaachia makanisa tu ambayo maaskofu wake wana degree za theology - hawa wengine wanawayumbisha wananchi.

Hii ndiyo hofu aliyonayo kamanda.
 
Back
Top Bottom