Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu

Marehemu Moses Kulola aliondoka TAG na kundi kubwa la waumini na kuanzisha EAGT huku wakiamini TAG itakufa lakini mpaka leo TAG ipo na inazidi kusonga mbele.

Hivyo, hakuna mkuu kuliko Taasisi. Huyo Mch. Kimaro anyenyekee tu vinginevyo asipokuwa makini ndio mwanzo wa huduma yake kuharibika.
 
Ni upuuzi tu mkuu
 
Anaitwa Mastai.

Hawa jamaa wanaogopeka sana.

Alikuwa Richard Hanaja.
Eliona kimaro.
Na MASTAI.

Hawa jamaa Wana uwezo mkubwa lakini wapo chini ya kanisa. Shida wanaota mapembe.

Sikio linataka kuzidi Kichwa.
Ndo naulizwa kwann haguswi mastai anaguswa eliona??
 
Tena wengine uongozi wanaupata kwa njia za kishirikina na makafala, imagine kiongozi wa hivyo atafurahia kazi anayoifanya Pastor Kimario?
Waache laana inakuja nyuma yao, Maaskofu walioacha alama ya kutukuka ni
Sendoro - Madhariki na Pwani
Kibira - Kagera
Mwamasika - Dodoma
Uhahula - Kusini
Lukilo - Kusini
Kolowa - Tanga
Askofu wa kwanza Arusha namsahau jina
Askofu wa Kwanza Rungwe kama sijakosea Konde
 
Wewe ndiye umefunga mjadala.
Asante kwa taarifa nzuri


Hana lolote huyo!

Ukimsoma vizuri kwa utulivu utagundua yeye Kuna mawili;
1. Ama ndiye Mchungaji Anna
Au
2. Ni wale wanafiki na mahasidi wa kanisa.

Wachawi nao wanasali makanisani!

Lakini Pastor Kimaro kama mmemuonea mjue Mungu anaenda kumuinua zaidi.

Roho wa Mungu ampe subira na hekima kuvuka jaribu hilo.

Ikimpendeza Roho namshauri afanye kama huduma ya Mwakasege.

Au aanzishe kanisa .
 
Kama PETRO aligombana na PAULO itakuwa hawa wa kuja?
 
Kwenye hili nahisi pastor kimaro ataenda kujitafakari
Mimi ni muumini wa KKKT hapo kijitonyama, shida iliyokuwepo kwa mchungaji kimaro ni kwamba alikua anaenda kinyume na utaratibu...
Kama haya uliyosema yana ukweli basi huyo Pastor wenu Kimaro ni moumbavu na anatakiwa kushikidhwa adabu ila Kwa wajinga wale cheap mind wataona anaonewa gere.
Haitegemewi mtu awe mkubwa kuliko na kujiona Bora kuliko Taasisi.
 
Kama unayoongea ndiyo basi waumini wengi sana wataondoka KKKT.
 
Kwa hili nakuunga mkono Sana ila hata huyu aliyeanzisha kusifu na kuabudu kwenye ibada, ashughulikiwe. Kimaro alijaa majivuno, na niliwahi kusema humu ndani nikapingwa vibaya Hadi matusi.
Kusifu na kuabudu Ni Jambo jema kwani tunamsifu mungu na siyo kimaro

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Huyo Mch Anna inaonekana ndo alikuwa anamchongea sana achukue hiyo nafasi
 
Migogoro katika kanisa imeanza muda mrefu enzi za waanzilishi wa kanisa.
Kati ya wale wanafunzi wa yesu ambao ndio mwanzo wa kanisa ulianzia kwao nao walikuwa na mafarakano baina yao dhidi ya waamini...
Ume hitimisha vizuri sana hapo mwishoni.

Mwenzao anafanya kazi kubwa , maombi watu wanajibiwa matatizo yao yanaisha, wanapata maarifa sahihi,
Wagonjwa wanapata kupona, ndoa zinapona,

Anafundisha hadi watu wanaimarika kiimani na kuanza kutoa zaka kwa hiyari yao baada ya kuelewa mafundisho ya Neno,

Sasa mahasidi, wafitini , wachawi hawataki wanaona anafaidika sana.

Viongozi hayo hawayaoni badala yake wanaangalia maslahi yao .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…