Opportunity Cost
JF-Expert Member
- Dec 10, 2020
- 9,034
- 6,913
Katika hali ya kushangaza, siku zote mzee wa Upako huwa upandevwa serikali.
Lakini leo ameamua kuvunja ukimya na kuinyoshea serikali kidole tena kwa ukali kuwa ijihahadhari isijekuharibu amani ya Tanzania.
Wakati akitoa angalizo hilo, amewataja kwa majina akianza na Kasim Majaliwa waziri mkuu, Rais Samia na Mpango.
Amewakumbusha kuwa sio vyama vya upinzani pekee huleta machafuko bali hata serkali huwa ni chanzo cha machafuko.
Ameonya kuwa uonevu ukizidi hata askari taratibu huungana na raia kinyume cha watawala kwani hata wanao onewa ni jamaa zao na maaskari.
Zaidi ameionya serikali kujiepusha na kuingilia mambo ya kidini kwani hata wakizifuta imani za dini ziko mioyoni mwa watu na sio kwenye usajili wa kiserikali.
Amekumbusha kuwa miakq ya 80 serikali ilijaribu kufuta usajili wa makanisa hata kuwafunga wengine lakini ilishindwa na tena wakristo waliungana.
Amesema watu wa imani moja huungana wakati wa kuonewa hivyo wajihadhari na jambo hilo.
Amesema kwasasa serikali ina matatizo makubwa kisiasa, corona nk kwa hiyo isiongezee mzigo wa kidini haitabaki salama.
Zaidi msikilize hapo chini kwenye link.
Kwanza naomba nieleze wazi kwamba utawala huu ni laini Sana ndio maana unachezewa ,hakuna anaeuonea.
Na hizi chokochoko mara nyingi hutokea kipindi cha viongozi wakiwa Waislamu wakristo na Waislamu huanza mivutano.
Nilichojifunza hii hutokana na upole wa viongozi wa kiislamu,Magu aliwanyoosha Sana kuanzia wakubwa wa makanisa hadi akina gwajiboy walipekuliwa hatukusikia kelele za watu wa imani kuungana au sijui eti kuonewa,hakuna utawala ulikuwa kandamizi kama wa Magu.
Mama stuka kuwa mkali Sana Hawa watakuchezea sharubu na usiwape airtime ya kuongea waufyate kama awamu iliyopita la sivyo watatoa kila matamko na kukupaka uchafu wote.
Bora uwe dikteta kuliko kuwapa watu uhuru wakautumia vibaya kwa propaganda za kijinga,na hii nchi imejaa wajinga huamini Sana propaganda.Magu alikuwa dikteta akawaaminisha watu propaganda wakawa upande wake huku anawaminya wanaonyanyua mdomo.
Ukiniuliza huyo uonevu gani hasa hana majibu,akikwambia Mbowe sijui gwajima ila atajifanya haelewi kwamba gwajiboy alipekuliwa uchi kwake,Akina Mbowe na wengine walikula mapanga,risasi na watu kupotea nk na hakuna alikuwa ananyanyua mdomo juu.Sasa Maza wachekee tuu na uwe unakaa kimya unaogopa kutoka hadharani kuongea kwa ukali na kwa vitendo.
Sasa hivi mzigo wa chanjo kaachiwa Waziri nyie kimyaa,subiri wakuoneshe shoo.