Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu

Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu

Kwenye hili nahisi pastor kimaro ataenda kujitafakari
Mimi ni muumini wa KKKT hapo kijitonyama, shida iliyokuwepo kwa mchungaji kimaro ni kwamba alikua anaenda kinyume na utaratibu wa kanisa na kibaya...
Huyo MASAI tena ni nani mbona sijawahi kumsikia mkuu? Lakini KKT nanyi mna mambo ya ajabu sana. Mnafanya ibada zenu kama Kanisa Katoliki.

Ibada hadi zinakuwa na ratiba ya mwaka mzima na hamtaki mtu ahubiri nje ya ratiba. Sasa mtu kama ana kipaji cha kwenda hadi nje ya ratiba hamuoni kwamba mnakuwa mnafunga kipaji chake?

Namshauri Kimaro afungue kanisa lake kama Mwingira apige pesa za kutosha. Unajua hata Mwingira alikuwa KKT lakini akafanyiwa mizengwe akaamua kauzisha kanisa lake mwenyewe.

Unaona sasa anavyopiga pesa ndefu?
 
Kufuatia semina iliyokuwa imeanza katika usharika wa KKKT KIJITONYAMA ikiongozwa na Rev Dr. Eliona Kimaro imelazimika kusimama kufuatia barua aliyopewa ya likizo ya siku 60 na kupelekea kushindwa kuendelea na semina hiyo...
Mchungaji Kimaro yupo sahihi 100%. Nawashangaa sana uongozi wa KKT unavyomuwekea mizengwe bila sababu za msingi. Bora tu afungue kanisa lake sisi tuhamie huko.
 
Achana na Hilo wazo mkuu Ni Bora umshauri awe na utiii tu na kufata misingi ya kanisa la kkkt ,na mambo ya mahubiri yake yako vzr

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
hata yesu alikuja kwaajili ya wenye kiu hapo ni wazi wameshashiba na kukinai let him move akaokoe nafsi zinazoangamia.
 
Ugomvi wa Mastai korogwe ni zaidi ya Ibada
Ni mambo ya sadaka
Asante kwa taarifa lakini mimi si muumini wa hapo, mambo ya Sadaka ni ngumu kujua, nilichogundua kwa haraka ni ibada kuwa tofauti kabisa na ibada za kilutheri nilizozoea.
 
Mchungaji Kimaro yupo sahihi 100%. Nawashangaa sana uongozi wa KKT unavyomuwekea mizengwe bila sababu za msingi. Bora tu afungue kanisa lake sisi tuhamie huko.
Hata kuandika KKKT huwezi ndugu yangu,wewe sio muumini wa kanisa hili...mchungaji wako yupo likizo,na wewe nenda nae likizo usisali.
 
wenye hili nahisi pastor kimaro ataenda kujitafakari
Mimi ni muumini wa KKKT hapo kijitonyama, shida iliyokuwepo kwa mchungaji kimaro ni kwamba alikua anaenda kinyume na utaratibu...
wazee wa kanisa uchwara naona mmeanza kuja!

tena nyie ndio waharibufu wakubwa wa KKKT!

Wangeondoa hiki cheo cha wazee wa kanisa kila kitu kingetulia!
 
Sina shida na mafundisho yake ila utii na kujikweza Ni mbaya Sana

Mara kadhaa namuona akaiwasifia RC Eti kkkt haiwezi kutoa kiti Cha urais wa nnchi hi yeye kimaro aliyasema mbele ya Dr mwigulu nchemba madelo..
Kaongea ukweli wake na wewe sema ukweli wako baas.
 
Kwenye hili nahisi pastor kimaro ataenda kujitafakari.

Mimi ni muumini wa KKKT hapo kijitonyama, shida iliyokuwepo kwa mchungaji kimaro ni kwamba alikua anaenda kinyume na utaratibu wa kanisa na kibaya zaidi alisha onywa zaidi ya mara 3 ila shida yake akiitwa akaonywa anakuja kanisani anaanza kuongea kwa waamini na kurusha vijembe kwa viongozi wake.

Tarehe 8 ukiweza fatilia alichokifanya kwa pastor mwenzake ANNA maneno aliyoongea kumuhusu huyo mchungaji kuna jambo utaelewa.

Kimaro ana kiburi cha umaarufu
Mchungaji hafati kalenda ya kanisa, yeye anafanya mambo yake, aliitwa akaonywa ila akaja kanisani hadharani na kusema hawezi kupangiwa cha kufanya ila Mungu tu, sasa hapo kweli kuna utii?

Kimaro toka amekuja usharikani anazo nyimbo 6 tu anazo imba kutoka kitabu cha tumwabudu Mungu wetu, aliitwa akaambiwa hiki kitu ila akawa mkaidi, ni mchungaji anayependa yeye aongee zaidi, hapendi kuwapa wachungaji wengine nafasi ya kuhubiri, ikitokea mchungaji mwingine akahubiri basi na yeye baada ya mahubiri atasimama na kuanza kujazilishia kuonekana kwamba mwenzake hajafanya kama inavyo paswa.

Ni kimaro na masai wa kimara ambao ukifatilia utaratibu wanao ufanya kanisani siyo wa kkkt ila najua wachache sana wataelewa hili.

Kama mtaweza kumbuka pia aliondolewa kwenye vipindi vya upendo Tv kisa mambo yake hayo ya kufanya kinyume na utaratibu wa kanisa ikabidi wamuonye ila akakaidi, baada ya kuondolewa alikuja kanisani hadharani na kuanza kusimanga na kuongea mbovu na tokea hapo hajawahi kutangaza kitu chochote kinacho husu upendo kama magazeti.

Alitamba sana kwamba kwa jinsi alivyo barikiwa na Mungu hakuna mwanadamu wa kumshusha hapo alipo, na haya alikua anaongea kanisani mbele ya waamini na kujitapa kabisa.

Kwa sisi waamini wachache ambao tulikua tunamuona kanisani na kutambua madhaifu yake tulijua hana mda mrefu atapigwa chini na kweli leo kaondoka.

Wengi mnaongea hamjui kilicho nyuma ya huyu kimaro ila nakuhakikishia KKKT KIJITONYAMA haiwezi kutetereka kisa kimaro kuondolewa na alishasema akitolewa Kjitonyama basi ataanzisha kanisa lake, ngoja nione atakachofanya baada ya hili.

Namuombea hekima na maarifa atambue kosa lake arudi kundini na awe mnyenyekevu kwa Mungu na Viongozi na Kanisa kwa ujumla.

ANAYEFATA NI MASAI WA KIMARA MWISHO.
Siku wakimng'oa huyo jamaa wa Kimara Korogwe ndo nitaona wako serious, maana pale kashajimilikisha usharika.
 
Kwenye hili nahisi pastor kimaro ataenda kujitafakari.

Mimi ni muumini wa KKKT hapo kijitonyama, shida iliyokuwepo kwa mchungaji kimaro ni kwamba alikua anaenda kinyume na utaratibu wa kanisa na kibaya zaidi alisha onywa zaidi ya mara 3 ila shida yake akiitwa akaonywa anakuja kanisani anaanza kuongea kwa waamini na kurusha vijembe kwa viongozi wake.

Tarehe 8 ukiweza fatilia alichokifanya kwa pastor mwenzake ANNA maneno aliyoongea kumuhusu huyo mchungaji kuna jambo utaelewa.

Kimaro ana kiburi cha umaarufu
Mchungaji hafati kalenda ya kanisa, yeye anafanya mambo yake, aliitwa akaonywa ila akaja kanisani hadharani na kusema hawezi kupangiwa cha kufanya ila Mungu tu, sasa hapo kweli kuna utii?

Kimaro toka amekuja usharikani anazo nyimbo 6 tu anazo imba kutoka kitabu cha tumwabudu Mungu wetu, aliitwa akaambiwa hiki kitu ila akawa mkaidi, ni mchungaji anayependa yeye aongee zaidi, hapendi kuwapa wachungaji wengine nafasi ya kuhubiri, ikitokea mchungaji mwingine akahubiri basi na yeye baada ya mahubiri atasimama na kuanza kujazilishia kuonekana kwamba mwenzake hajafanya kama inavyo paswa.

Ni kimaro na masai wa kimara ambao ukifatilia utaratibu wanao ufanya kanisani siyo wa kkkt ila najua wachache sana wataelewa hili.

Kama mtawna alishasema akitolewa Kjitonyama basi ataanzisha kanisa lakeeza kumbuka pia aliondolewa kwenye vipindi vya upendo Tv kisa mambo yake hayo ya kufanya kinyume na utaratibu wa kanisa ikabidi wamuonye ila akakaidi, baada ya kuondolewa alikuja kanisani hadharani na kuanza kusimanga na kuongea mbovu na tokea hapo hajawahi kutangaza kitu chochote kinacho husu upendo kama magazeti.

Alitamba sana kwamba kwa jinsi alivyo barikiwa na Mungu hakuna mwanadamu wa kumshusha hapo alipo, na haya alikua anaongea kanisani mbele ya waamini na kujitapa kabisa.

Kwa sisi waamini wachache ambao tulikua tunamuona kanisani na kutambua madhaifu yake tulijua hana mda mrefu atapigwa chini na kweli leo kaondoka.

Wengi mnaongea hamjui kilicho nyuma ya huyu kimaro ila nakuhakikishia KKKT KIJITONYAMA haiwezi kutetereka kisa kimaro kuondolewa na alishasema akitolewa Kjitonyama basi ataanzisha kanisa lake, ngoja nione atakachofanya baada ya hili.

Namuombea hekima na maarifa atambue kosa lake arudi kundini na awe mnyenyekevu kwa Mungu na Viongozi na Kanisa kwa ujumla.

ANAYEFATA NI MASAI WA KIMARA MWISHO.
.....na alishasema akitolewa Kjitonyama basi ataanzisha kanisa lake.

Labda hii ndio sababu ya kukaidi maonyo ya mara kwa mara maana alishajiona amekuwa maarufu na kuwa na uhakika wa kujipatia waumini wa kutosha watakao kidhi mahitaji yake.
 
Kwamba si mtii si kweli, hata kusimamishwa ametii hadharani na ame address viongozi wake kwa heshima zote. Hapo naona umetoa allegations nyingi za uongo ingawa mimi si muumini wa Lutheran!

Kusema hafati ratiba ya Kanisa si kweli, sema huwa anakuwa na ratiba za ibada ya huduma yake nje ya litrujia ya kawaida mfano mafungo maalum.

Huyu mchungaji ana kundi kubwa la watu ambao hata si walutheri, hiyo pekee ni huduma na Kanisa lingepaswa kumsaidia kumlea ili aweze kuhudumia hao. Hata Mwakasege ambaye ni Mlutheri injili yake haina mipaka ndio maana pamoja na kutii ibada ya Kanisa lake lakini ana huduma yake.

Nafikiri Mchungaji Kimaro hajapata Askofu wa kuelewa huduma yake, wanataka awe kawaida afanye huduma kama kila mchungaji.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Well said
 
.....na alishasema akitolewa Kjitonyama basi ataanzisha kanisa lake..... Labda hii ndio sababu ya kukaidi maonyo ya mara kwa mara maana alishajiona amekuwa maarufu na kuwa na uhakika wa kujipatia waumini wa kutosha watakao kidhi mahitaji yake.
Hata CDM ilizaliwa baada ya kuteswa na chama kimoja
 
Back
Top Bottom