Mchungaji Anthony Lusekelo, aionya Serikali ya Rais Samia juu ya amani ya Tanzania

Kwanza naomba nieleze wazi kwamba utawala huu ni laini Sana ndio maana unachezewa ,hakuna anaeuonea.

Na hizi chokochoko mara nyingi hutokea kipindi cha viongozi wakiwa Waislamu wakristo na Waislamu huanza mivutano.

Nilichojifunza hii hutokana na upole wa viongozi wa kiislamu,Magu aliwanyoosha Sana kuanzia wakubwa wa makanisa hadi akina gwajiboy walipekuliwa hatukusikia kelele za watu wa imani kuungana au sijui eti kuonewa,hakuna utawala ulikuwa kandamizi kama wa Magu.

Mama stuka kuwa mkali Sana Hawa watakuchezea sharubu na usiwape airtime ya kuongea waufyate kama awamu iliyopita la sivyo watatoa kila matamko na kukupaka uchafu wote.

Bora uwe dikteta kuliko kuwapa watu uhuru wakautumia vibaya kwa propaganda za kijinga,na hii nchi imejaa wajinga huamini Sana propaganda.Magu alikuwa dikteta akawaaminisha watu propaganda wakawa upande wake huku anawaminya wanaonyanyua mdomo.

Ukiniuliza huyo uonevu gani hasa hana majibu,akikwambia Mbowe sijui gwajima ila atajifanya haelewi kwamba gwajiboy alipekuliwa uchi kwake,Akina Mbowe na wengine walikula mapanga,risasi na watu kupotea nk na hakuna alikuwa ananyanyua mdomo juu.Sasa Maza wachekee tuu na uwe unakaa kimya unaogopa kutoka hadharani kuongea kwa ukali na kwa vitendo.

Sasa hivi mzigo wa chanjo kaachiwa Waziri nyie kimyaa,subiri wakuoneshe shoo.
 
Jamaa ameongea point sana, wewe wachokoze wakristo hadi wachokozeke hakuna rangi utaacha kuona
Nasema hivi mara nyingi wakristo huwa Wana chuki na viongozi wa kiislamu,kila kiongozi akiwa Muislam lazima wazushe upuuzi na ndio hasa huja kuwachochea Waislamu ku retaliate.

Magu aliwanyoosha hao wakristo to the maximum lakini hakuna aliyenyanyua mdomo.Mimi sio Muislam ila nimeobserve kila Kiongozi akiwa Mkristo matamko sijui nyaraka na uzushi mwingine huanza.

Viongozi wa kiislamu kuweni wakali Hawa huwa ni wanafiki.
 
Tozo ni kodi kama kodi zingine lazima kulipa linahusika vipi na imani zao? Hakuna hoja hapo.
 
Mbona hata dhalimu magufuli Viongozi wa kikristo mbali mbali WALIMKOROMEA? Sioni udini hapa zaidi ya kutetea HAKI, UHURU na USAWA wa Watanzania wote bila kujali itikadi zetu.
 
Kama nilivyosema awali alifaulu kwa propaganda si unajua hii nchi ina wajinga wengi,kwa hiyo alikuwa anafanya uovu kuanzia kwenye imani zao,vyama hadi ugumu wa maisha mtaani.

Sijawahi sikia maisha nafuu kipindi chote ilikuwa ni vilio vya vyuma kukaza sasa hivi kwa vile kuna tozo basi imekuwa ndio kisingizio.Nchi lazima uende tena hiyo tozo ni fair Sana kulinganisha na uporaji na uonezi uliokuwa unafanywa kipindi kile ni vile ilikuwa marufuku kutoa taarifa kama zile zinazokinzana na Serikali.
 
Kuna mambo mengi tena ya msingi sana ya kushughulika nayo kwa masilahi na ya manufaa kwa taifa na kwa Mtanzania mmoja mmoja. Hayo viongozi wengi wanajifanya hawayaoni wanakwenda kukimbilia vitu ambavyo havina madhara yoyote kwa taifa na wananchi kwa ujumla tena yana manufaa kwa wananchi ndiyo wanakimbizana nayo kuyablock ili huyu mwananchi aendelee kuteseka katika nchi yake.

Swala la dini za watu na hata wale wasiokuwa na dini zimeathiri nini kwenye taifa hili mpaka viongozi waamue kutoa nyaraka za kubana dini zetu.Naomba viongozi wetu wafahamu kuwa sasa hivi kwa hali ilivyo Watanzania wengi wanakimbilia misikitini,makanisani,angalau wapate amani na faraja mioyoni mwao baada kelele za hali ngumu ya maisha kutokusikilizwa vilio vyao na viongozi wao.Ada za watoto shule,mafuta ya kula kupanda sana bei (kitu ambacho hakijawahi kutokea kwa nguvu kali hivi Tanzania),tozo za simu kwa madai ya barabara za vijijini,mafuta petroli,diesel nk.kupanda bei kila kukicha na sijui tutaishia wapi nk. wakijua huko kwenye dini zao angalau watafarijika bado wanafwato huko kuhakikisha pia huko hawati walichofuata huko.Mnatupeleka wapi viongozi wetu, kumbukeni kwenye katiba (Japo wengine wanataka mpya) kuna haki ya kila mtu kufuata kuabudu dini anayotaka ali mradi havunji sheria za nchi.Ninyi mliapa kuilinda kwa nguvu zenu zote. Leo mmeshasahau mnakwenda tena kinyume nayo.Kwa hali hii hakuna namna ambavyo Watanzania wataacha kudai katiba mpya.

Leo hii uhuru wa Mtanzania kuabudu umevurugwa makusudi ili kiongozi aliyepo madarakani aonekane hafai wanamhujumu kwa makusudi.Tangu lini jeshi la polisi linaingia kwenye nyumba za ibada wakati ibada inaendelea na kuwakamata waumini na kuchafua utaratibu wote wa ibada hii kwa mara ya kwanza nimeona Tanzania kwa miaka yangu karibu 70 niliyo nayo sasa.Nasema tena hii ni hujuma anafanyiwa Mkuu wa Nchi.

Ila jambo la kushangaza viongozi wetu wa dini hawakuona umuhimu wa kukemea na kukataa kwa nguvu na kwa umoja wao na wala hawakuona kuwa mkuu wa nchi anahujumiwa, wao wakakaa kimya wakidhani kuwa wameguswa Wakatoliki wao wako salama,kumbe sio, haya waraka umetoka,je hauwahusu,je wamekuwa salama?'Ahsante hata kwa kiongozi huyu angalau ameoneshwa kuwa tuendako kama hatutajirekebisha hatupo salama.Haki huinua taifa,bali dhambi ni aibu kwa taifa.

Pamoja na hayo yote magumu anayopitia Mtanzania huyu ambaye nchi yake ni Tajiri,ina uchumi wa kati mbona haya yote hayabadilishi maisha ya Mtanzania kuwa bora bali yanaendelea kuwa duni zaidi ya jana,ni laana gani tuliyonayo Watanzania.

Viongozi wa dini zote sisi waumini wenu tunawaamini, Waislamu na Wakristo tunawasikiliza tumewasikiliza msaidieni Mkuu wa Nchi anahujumiwa huyu sie yule aliyesema hataki dhuluma,anapenda haki itendeke.Mbona mambo hayaendi kama alivyosema?,mbona mambo yanakwenda kinyume? Hujma, hujma,haiwezekani swala la tozo ya mihamala ya simu isiwe imetafutiwa ufumbuzi mpaka sasa wakati mkuu wa nchi alitoa agizo kwa Waziri kuwa kilio cha Watanzania kimefika kwake swala hilo lishughulikiwe haraka iwezekanavyo. Inasikitisha mpaka leo hii sijui sasa ni mwezi wa 3 kimya.

Sina hakika inawezekana kwa sababu ya kumhujumu wanamwambia lilishashughulikiwa. Mbona mambo mengine ya kisiasa, kamatakamata ya wanasiasa inakwenda fasta,Gwajma fasta,petrol panda fasta,gesi panda fasta Sabaya mahakamani fasta na mengine mengi tu.

Jamani Watanzania sisi wote ni ndugu,hatuwezi kuongoza wote.
 
Mbona hata dhalimu magufuli Viongozi wa kikristo mbali mbali WALIMKOROMEA? Sioni udini hapa zaidi ya kutetea HAKI, UHURU na USAWA wa Watanzania wote bila kujali itikadi zetu.
Haki,uhuru na usawa upi? Viongozi gani waliomkoromea Magu? Wote walinywea na Kuishia kuandika kwenye mitandao.

Ningekuwa mimi ni Rais kwa nature ya watu wa nchi hii kuongea Sana ningechukua mkondo wa ukandamizaji ila kwenye uchuynisingefanya hivyo,kiufupi ningewaziba midomo vinginevyo mtayumbisha nchi Sana
 
Hawa wanaleta chokochoko na kuzusha taharuki,binafsi ningewaonya wakome mara moja .

Kuwa na imani yako hakukupi fursa ya kuvunja sheria
 
Wameshindwa kuficha chuki zao za kidini.

Uonevu wa awamu ya tano walikuwa wanaubariki tena huyu mzee wa bapa alikuwa mstari wa mbele!
Watu walipigwa, teswa, dhulumiwa, pimwa mikojo yote yalikuwa kwa "neema za bwana"!
 
Kunywea kwao kwa dhalimu magufuli haina maana waendelee kunywea huku wakiona udhalimu na dhuluma zinazidi kushamiri nchini. Nchi hii ilishayumba siku nyingi sana basi tu Watanzania ni wavumilivu.
 
Ivi enzi zile za zama za 5 mzee hakuona au kusikia uonevu kweli ? Asipotoshe watu pengine na yy anatafuta political millage
 
mtajiuliza kwanini JPM akiwa Rais hata afanye nini hawa walikuwa hawanyanyui mdomo?...kuna mambo magumu sana kwenye kuingoza hii nchi, tuwe makini sana..
 
Mimi naamini,kila eneo,kila dini ina kiongozi wake,na maadili yake.Kila mahali kuna utaratibu wake ndiyo maana kila mmoja anawajibika mahali au kwa kiongozi fulani.Kama jambo fulani kama la mavazi na anayehusika pale halijawa kero kwake na kwa wengine na kwa uvaaji ule haujavunja taratibu zilizowekwa pale,hazijavunja sheria ya nchi hakuna shida. Kumbuka kila mtanzania ana uhuru wa kuabudu popote,kuvaa anavyopenda,alimradi tu, haendi kinyume na taratibu za mahali husika,na havunji sheria za nchi.

Fahamu kuwa anayevunja sheria ni huyu anayeingia kwenye taratibu za wahusika bila ridhaa yao, bila kujitambulisha na kuzivunja kwa makusudi kwa sababu tu,yeye ana nguvu ya pesa au ana nguvu ya kumiliki silaha.(Kwa nchi yetu ya Tanzania huyu mwenye nguvu ya pesa na silaha ana haki hajavunja sheria ila kwa wenzetu walioendelea kavunja sheria kufuatana na katiba).

Nataka nikuambie na ukipenda uelewe, hawa waliovamia kanisani walipaswa kukamatwa na kufunguliwa mashtaka ni magaidi hawa, Wakina baba wanaingia kwenye nyumba za ibada na mavazi ya heshima ila mengine yameandikwa,motuary attendants,we sell dogs, hallotel, Mtu awaye yeyote asiudharau ujana wako,video shooter,ccm,act wazalendo, m4c,katiba mpya,je,hawa wote utawavamia na kuwakamata. Tuache ubaguzi,tena tujifunze kilichotokea Afrika ya kusini juzi tu. Tanzania sio Rwanda au Burundi,Nigeria,Afghanistan.nk.kila mtu ana haki ya kuishi Tanzani, kuabudu popote,kuvaa vyovyote, usisahau,ALI MRADI,ALI MRADI HAVUNJI SHERIA ZA MAHALI ALIPO NA ZA NCHI.Hapo yupo salama.
 
Amezungumza baada ya serikali kusema taasisi za kidini zitatakiwa kisajiliwa upya kila baada ya miaka 5
 
mtajiuliza kwanini JPM akiwa Rais hata afanye nini hawa walikuwa hawanyanyui mdomo?...kuna mambo magumu sana kwenye kuingoza hii nchi, tuwe makini sana..
JPM alikuwa mwehu nani alikuwa na ubavu wa kujibizana nae wakati taarifa zake za milembe zilikuwa wazi kabisa
 
Nchi inateketea huku wanaojiita wasomi wakishangilia kwa post za kizandiki acha mawe yaongee
 
wafuasi wa chama cha mataahira (ccm) wataishia kumbeza tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…