Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu

Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu

Mimi nilikuwa sijui kinachoendelea hapo Kijitonyama ila ulivyoanza kuelezea tu kichwa changu kikaenda kwa Mchungaji Masai wa Kimara.

Nimesali pale Kimara mara moja moja nikimtembelea jamaa yangu, ni kweli ibada za pale sio za KKKT. Kuna siku ilibidi wenzangu waende pale mimi nikapitiliza nikaenda kusali Ubungo, niliwaambia mimi nimezoea ibada zetu za kilutheri hapo siwezi.
Kweli yaani hata mimi ilikua naelekea ubungo kusali maana kijitonyam a ulianza kua upuuxi hakuna ibada za kkkt
Hawa jamaa inabidi waondoshwe wote
 
Mimi nilikua nasali kkkt kila j2.. na nilikua nasali Kariakoo Kimaro akiwepo... Nilikuja kujua Askofu Malasusa amebadilisha katiba ili awe askofu milele nilichoka sana... Niligundua huyu askofu ni mroho na yupo kikaz sio kiroho nina miaka mitatu sijawahi kanyaga kanisani. Huyu askofu ana figisu sana na alikua karibu sana na mwenda kuzimu.. Kimaro anajituma sana anastahili kuwa juu na hayo matamshi yalikua ni mambo madogo tu ya kurekebishana.. yule ni binadamu anaeituma sana... iust imagine huamka toka Kimara hadi kanisani kwake saa 10 alfajiri kwa ajili ya morning glory
Kuna wakatai alipata kashfa ya kunyakua mke wa mtu
Sijui iliishia wapi ile kashfa
 
ASKOFU MWAMAKULA AZUNGUMZIA SUALA LA KUSIMAMISHWA KWA MCH. DKT. KIMARO

Taarifa za kupewa likizo na kusimamishwa kwa muda kwa Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Usharika wa Kijitonyama Mch. Dkt. Eliona Kimaro zimeanza kuenea katika mitandao ya kijamii na kuzua hisia nzito miongoni mwa waumini na wasio waumini wa KKKT. Kimaro ni miongoni mwa watu maarufu, hivyo suala hili haliwezi kuchukuliwa wepesi.

Hapa tumeweka tazamo wetu wa kitheologia ili kutoa mchango wetu katika hoja hii. Ni dhahiri kuwa misimamo binafsi ya Mch. Dkt. Kimaro imemtia katika misuguano mingi na uongozi wa KKKT kwa kipindi kirefu. Lakini, misimamo hiyo iliweza kuvumiliwa ndani ya KKKT na ndio maana alipewa kuongoza Usharika mkubwa katika Dayosisi ya Mashariki na Pwani.

Tumefuatilia kutoka kwa baadhi ya viongozi ndani ya Dayosisi ya Mashariki na kuelezwa kuwa matamshi ya Mch. Dkt. Kimaro aliyoyatoa hivi karibuni baada ya kutoka Marekani ndiyo yaliyopelekea uongozi wa Dayosisi kumuita na kumpa likizo ambayo imeibua hisia na mjadala mzito baada ya yeye Mch. Dkt. Kimaro kutoa hadharani jambo ambalo lilikuwa ni karipio la Kichungaji.

Kwa mujibu wa video iliyosambaa, Mch. Dkt. Kimaro amesikika akisema kuwa vijana wa Kikristo sio waaminifu bali vijana wa Kiislamu ndio waaminifu kuliko vijana wa Kikristo. Mch. Dkt. Kimaro amesikika pia akisema kuwa watu wote wanaosimama madhabahuni [Wainjilisti, Wachungaji na Maaskofu] ni matapeli na watu wote waliokaa kwenye viti [vya ibadani - Wazee wa Kanisa na waumini] ni matapeli pia. Mch. Dkt. Kimaro amekwenda mbali zaidi na kusema kuwa takwimu [hajataja ni takwimu gani na taasisi iliyotoa takwimu hizo] zinaeleza hayo aliyosema.

Kitheologia tunapata tafsiri kuwa Mch. Dkt. Kimaro hana imani na maadili ya Kikristo, hana imani na mafundisho ya Kikristo na pia hana imani hata na watumishi wenzake wote wa Kikristo kutoka madhehebu yote nchini Tanzania. Tafsiri hapa ni kuwa Mch. Dkt. Kimaro anaonesha kuwa ana imani na maadili ya Kiislamu, mafundisho ya Kiislamu na hata Mashehe wa Kiislamu. Pia, Mch. Dkt. Kimaro anaonesha kuwa hana imani pia na hata vijana wake wa Kikristo ndani ya KKKT na nje ya KKKT ambao siku zote yeye mwenyewe amekuwa akiwafundisha katika ibada, mikesha, semina, morning glory, bali ana imani kubwa na vijana wa Kiislamu ndio maana akawaajiri hao katika miradi yake.

Mtumishi ye yote (Mwinjilisti, Mchungaji/Padre au Askofu) kutoka katika madhehebu yetu ya Katholiko (RC, Moravian, Lutheran, Anglikana na Orthodox) akitoa kauli kama hizo, ni lazima aitwe na uongozi wake, ahojiwe na hata ikibidi achunguzwe. Hicho ndicho kilichotokea kwake Mch. Dkt. Kimaro kuitwa na uongozi wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani, kuhojiwa na kuchunguzwa. Kauli zake alizotoa zimepingana na imani, mafundisho na maadili ya Kikristo! Kauli ya Mch. Dkt. Kimaro hayakushambulia Ulutheri tu, bali kwa kujua au hata kutokujua, kauli yake ilishambuliwa Ukristo wote kwa ujumla katika nchi hii.

Kwa sababu hiyo, sisi Askofu tunatoa wito kwa waumini wote wa Kikristo nchini kuwa watulivu wakati KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani inashughulikia jambo la Mch. Dkt. Kimaro. Sisi tumelazimika kuandika baada ya kuona kuwa jambo hili limeanza kusambaa mitandaoni na kubeba hisia zaidi kuliko uhalisia na pengine kubeba upotofu mwingi zaidi kuliko ukweli.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula
Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki.
Kama ndivyo, Askosfu Mwamakula yupo sahihi na Dayosisi wapo sahihi
 
Unesema kweli mtumishi. Mimi siko ndani ya kkkt lakini nilikuwa nafuatilia mahubiri ya rev Kimaro. Mwanzoni nikimwelewa lakini baadaye nikiacha kumfuatilia baada ya kugundua kaingiwa na kiburi na ushabiki hasa mafundisho yake ya ndoa.

Anezidisha mwembembwe na washabiji zake wengi ni wanawake. Pia hudharau wachungaji wenzake.
Kweli kabisa jamaa anajiinua sana kupitiliza
 
Nanyi mnamatatizo sana, mlichosahau tu ni kuwa yeye pia ni Binadamu anaweza kuwa na mapungufu yake lakini anakpawa cha ufundishaji na kanisa limestawi.

Hayo mapungufu uliyoyaongea ni madogo sana sio sawa kumsimamisha kazi ya uchungaji
Hajasimamishwa uchungaji ila kapewa likizo na nina imani likizo hiyo atakua chini ya mafundisho ili akirudi kazini asirudie hayo madhaifu

Alafu kwani ni lazima abaki kijitonyama? Si anaweza kupelekwa hata kibamba huko si kanisa hilo pia?

Sema watu wanashabikia hawajui mambo ya kkkt na utaratibu wake, ukienda kinyume na kanisa unapewa onyo ukikaidi unatolewa kabisa
Nimesema hapo juu kwamba jamaa alionywa mara nyingi ila kiburi tu na kujiona mkubwa ndicho kinacho mponza
 
One ...mother

Nimekuelewa asilimia Mia 100 umenena Kweli tupu jamaaa wamejawa kiburii mafundisho yake ma mastai hayana tofauti kbsa wao hawafati kalenda Wala taratibu za ibada za kkkt

Sina tatizo nae kwenye mahubiri Yao ila kujikweza kwaoo hapna kwa Kweli Ni wasi kbsa jamaaa wamejawa kiburii na kujiona wao ndio wamefanya mapinduzi ya ukkkt DMP

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Kabisa kabisa sema watu hawaelewi hii kitu
 
Sasa si muumini wa hapo tulia
Waumini wamesema wana shida nae?


Hakuna kinachopambaniwa pale korogwe zaidi ya sadaka
Watu mpaka wanataka kuuana
Imebidi nicheke. Nimekumbuka kisa cha jamaa nayefahamiana naye alipewa kazi ya kusimamia uchaguzi wa Viongozi kwenye Dayosisi flani kubwa tu. Ila presha aliyokuwa akiipata mpaka anashangaa. Haamini kama 'Mzee flani' ana uroho kiasi hicho cha madaraka.

Hivi kwa Kimara ni kwamba Mastai ndiye mziba riziki pesa zisichukuliwe au naye ni mshirika ndiyo maana anaungwa mkono?
 
Hana lolote huyo!

Ukimsoma vizuri kwa utulivu utagundua yeye Kuna mawili;
1. Ama ndiye Mchungaji Anna
Au
2. Ni wale wanafiki na mahasidi wa kanisa.

Wachawi nao wanasali makanisani!

Lakini Pastor Kimaro kama mmemuonea mjue Mungu anaenda kumuinua zaidi.

Roho wa Mungu ampe subira na hekima kuvuka jaribu hilo.

Ikimpendeza Roho namshauri afanye kama huduma ya Mwakasege.

Au aanzishe kanisa .
Huwe,i kuelewa hii kitu utaishia kutukana watu bila sababu ila ngoja ukweli utajitenga na uongo
 
Inaonekana mkuu na wewe ni mmoja wa wanaomfanyia figisu huyo mchungaji, eti unamuombea arudi kundini na awe mnyenyekevu kwa Mungu, kwahiyo ina maana yeye kazi anayoifanya ni kumtukuza shetani...!
Siku zote usipokua mnyenyekevu kwa mamlaka hata kwa Mungu wewe si mnyenyekevu
Mungu mwenyewe anaagiza tutii mamlaka zetu maana zina kibari kutoka kwake
 
Umesema vema kabisaa mamii.

Kimaro na Masai hawafuati kalenda kabisa.k

.....na alishasema akitolewa Kjitonyama basi ataanzisha kanisa lake.

Labda hii ndio sababu ya kukaidi maonyo ya mara kwa mara maana alishajiona amekuwa maarufu na kuwa na uhakika wa kujipatia waumini wa kutosha watakao kidhi mahitaji yake.
Aende akaanzishe la kwake azidi kua maarufu
 
Hajasimamishwa uchungaji ila kapewa likizo na nina imani likizo hiyo atakua chini ya mafundisho ili akirudi kazini asirudie hayo madhaifu
Alafu kwani ni lazima abaki kijitonyama? Si anaweza kupelekwa hata kibamba huko si kanisa hilo pia?
Sema watu wanashabikia hawajui mambo ya kkkt na utaratibu wake, ukienda kinyume na kanisa unapewa onyo ukikaidi unatolewa kabisa
Nimesema hapo juu kwamba jamaa alionywa mara nyingi ila kiburi tu na kujiona mkubwa ndicho kinacho mponza
tunamsubiri Kibwegere huku
 
KANISA NI MALI YA MUNGU, sio saccos za KKKT. Mungu huabudiwa kwa roho, na kanisa halisi la Mungu lazima litoe solutions za matatizo ya waumini wake through maombi, na mafundisho yenye uzima. Zama za kufuatisha liturugia mpaka watu wanasinzia zimekwisha. Nawaunga mkono hawa pastors Kimaro na mastai at least wameleta uhai kwenye ibada za KKKT.
Kama kweli wanafanya hayo kwa ajili ya Kristo, hata wakiwatimua halafu wakaamua kuwa na huduma zao still watapata followers wa kutosha.
Bila liturujia hukuna ladha ya ukkkt ,sema wew ujui kuimba liturijia ndio maana unaponda na kuona kuwa haifai

Pmj na kina mastai kufundisha vzr ila Ni lazma waanzage na liturujiaa Tena kwa heshima zote Kisha tunaimba nyimbo yetu kuu ya " njoooni tumsifu mungu wetu"

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom