Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu

Hili la majigambo hâta mie nliona kitambo tu, na lilikuwa linanishangaza sana!!
 
Ndugu, unazungumziaje makosa yake yanayosemwa kuhusu kuwa kinyume na taratibu za kimisa za kilutheri..? Naona jamaa (uongozi KKKT) wanaweza kushikia bango hapo.
 
Hahahahahah sema mlimkamia sana wazee... Kwahio sahizi bahari itatulia sasa
 
Tumelijua hilo, ndio maana wengine tumazamia ktk maombi, ila mjue hata mkimtoa hapo... Bado uharibifu utaendelea tu maana Mungu kawekeza tayari😁😁
 
Daaaaa[emoji15][emoji15]..
Hv n kweliiii....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo tatizo ni lile lile tu la ngozi nyeusi, wivu, majungu na fitina. Jamaa nyota yake imewaka na anakubalika sana na ukishakubalika na jamii hela lazma upate nyingi tu kupitia hao hao unaowahudumia. Sasa naona wamejaribu kumbana bana wamemshindwa wameona anafaidi sana bora wamuondoe kisiasa.
 
Aanzishe ministry yake tu huwezi ukawa perfect na ukategemea kusurvive kwenye haya makanisa ya kimchongo.
Sio kanisani tu popote pale nchini, ukiwa na balls jiandae kuishi kama tai maana kila mahali watakuwa wanakuona mkorofi. Watanzania tumezoeshwa ukondoo toka nchi hii inaasisiwa.

1.Shuleni ufanyiwe uonevu ukae kimya, ukikaza unaonekana mtukutu. Utahamishwa tu.

2.Kazini ukiwa mshapu na mtoaji ideas utaitwa kiherehere tayari watu wanakuchukia. Huwezi toboa.

3. Uraiani ukitoa views zako kuhusu hali ya maisha nchini. Mchochezi. Hapo hapo una haki ya kutoa mawazo yako. Ila unaitwa mchochezi.

4.Kanisani kama hivyo, una kipaji cha neno na watu wanakupenda unasimamia ukweli. Unaambiwa unakiuka taratibu.

Hii ndio Tanzania, ukiwa na misimamo yako binafsi basi hakikisha hufungamani na taasisi yeyote.
 
Ndio ukweli wenyewe hata kama hautaki, its either uwe RC ama Muislamu ndio dini zinazotambulika kitaifa. Official religions of the nation.
 

Kimaro hakuwa specific yeye ali generalize kitu ambacho mimi naona siyo kweli huwezi ukasema wakristo wote ni wezi,basi hata magereza nafikiri yangejaaa Christian tuu
 
Kiufupi huyu Kimaro ameamua ku Mordenize kanisa la KKKT kutoka kwenye old and boring formula ya liturujia tu. Watu sikuhizi wanafocus zaidi kwenye vibe. Vizazi vimebadilika sana vijana wengi wanaohudhuria hizo ibada ni uzao wa kuanzia mwaka 2000.
Mindset zipo tofauti na wazazi wao sio watu wa miaka ya 60 au 70 kama baba zetu.
 
UMEZUNGUMZIA UTARATIBU WA WAKUBWA. HAPO HAPO TU ULISHAMALIZA KILA KITU. KILA TAASISI INA UTARATIBU WAKE. USIPOFUATA UTAONA UNAONEWA.
Ni kweli tumeona hata EFM yule mtangazaji amefukuzwa kazi kwa kutoa maoni yake tu dhidi ya hali ya nchi inavyokwenda.

Katiba inasema kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni na haija specify sehemu gani exactly mtu atoe hayo maoni. Ingeandika maoni yatolewe chooni kwako au chumbani kwako ingekuwa rahisi kumhukumu yule mtu.

Hio ndio hali ya Tanzania ilipofikia halafu tunakazi ya kulaumu kwanini watu wengi wamekuwa na tabia ya unafiki. Misingi ya maisha imejikita kwenye unafiki leo hii huwezi kusema ukweli wako wazi ila lazma uangalie huo ukweli unamwambia nani. This is not how its supposed to be.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…