Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu

Kweli yaani hata mimi ilikua naelekea ubungo kusali maana kijitonyam a ulianza kua upuuxi hakuna ibada za kkkt
Hawa jamaa inabidi waondoshwe wote
 
Kuna wakatai alipata kashfa ya kunyakua mke wa mtu
Sijui iliishia wapi ile kashfa
 
Kama ndivyo, Askosfu Mwamakula yupo sahihi na Dayosisi wapo sahihi
 
Kweli kabisa jamaa anajiinua sana kupitiliza
 
Nanyi mnamatatizo sana, mlichosahau tu ni kuwa yeye pia ni Binadamu anaweza kuwa na mapungufu yake lakini anakpawa cha ufundishaji na kanisa limestawi.

Hayo mapungufu uliyoyaongea ni madogo sana sio sawa kumsimamisha kazi ya uchungaji
Hajasimamishwa uchungaji ila kapewa likizo na nina imani likizo hiyo atakua chini ya mafundisho ili akirudi kazini asirudie hayo madhaifu

Alafu kwani ni lazima abaki kijitonyama? Si anaweza kupelekwa hata kibamba huko si kanisa hilo pia?

Sema watu wanashabikia hawajui mambo ya kkkt na utaratibu wake, ukienda kinyume na kanisa unapewa onyo ukikaidi unatolewa kabisa
Nimesema hapo juu kwamba jamaa alionywa mara nyingi ila kiburi tu na kujiona mkubwa ndicho kinacho mponza
 
Kabisa kabisa sema watu hawaelewi hii kitu
 
Sasa si muumini wa hapo tulia
Waumini wamesema wana shida nae?


Hakuna kinachopambaniwa pale korogwe zaidi ya sadaka
Watu mpaka wanataka kuuana
Imebidi nicheke. Nimekumbuka kisa cha jamaa nayefahamiana naye alipewa kazi ya kusimamia uchaguzi wa Viongozi kwenye Dayosisi flani kubwa tu. Ila presha aliyokuwa akiipata mpaka anashangaa. Haamini kama 'Mzee flani' ana uroho kiasi hicho cha madaraka.

Hivi kwa Kimara ni kwamba Mastai ndiye mziba riziki pesa zisichukuliwe au naye ni mshirika ndiyo maana anaungwa mkono?
 
Huwe,i kuelewa hii kitu utaishia kutukana watu bila sababu ila ngoja ukweli utajitenga na uongo
 
Inaonekana mkuu na wewe ni mmoja wa wanaomfanyia figisu huyo mchungaji, eti unamuombea arudi kundini na awe mnyenyekevu kwa Mungu, kwahiyo ina maana yeye kazi anayoifanya ni kumtukuza shetani...!
Siku zote usipokua mnyenyekevu kwa mamlaka hata kwa Mungu wewe si mnyenyekevu
Mungu mwenyewe anaagiza tutii mamlaka zetu maana zina kibari kutoka kwake
 
Umesema vema kabisaa mamii.

Kimaro na Masai hawafuati kalenda kabisa.k

.....na alishasema akitolewa Kjitonyama basi ataanzisha kanisa lake.

Labda hii ndio sababu ya kukaidi maonyo ya mara kwa mara maana alishajiona amekuwa maarufu na kuwa na uhakika wa kujipatia waumini wa kutosha watakao kidhi mahitaji yake.
Aende akaanzishe la kwake azidi kua maarufu
 
tunamsubiri Kibwegere huku
 
Bila liturujia hukuna ladha ya ukkkt ,sema wew ujui kuimba liturijia ndio maana unaponda na kuona kuwa haifai

Pmj na kina mastai kufundisha vzr ila Ni lazma waanzage na liturujiaa Tena kwa heshima zote Kisha tunaimba nyimbo yetu kuu ya " njoooni tumsifu mungu wetu"

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…