Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu


Ndio aende huko nje akafanye anachotaka. Wewe kijakazi wa nyumba unataka uweke taratibu zako kwenye nyumba ya mwajiri. Aende na washirika wake huko nje ya KKKT.
 
Kimaro alishainuliwa na Mungu huyo..
Hakuna atakayemshusha.
Mungu ana sifa ya kujipambania mwenyewe .

Peleka huo ushauri kwa kijitonyama.
Mimi si mlutheri na wala sipo kijitonyama.

Nyie ndio mnaoleta fujo kwenye issue ya kimaro. Wewe sio KKKT lakini mambo ya Kimaro unayashadadia. Wote wale wanaaandamana sio KKKT ni wahuni kutoka nje. Ndio maana Sasa hivi utaratibu upo wa kuhakiki washirika wa kijitonyama. Ambao siyo washirika wamekaa nje kwa aibu.
 
Mara zote nasema sio vizuri kudakia jambo na kuanza kulaumu upande mmoja. Ni vyema kuwa watulivu na kusikiliza pande zote. Siku zote muda ni jibu sahihi kwa kila jambo. Asante mwandishi kwa kutufungua macho kwa upande huo. Wacha tuendelee kusikiliza huenda upande wa kimaro nao watanena neno kisha tuanze kutathmini yapi ni makapi na zipi ni ngano.
Ubarikiwe
 

Amepewa Likizo baada ya kikao na Msaidizi wa Askofu. Wakakubaliana aende likizo kwanza. Kwa jeuri kaja kulilia washirika kanisani.
 

Kama ni habari ya mjini aende huko akafungue kanisa na wale wanawake wavaa suruali za kubana.
 
Yaani Bina usije kushangaa huko motoni wengi wakawa wakristo, tena viongozi na hawa wenye makasiriko na mtu aliyeinuliwa na Mungu.

Mbinguni ni matendo yako sio Ukristo wala uislamu. Mtu kaja kuchochea uasi kwa nini asiambiwe umweli. Kuinuliwa na Mungu ndio Nini?. Mbona Mwakasege kainuliwa miaka Sasa zaidi ya 30 lakini kajishusha kanisani, na jumapila anakaa benchi kusikiliza mafundisho. Sembuse Kimaro motivational speaker
 
Daahhhh nimechoka sana Bina maana ukiona comments za humu za chuki za wazi wazi as if alikua anazibia watu riziki,amekula wake za watu au ametukana watu,au ameiba pesa
Mapungufu madogo yakibinidamu Ndo yananyomfanya humu watu wamshambulie looh

Kuita vijana wa kikristo in General kuwa sio waaminifu alikuwa haoneshi chuki. Hakuna chuki kwa Kimaro Bali anavuna alichopanda. Yeye mwenyewe alisimamishwa Kariakoo miezi miwili baada ya kugundua kuwa alifoji cheti.
 

Unafiki zaidi wa Kimaro? Huyu kimaro aliyesimamishwa KKKT Kariakoo kwa kufoji cheti?. Usifanye watu wakafukua makaburi. Kafungueni kanisa mkae kwa amani.
 

Hiyo semina kapanga akijua atapewa likizo. Huyo angeondoka tu akafanye semina zake nje ya KKKT.
 
KKKT wanamtania Mungu.
Mungu ameandaa semina kupitia mtumishi wake,wanaibuka watu kuitengua.
Mimi nipo na hili tu.
Mungu hadhihakiwi.

Mchungaji kaanda semina Kama mtego akijua anaweza simamishwa muda wowote. Wewe unadhani alifanya kwa bahati mbaya?. Alipanga. Nachofurahi, KKKT DMP wapo kimya, maana wakiongea Kuna watu watajoficha.
 
Yule alijitengeneza na akajua hawezi ondolewa , maana kashapata jina.
Kiburi, huyo wanaosema angeonywa kwa upole wamtafute wamuulize ameonywa mara ngapi na hakusikia.

Kama itafika wakati uongozi wa kanisa uogope kusimamia misingi yake kisa umaarufu wa mtu, itakuwa hatari sana kwa kesho ya taasisi.

KKKT iweke utaratibu wa kuwahamisha wachungaji kila wanapotimiza mwaka mmoja wa huduma katika usharika filani, hii itasaidia sana Mchungaji kutoona kama anawamiliki waamini wa usharika fulani.

Inashangaza sana mchungaji anahamishwa sehemu anaona kama ameonewa hadi analia katika hali ya kusingizia anaomba, inatia shaka kuna nini hapo anapoondoka?
 
Mkuu hujakosea kabisa ila huwa kama unanifuatilia kwa makini utakuja kugundua kuwa hoja ya mtoa mada ndio huwa inani guide kutoa response ya aina gani.

Hoja ya kipuuzi itajibiwa kipuuzi tu, kitu sensible kitajibiwa with highest degree of sanity.
[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
 
1. Hivi nyoote mnaomhukumu Kimaro, na kutoa maelezo kwamba kajiinua, kadharau viongozi wake, n.k. mlikuwa kwenye kikao chake na huyo msaidizi wa askofu mkasikia kilichozungumzwa?

2. Hivi, mnaposema mchungaji ni "mtumishi wa Mungu" lakini LAZIMA atii mamlaka zilizopo, mchungaji husika akiona mamlaka husika kwenye kanisa lake zinaenda kinyume na neno la Mungu, atii tu hata kama viongozi wake hawako sawa?

3. Kama kanisa ni MALI YA MUNGU, kwa nini viongozi wasimshirikishe Mungu KABLA ya kufanya maamuzi yanayohusu kiongozi yeyote wa kanisa hilo? Kwa nini wameweka taratibu ya viongozi wa juu (yaani askofu na wasaidizi wake) ndio waamue jambo lolote bila kushirikisha viongozi wa kanisa alilopo huyo kiongozi? Kanisa la Kijitonyama lina baraza lake la wazee. Lina waumini wake. Linao pia watu waliobobea katika mambo ya kijamii na kisheria.

Kwa nini ofisi ya askofu na wasaidizi wake waamue jambo bila kushirikisha baraza la wazee na hao wengine wenye hekima hapo Kijitonyama? Kwa nini wasitake hilo baraza la wazee na wenye hekima na hata waumini wengine WAMWOMBE MUNGU kabla ya kumchukulia hatua za nidhamu mchungaji yeyote?

4. Wengi wenu mmesema kila kanisa lina taratibu zake. Kama hizo taratibu HAZIMSHIRIKISHI MUNGU (kwa maombi) kabla ya kufanya maamuzi mnaona ni sawa?

Mchungaji au padri ANAPEWA WITO NA MUNGU KWANZA ndipo anaenda seminari na shule ya uchungaji. Na ni Mungu mwenyewe anaweka mipango ili mchungaji fulani akae kwenye kanisa fulani (NDIPO WAKUU WA KANISA WANAMWEKA KWENYE KANISA WALIOAMUA).

Ni kosa kubwa sana kumwadhibu mchungaji au mtumishi wa Mungu yeyote yule BILA KUMSHIRIKISHA MUNGU KWA MAOMBI.

Naomba mkiweza, wapelekeeni ofisi ya askofu na watu wake hili post waisome. Wajipime kama kweli walifuata kanuni za Mungu kumwadhibu Kimaro (hata kama amefanya makosa makubwa sana).

Kwani, nyie wote mnaosoma hii post si mnajua baadhi ya mapungufu ya viongozi wa kanisa? Na Wakristo mnajua Yesu alisema USIHUKUMU maana utahukumiwa?

Na kila mmoja wenu si anajua anatakiwa amsamehe aliyemkosea SABA MARA SABINI?
 
Alijitapaje alionesha dharau gani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…