Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu

Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu

Eti kufuata Calendar
Shetani anapanga na kupangua mbinu kila siku, nyie mmekaa mmeshikilia Calendar.

Maombi ya asubuhi na jioni,na semina
Ndivyo vinavyowafanya waseme amekiuka taratibu.
Hivi kuimba,kuomba na kujifunza neno ni dhambi??
KKKT wana moto wao special aisee.

Ndio aende huko nje akafanye anachotaka. Wewe kijakazi wa nyumba unataka uweke taratibu zako kwenye nyumba ya mwajiri. Aende na washirika wake huko nje ya KKKT.
 
Kimaro alishainuliwa na Mungu huyo..
Hakuna atakayemshusha.
Mungu ana sifa ya kujipambania mwenyewe .

Peleka huo ushauri kwa kijitonyama.
Mimi si mlutheri na wala sipo kijitonyama.

Nyie ndio mnaoleta fujo kwenye issue ya kimaro. Wewe sio KKKT lakini mambo ya Kimaro unayashadadia. Wote wale wanaaandamana sio KKKT ni wahuni kutoka nje. Ndio maana Sasa hivi utaratibu upo wa kuhakiki washirika wa kijitonyama. Ambao siyo washirika wamekaa nje kwa aibu.
 
Kwenye hili nahisi pastor Kimaro ataenda kujitafakari.

Mimi ni muumini wa KKKT hapo Kijitonyama, shida iliyokuwepo kwa mchungaji Kimaro ni kwamba alikuwa anaenda kinyume na utaratibu wa kanisa na kibaya zaidi alishaonywa zaidi ya mara 3 ila shida yake akiitwa akaonywa anakuja kanisani anaanza kuongea kwa waamini na kurusha vijembe kwa viongozi wake.

Tarehe 8 ukiweza fatilia alichokifanya kwa pastor mwenzake ANNA maneno aliyoongea kumuhusu huyo mchungaji kuna jambo utaelewa.

Kimaro ana kiburi cha umaarufu. Mchungaji hafati kalenda ya kanisa, yeye anafanya mambo yake, aliitwa akaonywa ila akaja kanisani hadharani na kusema hawezi kupangiwa cha kufanya ila Mungu tu, sasa hapo kweli kuna utii?

Kimaro toka amekuja usharikani anazo nyimbo 6 tu anazoimba kutoka kitabu cha tumwabudu Mungu wetu, aliitwa akaambiwa hiki kitu ila akawa mkaidi, ni mchungaji anayependa yeye aongee zaidi, hapendi kuwapa wachungaji wengine nafasi ya kuhubiri, ikitokea mchungaji mwingine akahubiri basi na yeye baada ya mahubiri atasimama na kuanza kujazilishia kuonekana kwamba mwenzake hajafanya kama inavyopaswa.

Ni kimaro na masai wa kimara ambao ukifatilia utaratibu wanao ufanya kanisani siyo wa KKKT ila najua wachache sana wataelewa hili.

Kama mtaweza kumbuka pia aliondolewa kwenye vipindi vya upendo Tv kisa mambo yake hayo ya kufanya kinyume na utaratibu wa kanisa ikabidi wamuonye ila akakaidi, baada ya kuondolewa alikuja kanisani hadharani na kuanza kusimanga na kuongea mbovu na tokea hapo hajawahi kutangaza kitu chochote kinacho husu upendo kama magazeti.

Alitamba sana kwamba kwa jinsi alivyo barikiwa na Mungu hakuna mwanadamu wa kumshusha hapo alipo, na haya alikua anaongea kanisani mbele ya waamini na kujitapa kabisa.

Kwa sisi waamini wachache ambao tulikua tunamuona kanisani na kutambua madhaifu yake tulijua hana mda mrefu atapigwa chini na kweli leo kaondoka.

Wengi mnaongea hamjui kilicho nyuma ya huyu kimaro ila nakuhakikishia KKKT KIJITONYAMA haiwezi kutetereka kisa kimaro kuondolewa na alishasema akitolewa Kjitonyama basi ataanzisha kanisa lake, ngoja nione atakachofanya baada ya hili.

Namuombea hekima na maarifa atambue kosa lake arudi kundini na awe mnyenyekevu kwa Mungu na Viongozi na Kanisa kwa ujumla.

ANAYEFATA NI MASAI WA KIMARA MWISHO.
Mara zote nasema sio vizuri kudakia jambo na kuanza kulaumu upande mmoja. Ni vyema kuwa watulivu na kusikiliza pande zote. Siku zote muda ni jibu sahihi kwa kila jambo. Asante mwandishi kwa kutufungua macho kwa upande huo. Wacha tuendelee kusikiliza huenda upande wa kimaro nao watanena neno kisha tuanze kutathmini yapi ni makapi na zipi ni ngano.
Ubarikiwe
 
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 Kwanini huyo kiongozi asiongee na Mungu ili amrekebishe mtumishi mwenzie Kimario aache kuwapiga spana. Kwanini asingetumia njia hio instead of kumpa likizo bila kuomba.

Ukichunguza zaidi utakuta ni wivu wa kike tu. Yale yale ya yule kiwete wa ubelgiji kuleta fyoko fyoko hadi alipopatiwa dawa 🤣🤣🤣 halafu akaanza kulia lia kuwa kaonewa.

Amepewa Likizo baada ya kikao na Msaidizi wa Askofu. Wakakubaliana aende likizo kwanza. Kwa jeuri kaja kulilia washirika kanisani.
 
Kibri kipi bwana ukweli chuki tu ukweli usemwe Kimaro Ndo habari ya mjini tukubali tukatae Mimi ujue sikosagi vipindi vyake nikipata nafasi anatia faraja yule anafundisha nadhani wameogopa anawaoutshine Sanaa viongozi.

Kuhusu picha ni vitu vidogo tafsiri zao Ndo zao yeye ukute hamaanishi wanavomaanisha. Ni wivu tu hakuna lingine wanadamu wanaangalia kitu kidogo sana Ndo wanakibeba kuliko mema yake

Si wangesubiri amalize semina kama wao Wana hofu na Mungu kweli!mtu amejipanga halafu mnamkatisha palipo na riziki hapakosi fitna.

KKKT wamefeli Kwa hili

Kama ni habari ya mjini aende huko akafungue kanisa na wale wanawake wavaa suruali za kubana.
 
Yaani Bina usije kushangaa huko motoni wengi wakawa wakristo, tena viongozi na hawa wenye makasiriko na mtu aliyeinuliwa na Mungu.

Mbinguni ni matendo yako sio Ukristo wala uislamu. Mtu kaja kuchochea uasi kwa nini asiambiwe umweli. Kuinuliwa na Mungu ndio Nini?. Mbona Mwakasege kainuliwa miaka Sasa zaidi ya 30 lakini kajishusha kanisani, na jumapila anakaa benchi kusikiliza mafundisho. Sembuse Kimaro motivational speaker
 
Daahhhh nimechoka sana Bina maana ukiona comments za humu za chuki za wazi wazi as if alikua anazibia watu riziki,amekula wake za watu au ametukana watu,au ameiba pesa
Mapungufu madogo yakibinidamu Ndo yananyomfanya humu watu wamshambulie looh

Kuita vijana wa kikristo in General kuwa sio waaminifu alikuwa haoneshi chuki. Hakuna chuki kwa Kimaro Bali anavuna alichopanda. Yeye mwenyewe alisimamishwa Kariakoo miezi miwili baada ya kugundua kuwa alifoji cheti.
 
Ukiwauliza wengi wanafata tu mkumbo kumchukua baba wa watu [emoji1787]
Ila Mungu alishamuinua, watazidi kudhalilika tu.

Makanisani huku unafiki ni mwingi.. unakuta mtumishi badala ahubiri injili yake, unakuta yupo busy kumsagia kunguni mtumishi mwingine wa dhehebu jingine.

Unafiki zaidi wa Kimaro? Huyu kimaro aliyesimamishwa KKKT Kariakoo kwa kufoji cheti?. Usifanye watu wakafukua makaburi. Kafungueni kanisa mkae kwa amani.
 
Halafu anatokea mtu anakuambia ooh Kimaro ana kiburi
Kwanini apost picha imeandikwa from bitter to better[emoji16]

Kitendo tu cha kumpa likizo katikati ya semina ni kitendo Cha kijuha na kishetani.
Wakristo wengi tunaelewa, namna maandalizi ya semina yalivyo..
Mtu anakatishwa ghafla tu
Wamewazuilia watu ambao pengine wangeokoka na wangepiga hatua kwenye hiyo semina.
Wallah watatoa hasabu yake.

Hiyo semina kapanga akijua atapewa likizo. Huyo angeondoka tu akafanye semina zake nje ya KKKT.
 
KKKT wanamtania Mungu.
Mungu ameandaa semina kupitia mtumishi wake,wanaibuka watu kuitengua.
Mimi nipo na hili tu.
Mungu hadhihakiwi.

Mchungaji kaanda semina Kama mtego akijua anaweza simamishwa muda wowote. Wewe unadhani alifanya kwa bahati mbaya?. Alipanga. Nachofurahi, KKKT DMP wapo kimya, maana wakiongea Kuna watu watajoficha.
 
Yule alijitengeneza na akajua hawezi ondolewa , maana kashapata jina.
Kiburi, huyo wanaosema angeonywa kwa upole wamtafute wamuulize ameonywa mara ngapi na hakusikia.

Kama itafika wakati uongozi wa kanisa uogope kusimamia misingi yake kisa umaarufu wa mtu, itakuwa hatari sana kwa kesho ya taasisi.

KKKT iweke utaratibu wa kuwahamisha wachungaji kila wanapotimiza mwaka mmoja wa huduma katika usharika filani, hii itasaidia sana Mchungaji kutoona kama anawamiliki waamini wa usharika fulani.

Inashangaza sana mchungaji anahamishwa sehemu anaona kama ameonewa hadi analia katika hali ya kusingizia anaomba, inatia shaka kuna nini hapo anapoondoka?
 
Mkuu hujakosea kabisa ila huwa kama unanifuatilia kwa makini utakuja kugundua kuwa hoja ya mtoa mada ndio huwa inani guide kutoa response ya aina gani.

Hoja ya kipuuzi itajibiwa kipuuzi tu, kitu sensible kitajibiwa with highest degree of sanity.
[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
 
1. Hivi nyoote mnaomhukumu Kimaro, na kutoa maelezo kwamba kajiinua, kadharau viongozi wake, n.k. mlikuwa kwenye kikao chake na huyo msaidizi wa askofu mkasikia kilichozungumzwa?

2. Hivi, mnaposema mchungaji ni "mtumishi wa Mungu" lakini LAZIMA atii mamlaka zilizopo, mchungaji husika akiona mamlaka husika kwenye kanisa lake zinaenda kinyume na neno la Mungu, atii tu hata kama viongozi wake hawako sawa?

3. Kama kanisa ni MALI YA MUNGU, kwa nini viongozi wasimshirikishe Mungu KABLA ya kufanya maamuzi yanayohusu kiongozi yeyote wa kanisa hilo? Kwa nini wameweka taratibu ya viongozi wa juu (yaani askofu na wasaidizi wake) ndio waamue jambo lolote bila kushirikisha viongozi wa kanisa alilopo huyo kiongozi? Kanisa la Kijitonyama lina baraza lake la wazee. Lina waumini wake. Linao pia watu waliobobea katika mambo ya kijamii na kisheria.

Kwa nini ofisi ya askofu na wasaidizi wake waamue jambo bila kushirikisha baraza la wazee na hao wengine wenye hekima hapo Kijitonyama? Kwa nini wasitake hilo baraza la wazee na wenye hekima na hata waumini wengine WAMWOMBE MUNGU kabla ya kumchukulia hatua za nidhamu mchungaji yeyote?

4. Wengi wenu mmesema kila kanisa lina taratibu zake. Kama hizo taratibu HAZIMSHIRIKISHI MUNGU (kwa maombi) kabla ya kufanya maamuzi mnaona ni sawa?

Mchungaji au padri ANAPEWA WITO NA MUNGU KWANZA ndipo anaenda seminari na shule ya uchungaji. Na ni Mungu mwenyewe anaweka mipango ili mchungaji fulani akae kwenye kanisa fulani (NDIPO WAKUU WA KANISA WANAMWEKA KWENYE KANISA WALIOAMUA).

Ni kosa kubwa sana kumwadhibu mchungaji au mtumishi wa Mungu yeyote yule BILA KUMSHIRIKISHA MUNGU KWA MAOMBI.

Naomba mkiweza, wapelekeeni ofisi ya askofu na watu wake hili post waisome. Wajipime kama kweli walifuata kanuni za Mungu kumwadhibu Kimaro (hata kama amefanya makosa makubwa sana).

Kwani, nyie wote mnaosoma hii post si mnajua baadhi ya mapungufu ya viongozi wa kanisa? Na Wakristo mnajua Yesu alisema USIHUKUMU maana utahukumiwa?

Na kila mmoja wenu si anajua anatakiwa amsamehe aliyemkosea SABA MARA SABINI?
 
Unajua kibri kimemponza!
Tangu askofu, mkuu wa jimbo pamoja na wachungaji wenzake waende msibani kule kijijini jirani na kwake (baba mzazi wa mchungaji aman lyimo)alipofariki baadhi ya viongozi wengi waliendavkuzika walilala nyumbani kwake kule kijijini maana kimaro na huyu aman kwa kule kijijini wako karibu sana ni kama kilomita 2 hivi kwa kimaro na amani,sasa huyu kimaro kajijenga sana mpaka ndugu zake wote kawajengea mi block ya nguvu pale kijijini sasa kuanzia siku hiyo alianza kuleta dharau na kujitapa huenda hili nalo limechangia au huwezi jua ka wivu ka kipato kwa wakubwa huko
Alijitapaje alionesha dharau gani
 
Back
Top Bottom